Sunday 2 June 2013

Re: [wanabidii] KONGAMANO LA WAISILAMU JIJINI DAR, Sheikh Ponda aunguruma, Awasihi waisilamu kuwa na umoja, Nuru inakaribia.

--- On Sun, 6/2/13, Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] KONGAMANO LA WAISILAMU JIJINI DAR, Sheikh Ponda aunguruma, Awasihi waisilamu kuwa na umoja, Nuru inakaribia.
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, June 2, 2013, 6:54 PM

Matatizo mengi ya kuonekana dini fulani au kabila fulani linabaguliwa au kuonewa yataisha kama makabila na madhehebu hayo yatakazania elimu ya darasani yenye kupatia wanafunzi life skills. Sio kusoma dini tu. Pia, yatakuwa na malengo ya kujiendeleza kwenda na wakati. Mfano sio kuzurura na mifugo, kuchimba madini na kuoza visichana kuongeza mifugo uonekane tajiri-bali kufuga kisawa wachache bora, kuuza mazao yao, kusomesha na kuleta maendeleo ya familia. Kuwa na familia ndogo ya wafanyakazi waliojiri na kuajiriwa. Mungu nipe na mchele mkononi!! yaani-Sala ziende na ufanyaki kazi productively kwa maendeleo yako. Culture iende na maendeleo sio kinyume chake.

Muhimu dini yoyote kwa karne hii ni kuondoka utumwani. Ule uliokuja na waeneza dini walioitumia kutunyonya. Budi kuhimiza waumini kujituma, sio kukaa barazani tu, sio kuwa na mikesha ya sala bila ya kufanyakazi au kushinda kutwa unakwenda kusali sio kuzalisha mali. Ukisha kusali tumbo linataka kitu.

Wanadini/waumini wahimizwe kuchangia maendeleo yao-sio kujenga mahekalu ya dini ya mamilioni. No, hii haitoishi. Wakiwa katika Ibada-waelimishwe umuhimu wa kuchangia wajenge shule, zahanati, huduma za maji hata kuanzisha Vikoba na bank za kidini kupata mikopo kuepuka bank binafsi zinazotoza riba kubwa; kuwa na vituo vya malezi ya yatima, wazee, wenye ukoma, na walemavu wengine wasiotakiwa majumbani wananyanyaswa.

Kutetea haki za binadamu, vijana, wanawake. Iwe marufuku kikabila, kidini kuzuia wasichana wasisome na kuwaoza ktk umri mdogo. Kupunguza ndioa za wake wengi maana husaidia kuambukiza Ukimwi, virus wanaosababisha cancer za uterus na maradhi mengine kwa wababa, kuwa na familia kubwa masikini yenye watoto wengi.

kila mtu wa dini popote alipo ajue kuwa havitoshuka kama mkate waliopewa waisrael jangwani enzi za Musa, havitoshuka kama mvua bali kwa kutafutwa kwa kazi ngumu kwa kutumia raslimali zilizopo. hata kama utachukua madaraka-fahamu dunia kwa sasa haitoi tena misaada ya bure ili utoe huduma bure kwa wananchi wako, ni kwa kufanyakazi kodi igharimie aidha maendeleo au huduma utakazo kutoa bure. Bure kutoka China, England, Russia, USA imekwisha.

Ukitoa mchango kanisani au msikitini-itumike kuhudumia hekalu na maendeleo ya jamii. Mchango wa 15,000/- kutwa moja kwa hekalu la dini lililojaa waumini ni sawa na kichekesho ambapo waumini hao wana daladala, maduka, mahoteli, migahawa, mikarafuu, korosho, pamna, kahawa, minasi, wauza samaki, madini. Kutoa kwa moyo michango ktk mahekalu kutasaidia kulipia maendeleo ya waumini. Kwa wakristu madhehebu mbali mbali misa moja inafika laki 1 hadi 7. inategemea kanisa ni la mjini, kijijini, City na lina misa ngapi. per day michango ya matoleo kanisa lingine hupata 4-10 million ambazo zinalisha mapadri na masista, huduma za umeme, maji; kugharimia mashule, zahanati, ujenzi mbali mbali nao hupata michango maalum mpaka harambee. Dhehebu kuwa na Colleges, Universities na wasomi wa kuendesha miradi ya dhehebu, kuajiri wataalamu, kuwa na vitega uchumi ili kupunguzia mzigo waumini ndio fashion ya sasa ulimwenguni. Wabongo waangalie haya sio kutegemea vije tu au dhehebu ligharimiwe na GVY kupitia hela za walipa kodi ambao sio waumini wa dhehebu hilo. Ni pale tu dhehebu lina Zahanati, Hospitali kubwa ambayo hutoa huduma ndio inapata madaktari, wauguzi na health kit inayotolewa na wizara ya afya kwa sababu inatoa huduma na kupunguza mzigo kwa GVT kujenga service ya namna hiyo hapo. haina haja ya GVT kujenga another hospital ambapo e.g. Aga Khan, KCMC zipo au zinaongezea huduma zaidi ya Muhimbili au kuipunguzia mzigo. Kama ni mahakama ya kidini-kila dini inao mfumo wake wa mahakama ijigharimie vyote ila mikopo ya Vyuo vikuu-hata wale waendao Universities za Dini wanapatiwa.

Tuungurume tu Kidini, kimadhehebu, kikabila kuonekana tunaonewa na serikali au jamii lakini tunayaharibu wenyewe sehemu kubwa mfano-raslimali zipo ila  tumebweteba wavivu tupo barazani kutwa. Mama akienda shamba asindikizwe na kijana au asiende pekee wakati baba anavua na anaweza kwenda mwenyewe ila haruhusiwi kutoka;  au wasichana hawapewi kipaumbele kusoma na elimu dunia haipewi kipaumbele; mzazi hatumii kuuza mifugo kusomesha au kuchangia ujenzi wa shule kwa kuuza mbuzi mmoja au kutoa 20,000/= kwa mwaka lakini analewa daili au anaoa na kuhonga daily zaidi ya hizo. Hana kipaumbele cha elimu. watoto watasomaje chini ya mti wakati miti mnakata mbao unapeleka nchi jirani, miti mnachoma mkaa. kijijini mnafyatua tofari za kuchoma mnauza na kujengea na kijiji kina mafundi wa kienyeji pia wajengao nyumba za tope au za tofari za aina zote? Kuwaje hakuna harambee ya kufyatua tofari mkajenga darasa moja kila mwaka? Aibu na excuses za kijinga. Eti unakwenda Dar au China unasafirisha mitumba mpaka kijijini mbali porini ukitumia malori ya mizigo au kukodi. Kwa mbinu hiyo-huwezi kusafirisha mchele kutoka huko kuja dar-mchele hauna soko kijijini kwa vile hakuna barabara/miundo mbinu! Mitumba kafa ulaya maroba kibao-imefikaje; madela toka uarabuni na maembe ya kutoka Sudan na S. africa yapo kilombero gulioni, Iringa Mjini au Makete remote area? Kituko bongoland! Kumbe miundombinu si issue hapa!! Shule zipo-haendi shule na akienda hana daftari lakini baba kutwa anavuta sigara pakti na kuja viroba!

Kama ni kikabila tunaoa na kuoza vichanga visisome, au tunaharibu mazingira kwa kulima na kufuga unsustainably. Mengi tunayolaumu yapo chini ya uwezo wetu. Ifike kila dhehebu mwalimu wa dini wa chekechea awe naye na cheti cha form 4 ambayo kwa sasa ukitaka ajira ya kufagia ofisini au kupika chai ni cheti cha form 4. Shekh au Padri awe angalau na degree asiwe na cheti cha dini tu-awe msomi muona mbali aongoze wengine. Kwa wakristu hii sio tatizo. Padri, Sister ni Msomi sio wa dini tu na elimu ya darasani.

DINI ZIWE NA DIRA YA ELIMU DUNIA PIA INAYOTOA AU KUELIMISHA LIFE SKILLS NA KUWAWEZESHA WAUMINI KUWA NA PROFESSIONAL SKILLS ILI KUJIAJIRI AU KUPATA AJIRA. Tukitegemea vizuke kama mvua-tutakaumizana na kuoneana daima, tutapigana na kuuana kwa kushukiana. Mpe mwanao elimu akasome shule yoyote uionayo bora. Una maduka, biashara ushindwe nini kusomesha umuweke auze duka tu; afuge tu, avue samaki tu. Somesha aweze kuuza duka kibiashara, kununua bidhaa bongo asafirishe nchi za nje. Wahindi wameweza kuwa na viduka hadi vikawa viwanda na kuexport na kuwa na miradi Kenya, Canada etc. Waafrika tuige na tuige Wachaga kibiashara ua uwekezaji. Tutapigana na kuwa wakimbizi maporini maana hatuna pa kukimbilia nchi jirani nako kunawaka.

--- On Sun, 2/6/13, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] KONGAMANO LA WAISILAMU JIJINI DAR, Sheikh Ponda aunguruma, Awasihi waisilamu kuwa na umoja, Nuru inakaribia.
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, 2 June, 2013, 18:47

Ukifuatilia typology ya kueneza uislam katika pwani ya Afrika mashariki utagundua kwamba kulikuwa na tatizo lililofanywa na waarabu katika mikakati ya kueneza uislam.  Walipokuja wamissionari wakawa na mikakati iliyoziangalia jamii za kiafrika na kuweza kujipatia wafuasi kiulaini. Kama ni shule waarabu ndo wa kwanza kuzianzisha hapa kwetu lakini zilishindwa kuimarika kama za wenzao ambao waliokuja baadaye.

Wawe waarabu au wazungu hakuna aliyekuja na lengo moja tu la kueneza dini kama dini, walikuja na lengo jingine ambalo ni uchumi. Tatizo watu wengi tunalibeba tatizo hilo la kihistoria na kuliingiza katika jamii ya kizazi kingine kwa namna tunavyotaka liwe badala ya kuangalia ualisia tangu zilipoletwa kwetu. Ni vyema watu wakaisoma historia vizuri tangu mwanzo wa ujio wa dini hizi maana ukianzia mbele lazima kutakuwepo mkanganyiko

On Sun, Jun 2, 2013 at 7:29 PM, richard bahati <ribahati@gmail.com> wrote:
Sheikh Ally Basaleh nae hakusita kuwaambia serikali kuwa kwenye daladala waliopanda watanzania kuna watu wamevaa ndala na kuna wengine wamevaa buti wenye ndala wanakanyagwa ndio maana wanasema! Kwahiyo badala ya kufanya hasira na kuchukua maamuzi ya nguvu bora wawasikilize wanaosema wanakanyagwa.....................

http://goldentz.blogspot.com/2013/06/kongamano-la-waisilamu-jijini-dar.html

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment