Tuesday 18 June 2013

Re: [wanabidii] Katiba Mpya!

Muhingo'
Muundo wa serikali 3 ni mzuri. Hata kama ni gharama kubwa kuendesha serikali 3, ni bora mkafahamu kwamba serikali hizo hazitadumu sana kabla muungano haujafa. Watanganyika wataitaka TANGANYIKA yao iliyozikwa na mafisadi. Wazanzibar wana serikali yao kamili (wana wimbo wa taifa lao, nembo ya taifa lao, bunge lao, nk) wakati serikali ya Tanaganyika mara zote imekuwa ikifichwa ndani ya muungano (ambamo wazanzibar hufaidika pia). Utaona kwamba wakati wazanzibar wakifaidika kupitia serikali yao kwa binafsi yao, lakini pia wanapata manufaa kupitia serikali ya muungano. Ina maana wao wananufaika mara mbili huku watanganyika tukinufaika mara moja tu, tena kiduchu sana.
 
Kwa maoni yangu, muundo wa serikali tatu ni mzuri kwa kuwa hii ndio itakuwa tiketi kuelekea kufa kwa muungano ili kila nchi ikae kama ilivyokuwa kabla ya tarehe 26/04/1964. Kwa nini nasema hivyo? Kimsingi serikali ya Muungano itakuwa kama mapambo tu kwa kuwa haitakuwa na mamlaka ya kuingilia serikali hizi mbili (Tanganyika & Zanzibar). Kulemaa kwa srikali ya muungano kutaifanya ionekane ipo ipo na hatimaye wananchi watataka muungano uvunjike ili kila nchi (Tanganyika & Zanzibar) ikae kivyake. Kwa kufanya hivyo, muungano utakuwa umekufa kifo cha mende.
 
Kuvunjika kwa muungano kutasaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wazanzibar ambao siku zote wamekuwa wakidai kunyonywa, kukandamizwa na kuburuzwa na seriklai ya Tanzania Bara (Tanganyika) katika maswala mbalimbali ya kiuchumi na katika diplomasia ya kimataifa. Kwanza sababu za kuundwa kwa muungano zilishapitwa na wakati na hazina mantiki yoyote mpaka wakati huu. Moja ya sababu ambayo ilipelekea mwalimu Nyerere kuunda muungano, lilikuwa ni swala la usalama, tishio ambalo halipo tena sasa. Manufaa ya kung'ang'ania kuwa na muungano ni kidogo sana ukilinganisha na hasara za kuwang'ang'aniza wazanzibar waendelee kuwa ndani ya muungano kwa shingo upande! Tulitafakari hili suala kwa umakini sana kabla halijaleta mgogoro mkubwa zaidi kama dalili zilivyoanza kujitokeza.






From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, June 12, 2013 1:47 PM
Subject: Re: [wanabidii] Katiba Mpya!

Pole sana Pius.
Watu mkini tunaipenda Tanzania.
Tanganyika ni matokeo ya kazi ya wakoloni.
Tanzania ni matokeo ya kazi yetu sisi. Wanaotukana wanasema ya Nyerere na Karume. Niyo Nyerere na Karume tuliowachagua watuongoze. Tanganyika ni matokeo ya nani na aliwekwa na nani.
 
Naomba nikupe mawazo yangu ndugu Pius na wote watakaosoma maoni yangu:
Ili kuipata Tanzania unayotaka ni lazima muundo wa Jamhuri ya Muungano uongozwe kwa serikali tatu. Serikali mbili zimeuvunja Tayari.
Mfumo wa Serikali mbili naweza kusema aliuweza Nyerere. Ulianza kumong'onyoka wakati wa Rais Mwinyi. Umevunjika kabisa baada ya Katiba mpya ya Zanzibar.
Wasiokubali hili wana matatizo. Kuendelea kuushikilia kwa serikali mbili ni lazima utameguka kabisa bandage iliyoushikilia (CCM) ikichoka au kuondolew madarakani.
Hatari kubwa inayoukabili mfumo huu ikitokea ukavunjika ni kipande cha Tanganyika kuwa na ombwe la uongozi. Kumbuka Rais wa jamhuri ya Muungano si kiongozi wa Tanganyika. Itokee uvunjike ni vurugu tupu. Huo ni uzuri mwingine wa mfumo wa Serikali tatu.
 
Ninachoamini ni hiki
Serikali tatu huenda zikadumu muda mfupi Wazanzibari ambao wametaka kuimarisha madaraka yao watagundua si mbali sana katika mfumo wa Serikali mbili kuwa kumbe walikuwa wanafaidi vitu fulani ambavyo sasa watavikosa kwa kuwepo serikali ya Tanganyika. Watakaporudi kutaka mabadiliko watanganyika watakuwa hawawezi tena kukubali serikali mbili ila Moja. Huo ndio mlango pekee wa kuleta Serikali moja.
lakini isipotokea hivyo Basi tunaweza kuuimarisha muungano wa Serikali tatu kwa kuongeza kidogo kidogo mambo ya muungano na kuyapunguza serikali za washiriki.
Naiomba Tume itupe orrotha ya mambo ishirini na mbili yaliyokuwa kwenye muungano sasa na yale kumi na moja yaliyokuwemo wakati wa kuuasisi.
Kw\ nia hiyo tutauimarisha.
 
Ikitokea ukaparaghanyika basi ni kutafuta ujirani mwema kama Ethiopia na Elitrea au jamhuri za USSR zilizotengana na urusi.
nakupa pole sana lakini kwa matumaini hayo
Elisa

--- On Wed, 6/12/13, Pius Makomelelo <makomelelopius@yahoo.co.uk> wrote:

From: Pius Makomelelo <makomelelopius@yahoo.co.uk>
Subject: [wanabidii] Katiba Mpya!
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, June 12, 2013, 1:02 AM

Naililia nchi yangu Tanzania. Sijaishi upande wa visiwani nikajua fika matatizo waliyonayo wenzetu hawa kuhusiana na mfumo wa utawala tulio nao. Ninachojua Zanzibar siyo koloni la Tanganyika. Natafakari, naona kama kuna kosa vile lilifanyika. Kama Tanganyika ilifutwa kutoa nafasi kwa nchi ya muungano inayoitwa Tanzania, kwanini pia tusifikilie kuondokana kabisa na hizi serikali ndani ya serikali!! Hivi Muungano huu ni wa nani? Kama si wa wachache, kwanini tusitangaze tu uwepo wa serikali moja ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania yenye kuongozwa na serikali moja na si mbili wala tatu!!. Tupeni basi nafasi tupige kura kama kusikilizana kwa kawaida imeshindikana. Hapo tutapata maoni sahihi ya kila upande. Hivi Tume ya Katiba kwanini wanapata kigugumizi kutoa pendekezo hili kama kweli muungano huu tunaupenda sote? SITAKI kufikia mahali kulazimika kuomba uraia wa Tanganyika au Zanzibari kama tokeo la shinikizo la mabadiliko toka kwa watu wachache wenye uchu wa madaraka!! Najaribu kutafakari!!! 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment