Sunday 26 May 2013

[wanabidii] Ya Mtwara, Tafadhali Usininukuu!

Ndugu zangu,

KWETU wanadamu, mengi yanayotufanya tufarakane na hata kugombana yanatokana na sisi wenyewe wanadamu. Na ndivyo ilivyo hata kwa ndege na wanyama.

Ukiwaona ndege wanagombana, ukiwaona kuku wanagombana, na hata ng'ombe, basi, sababu kubwa ni ya viumbe hao wenyewe. Na mara nyingi, kugombana huku hutokana na kugombania kisichotosha.



Hivyo basi, suluhu ya yale tunayogombania kama wanadamu yapaswa itokane na sisi wanadamu wenyewe. Na tangu karne ya 17 kuna wanadamu walioliona hili.



Mwanafalsafa Thomas Hobbes alibainisha, kuwa migogoro mingi miongoni mwetu hutokana na ushindani wa kugombania kisichotosha. Kwa vile sote tuna mahitaji yenye kufanana, basi, Thomas Hobbes anasema, kuwa migogoro hii itaendelea, kugombania kisichotosha.



Na Hobbes huyu anaamini, kutokana na hatari hii, basi, jukumu muhimu na kubwa kwa Serikali yeyote ile iwe ni kulinda amani ya nchi. Kwamba kwa kutofanya hivyo, jamii itarudi katika hali ya kutokuwa na taratibu; vurugu, kuuana, umasikini na kupelekea maisha mafupi.



Hata hivyo, tunaamini pia, kuwa siku zote, pasipo haki na usawa hakuna amani, ingawa, katika jamii yeyote ile, uwepo wa amani na utulivu ni msingi mzuri katika kutafuta haki na usawa, kwa njia ya majadiliano.
( Hii ni sehemu ya makala yangu kwenye Mwananchi, leo Jumapili)

Maggid Mjengwa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment