Tuesday 21 May 2013

[wanabidii] Watu 91 wafa kwa kimbunga usiku wa leo huko Oklahoma Marekani

Watu 91 wanasadikiwa kuwa wamefariki dunia, kati yao 51 wameshathibitishwa kutokana na kimbunga kikali kilichotokea usiku wa kuamkia leo huko Oklahoma Marekani. Plaza Towers ambamo kuna shule ya msingi ni kati ya majengo yaliyoharibiwa vibaya na inasadikiwa watoto zaidi ya 24 wenye umri kati ya miaka 8-9 wamepoteza maisha na wengine zaidi wakiwa hawajulikani waliko.
Majengo mengi ya jiji katika sehemu kilipopita kimbunga hicho chenye upana wa maili mbili. Waokoaji wengi walijikita katika shule ambayo ilikiwa na waalimu na wanafunzi 75 usiku wa kimbunga hicho na watoto wengi wameokolewa kutoka katika matakataka na kuta na kupelekwa katika kituo cha afya kwa matibabu.

 Kimbunga hiki kimekuja wiki moja tu baada ya kimbunga kingine kilichopita maeneo hayo ya Oklahoma na Kansas na kuacha uharibifu mkubwa pamoja na kuuwa wazee wawili na kujeruhi watu 39. Hata hivyo, Jiji la Oklahoma lipo katika mkondo wa vimbunga kwani vimekuwa vikitokea mara kwa mara kwani mwaka 1999  kimbunga kama hiki kiliuwa watu 36
Tazama picha hapa
http://goldentz.blogspot.com/2013/05/watu-91-wafa-kwa-kimbunga-usiku-wa-leo.html

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment