Saturday 11 May 2013

[wanabidii] MAJI YA KUNYWA BADO NI MACHAFU NZEGA.

Hivi karibuni mheshimiwa Rais JK alifanya ziara hapa Nzega na akafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya parking. JK aliongozana na watu wengi katika ziara yake wakiwemo viongozi wa mkoa na  mawaziri kadhaa akiwemo waziri wa maji mheshimiwa Maghembe na mheshimiwa Pombe  Magufuli  ,pamoja  na mbunge wetu wa Nzega mheshimiwa Kigwangala. Kero kubwa kutoka kwa wananchi wa Nzega ilikuwa ni  kukosekana  kwa maji safi. Mheshimiwa mbunge Kigwangala alisimama na kuielezea kero hiyo kwa umahiri mkubwa na kwamba mhandisi wa maji aondoke na JK akimaliza ziara yake maana ameshindwa kazi,huku akishangiliwa na wanachi wa Nzega kwa makofi na vigelegele. Waziri wa maji alisimama na kuahidi kuikomesha kero hiyo mara moja kwani wizara ina uwezo huo. Na aliposimama mwenyewe JK  alihitimisha kwa kusisitiza kuitokomeza kabisa kero hiyo na hapo furaha na shangwe viliongezeka kwa wananchi wa Nzega. Ni kweli baada ya ziara ile wana Nzega tulipata maji kwa wingi tena meupe kama theluji na  barabara zetu zilichongwa na kuwa safi tukashukuru  ujio wa mheshimiwa JK. Cha kushangaza ni muda mfupi umepita na hivi ninavyoongea pamoja na kwamba mvua zilinyesha kwa wingi sana na kujaza mabwawa yetu tunayoyategemea kwa maji  hadi yamefurika lakini maji hayapatikani, na pale yanapotoka ni kidogo na machafu kama hali ile ile ilivyokuwa mwanzoni kabla ya ziara ya JK. Jamani kulikoni huko idara ya maji? kuna matatizo gani? tumedanganywa sisi wananchi au amedanganywa mheshimiwa JK na mawaziri wake?mheshimiwa Kigwangala una habari? Namuomba JK arudi tena Nzega ili tupate maji safi na barabara zetu zichongwe mana zimeharibika kwa mvua sina hakika kama zitarekebishwa bila JK kurudi Nzega.
Suleiman
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment