Friday 10 May 2013

[wanabidii] Hofu Ya Ugaidi (3)

Na Maggid Mjengwa,

LEO tutaliangalia kwa karibu tukio la kigaidi lililoushtua ulimwengu  na hata kuigizwa kama
filamu ya Hollywood.  

Ni tukio  la utekaji wa ndege  ya abiria ya Ufaransa iliyokuwa na abiria wengi wa Kiyahudi.  Na mmoja wa wahusika wakuu katika tukio hili la kigaidi alikuwa Jenerali Idd Amin Dadah wa Uganda.

Ndio, licha ya kuwa Jenerali Idd Amin kuendesha ugaidi wa dola kwa maana ya State Terrorism, kwenye tukio hili, Jenerali Idd Amin alishiriki rasmi kwenye Ugaidi wa Kimataifa. Maana, tukio lile la utekaji ndege lilianzia Ulaya, likaambaa Mashariki ya Kati na kumalizikia kwenye ardhi ya Uganda. Ni kwenye  uwanja wa ndege wa Entebbe huku Idd Amin mwenyewe akishiriki kuratibu harakati za kigaidi.
 
Maelezo marefu juu ya sakata ya Entebbe yanasimuliwa kwa umahiri
mkubwa na mwandishi  William Stevensson katika kitabu chake cha (90 Minutes
At Entebbe), Yaani Dakika 90 katika Entebbe.

Ndege hiyo ilitekwa nyara Juni 27, 1976  mara ilipoanza kuruka
kutoka uwanja wa ndege wa Athens nchini Ugiriki kuelekea Tel Aviv. Miongoni
mwa watekaji nyara,  walikuwemo Wapalestina, lakini raia mmoja wa Ujerumani
naye alishiriki utekaji  huo.  Mjerumani huyo alikuwa ni mfuasi wa kikundi
cha kigaidi cha Ujerumani kulichojulikana kama  "Baader-Meinhof."

Inasadikiwa, kuwa  Dr. Wadi Hadad, mwanaharakati na Kiongozi wa chama
cha ukombozi wa Wapalestina cha PFLP (Popular front For Liberation of
Palestene) alishiriki kwenye kupanga kazi hii ya kigaidi. Bila shaka,
inaaminiwa pia, kuwa  aliyekuwa gaidi nambari moja wakati huo, Ramirez
Carlos, ambaye pia alijulikana kama  "The Jackal", alikuwa na mkono wake
kwenye kazi hiyo.

Baada ya kutua na kujaza mafuta Tripoli , Libya, ndege hiyo.... Soma zaidi...

Baada ya kutua na kujaza mafuta Tripoli , Libya, ndege hiyo...Soma zaidi...http://www.mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/2615-hofu-ya-ugaidi-3.html#.UY3Idcq86Ag

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment