Sunday 19 May 2013

[wanabidii] Hali Ya Utulivu Imerejea Iringa...

Ndugu zangu,

Jioni hii baada ya mazoezi ya mpira wa  watoto  niliongozana na makamanda wangu hadi mitaa ya kati ya Iringa. Nilifika maeneo ya Stendi Kuu, Mashine Tatu na hata Soko Kuu. Hali ya utulivu imerejea. Sikuona hata polisi mmoja barabarani.

Baadhi ya shughuli za biashara zimerejea kama kawaida. Lakini, la msingi, katika miaka yangu kumi ya kuishi hapa Iringa hili ni tukio la kwanza la aina yake.

Bado naamini, kuwa hili la Wamachinga na Manispaa ni jambo dogo ambalo, kama wahusika watatanguliza hekima na busara, linaweza kumalizwa mezani na kunusuru amani na utulivu wa Mji wa Iringa.

Maana, katika nchi za wenzetu kwa yaliyotokea leo wangefanya pia mahesabu ya hasara ya kiuchumi iliyotokana na kusimama kwa shughuli za kiuchumi.

Maana, kama mtu atapiga hesabu za haraka tu kuangalia machache yafuatayo: Gharama za mafuta na posho kwa idadi ya magari ya polisi yaliyotumika,  idadi ya polisi walioshiriki zoezi la leo. Idadi ya mabomu yaliyotumika leo na gharama yake.

Iangaliwepia  hasara ya  kimapato kwa idadi ya maduka yaliyofungwa kwa siku ya leo. Daladala zilizoshindwa kufanya kazi. Achilia mbali mali zilizoharibiwa.

Maana, kadhia kama hii ya leo imepelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha mzunguko wa fedha na hivyo kuwaathiri wengi kiuchumi.

Ni dhahiri, kuwa ni muhimu kwa Wamachinga wakatafutiwa namna ya kufanya kazi yao ya kujipatia riziki, lakini, itangulizwe pia hekima na busara katika kulitafuta jawabu ili kuepusha madhara ya kiuchumi na kijamii.

Ni matumaini yetu, kwa mji wetu wa Iringa na Mkoa wetu kwa ujumla, tukio la leo liwe pia fundisho la kubaini njia bora za kutatua migogoro yetu , ya kisiasa na kijamii.  Na hakuna njia iliyo bora kabisa, kama njia ya mazungumzo.

Na kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine ya kutufikisha hapa, basi, watafakari kwa makini, ili kilichotokea leo kisitokee tena, kama inawezekana.

Maggid,
Iringa.
0754 678 252

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment