Sunday 19 May 2013

[wanabidii] Kumbe udini una mkono wa nje!

Rais Kikwete: Udini unaoibuka una mkono wa nje
 
Dodoma. Rais Jakaya Kikwete amebainisha kuwa vurugu za kidini na kisiasa zinazotokea nchini, zina uhusiano na watu wa nchi za nje.

Alitoa kauli hiyo jana kwenye ibada maalumu ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mkuu wa Sitta wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya.

Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.

"Wanaohamasisha vurugu hizo ni watu wenye uhusiano ya karibu na watu wa nje ambao mambo yakiharibika nchini watakuwa wa kwanza kupanda ndege, ilhali wakiendelea kutoa matamko ya uchochezi wakiwa nje ya nchi wakati wengine wakiendelea kuumia," alisema Kikwete.
 
Endelea: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Udini-unaoibuka-una-mkono-wa-nje/-/1597296/1856798/-/10s0m89/-/index.html

0 comments:

Post a Comment