Tuesday 28 May 2013

[wanabidii] ELIMU YA JUU KUANZIA WALE WALIOISHIA DRS LA 7

Hatimaye Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (Tanzania Commission for Universities) imetangaza utaratibu na sifa kwa watu wanaotaka kusoma masomo ya shahada (degree) ya kwanza katika vyuo vikuu nchini; kuanzia wale walioishia darasa la saba. 

Waombaji hawa wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
1) Wawe na umri kuanzia miaka 25
2) Wawe angalau wamemaliza darasa la saba
3) Wawe na uzoefu katika nyanja fulani
4) Wawe na nia ya kujieleza kwa kusoma masomo ya shahada ya kwanza
5) Wawe wanamudu kutumia lugha ya Kiingereza kwa ufasaha kwa kuandika na kuzungumza pia 

Kuna vigezo vingine ambavyo wanatakiwa kutimiza. Hivi ni pamoja na kuambatanisha vyeti za kuzaliwa, picha, CV, vyeti vya kitaaluma kwa mambo mbalimbali waliowahi kujiunza, na ripoti za aina mbalimbali kutoka kwa waajiri au wasimamizi wao wa kazi-huko walikokuwa wanafanya kazi.

Utaratibu unaeleza kwamba kwa wale watakaofikia vigezo; watalazimika kufanya mtihani wa kupimwa uwezo wao. 

Maeneo ambayo wanaweza kujiendeleza ni: Elimu, Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Kilimo na Elimu ya Wanyamapori, Utawala, Uhasibu, Sheria na masomo yanayoendana na teknolojia. Kwa maelezo zaidi soma hapa:http://bit.ly/12uSxqU

Una maoni gani kuhusu fursa hii ya kujiendeleza?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment