Tuesday 28 May 2013

[wanabidii] ELIMU-MSINGI KWA MIAKA 10

Rasimu ya sera mpya ya elimu na mafunzo inayojadiliwa sasa na wadau inapendekeza kuunganishwa kwa elimu ya msingi na sekondari ya kawaida ya sasa ili kuunda elimu msingi itakayotolewa kwa miaka 10; kuanzia mwaka 2018. Hebu soma hapa kwa maelezo zaidi: http://bit.ly/17JzRLa

Rasimu hiyo ya sera inapendekeza kwamba wanafunzi watakaofaulu elimu-msingi, ndio watapata fursa kusoma elimu ya sekondari; ambayo ni sawa na kidato cha tano na sita; au ufundi stadi. 

Miaka 5 kuanzia sasa ni muda unaotosha kufanya maandalizi sahihi. Kwa bahati mbaya-uzoefu unaonesha kuwa nchi yetu huwa inaleta mabadiliko katika mfumo wa elimu bila maandalizi ya kutosha. Kwa mfano, mipango kama MMEM na MMES-na shule za sekondari za kata zilianzishwa bila maandalizi ya kutosha kwa upande wa walimu, vitabu, mfumo, nk. Matokeo yake-hali ya elimu nchini inazidi kuyumba japo shule zipo nyingi na watoto wengi zaidi wako shule. 

Hili la kuleta elimu-msingi ni jambo kubwa sana. Lina mabadiliko mengi ya kimfumo, kimuundo, mitaala na ujengaji uwezo kwa walimu. Lisipotazamwa kwa makini linaweza kuyumbisha zaidi elimu yetu. Kwa kuwa wabunge wanatakiwa kujadili suala hili hivi karibuni; ni muhimu kwanza waulize na kujiridhisha maandalizi ambayo serikali inafikiria kuyafanya na kwa wakati gani yatakayoweza kubeba mabadiliko haya makubwa. 

Mjadala usiende kwa haraka kuangalia kwamba miaka 10 hiyo ni sahihi-au hapana. Tukienda huko tutajikita kwenye maudhui ya mfumo huo. Kumbe mjadala unatakiwa kwanza kuangalia uwezo wa nchi kutekeleza mfumo huo mpya. Yaani mpangilio wa kitaasisi, ukaguzi, uandaaji wa walimu, uwezeshaji wa walimu, bajeti ya elimu, nk. Hili la bajeti ni muhimu sana kwa kuwa watoto wote wanaoanza shule za msingi wataenda mpaka sekondari. Ni nini kinachoifanya serikali iamini kuwa hili linawezekana-hasa ukiangalia mazingira ya sasa kwamba shule zinakosa mahitaji muhimu? Kwa nini serikali isipimwe kwa kuonesha uwezo kwanza wa kusimamia na kugharamia elimu vizuri kwa utaratibu uliopo (ambapo matumaini yanazidi kufifia); angalau kwa miaka 3 ijayo; kabla ya kuleta kitu kipya? Katika kipindi hiki kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo-tunataka kuona dalili zipi zitakazotuaminisha kwa tutafanikiwa? 

Haya ni baadhi ya maswali tu. Bila shaka wadau wa elimu mtakuwa na maoni na maswali kadhaa kuhusu suala hili. Tafadhali mjulishe mbunge wako kama utakuwa na maoni kuhusu suala hili. Hivi karibuni tutawawekea hapa nakala ya rasimu hiyo ili muweze kutoa maoni kwenye maeneo mengine pia. Sote tuna nia njema ya kuona elimu yetu inaleta mafanikio kijamii, kiuchumi na mambo mengine bora.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment