Sunday 5 May 2013

[wanabidii] BREAKING NEWS - MLIPUKO MKUBWA UNAOSADIKIWA KUWA NI BOMU UMELIPUKA KANISA KATOLIKI ARUSHA

Redio Maria ipo hewani ikitangaza juu ya tukio la mlipuko mkubwa unaosadikiwa kuwa kusababishwa na bomu la kurushwa wakati ibada ilipokuwa ikiendelea.

Leo kulikuwa na uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasit mjini Arusha. Mgeni rasmi alikuwa Mwakilishi wa Papa toka Vatican. Kulikuwa na wageni wengi waliambatana na mwakilishi wa papa, wakiwemo maaskofu, mapadre na watawa kutoka mataifa mbalimbali.

Mtoto mmoja ameeleza kuwa aliona watu waliokuwa kwenye mini bus wakirusha kitu kuelekea kwenye mkusanyiko wa wakristo waliokuwepo kwenye ibada.

Taarifa zinaeleza kuwa eneo kubwa limetapakaa damu, watu wengi wamejeruhiwa. Inasadikiwa kuwa wapo waliokufa lakini haijathibitika. Muda huu vyombo vyote vya usalama vipo eneo la tukio.

Kwa update zaidi sikiliza Radio Maria http://streema.com/radios/play/6848.

Hivi sasa kuna taharuki kubwa, na kuna taarifa ya milipuko mingine, haijulikani kama ni ya washambuliaji au ya polisi, mbali na eneo la ibada.

Nawapeni pole nyingi waliokumbwa na mkasa huu, wakatoliki, wakristo wote na wanaolitakia amani Taifa letu.

Bart

0 comments:

Post a Comment