Hata kule wanakochimba wenyewe dhahabu, Tanzanite na vito vingine artisanal miners utakuta eneo hilo ni vurugu tupu, mabanda ya beer, video chafu, mabanda ya shutashuta (Geita-maanake kujamiiana kwa chapu chapu), kuoana bila ya kupia HIV; uharibifu wa mto wa maji na misitu maji, kuchezea mercury bila kuzingatia elimu wapewayo; kutumia hela katika anasa (hata Joti aliigiza ktk michezo ya TV jinsi maisha yalivyo) ni matatizo tupu. Niliwahi kuweka attachment humu kuhusu hali halisi ilivyo mfano Mugusu Geita Gold mining site. Licha ya kuwa hawana maendeleo lakini wananchi baadhi wamejenga lodges, maduka ambayo ndio biashara zetu. Sio zile za economic productive za mashamba, viwanda vidogo vidogo kwa kujiunga kuunda kampuni. Serikali itawajengea labda barabara, shule, zahanati, mengine matajiri wetu waunde kampuni wawekeze.Sio kulimbikiza mifugo na kuoa wake wengi na kuranda mnada hadi mnada kuongeza mifugo. Tunayo safari ndefu. Makala ya Patrice Tsakhara inaelimisha sana na hivi ndivyo ilivyo duniani. Ila sisi wabongo ni wepesi wa kushabikia kitu hata kama si chakweli tunapenda kukikuza na kukwepa ukweli. Huu uswahili wa ushabiki, majungu na utaranta wa lugha mineno mingi ndio unaoturudisha sana nyuma hata katika familia. Hakupangwi kukapangika kikafanyika labda iwe ni arusi tu. hapo tutachanga na kujimaliza. Lakini kupanga vya ushirikiano kufanya pamoja cha kuendelea-makabila machache labda Mchanga, Mkinga, Mpemba na siku hizi Mha anakuja juu sana. Coastal zone-sleeping giant-ni uswahili, mitazamo finyu, sifa mtu anapoeleza hata visivyo vya kweli. Mungu atusaidie na anisamehe. --- On Fri, 24/5/13, paul lawala <pasamila292000@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment