Sunday 26 May 2013

Re: Re: [wanabidii] TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUHUSU MTWARA

Ukipangilia hivyo unapata jibu unalotaka ambalo si jibu sahihi la tatizo. Hivyo hufai kumaliza tatizo lakini unafaa kuliendeleza. Tunataka liishe.

----------
Sent from my Nokia Phone

------Original message------
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, May 26, 2013 2:59:07 PM GMT+0100
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUHUSU MTWARA


Mimi sielewi; Mwananchi anapokula njama na kutumia suala la Gas kama kitu cha kumfanya aanze kuchoma nyumba, kuharibu mali za wasio na hatia, kuvunja madaraja kwa  baruti, kukata miti ya umeme kwa vile wa upande mwingine wamegoma kuandamana kuwakomoa wasipate umeme.  Kisha baadhi wa wanakijiji wenzake wakaungua na kufa kwa moto achomao; wakampiga mtumishi wa serikali au muandishio; akina mama na wagonjwa wakakosa huduma hospitali kwa vile usafiri wa aina yoyote utachomwa moto ukionekana barabarani na daraja limebomolewa.
Baada ya uharibifu wote huu wa mali nyingi, kinaingia kikosi cha jeshi. wananchi wana silaha za jadi za mishale ya sumu, mikuki, mawe na matairi na petroli ya kuwasha moto tairi na magogo njiani. Wanajeshi wa Serikali inabidi watumie silaha kali ambazo zinaua-wakapigwa wachache wakafa au mmoja akafa Hili linakuwa ni kosa kubwa ilioje kuliko makosa yote waliyofanya wananchi!

Fikiria kati ya aliyeuawa ni baba au ndugu yako aliyegoma kuandamana au akienda shamba kwa gari lake hajui kinachoendelea. Na aliyepigwa risasi ni yule akiwalenga mshale wanajeshi au akitumia silaha aliyokuwa nayo ya bunduki au aliyekuwa akikatiza ikampata kwa bahati mbaya. Yaani daima ni askari tu wakosa waannchi ni clean?

Je, ikiwa daima twaona upande mmoja tu wa GVT tukiambiwa tunajitafutia umaarufu wa NGO zetu au mashirika yetu kuonekana ili yapate misaada daima kwa kutumia suala la gas kama issue itakuwa kosa? Mimi ninaona, shirika ambalo linapenda kusaidia kukomesha vurugu hizi, lijipange, au litafute hela na kupanga mpango mkakati, au lijitolee kufanyakazi na GVT ya kujua ni kitu gani cha kuwaelimisha wananchi waelewe kuhusu mafao yao katika gas hii ili kuelimisha wananchi kieleweke.

Ikiwezekana, serikali, izidi kutoa kimaandishi magazetini  kwa mwaka, itoe tarehe na majina, mafao yote ambayo yamekwisha kupatikana na kutolewa maeneo ya mali asili-gas_Mtwara, Songosongo etc; Umeme (Pangani, Kidatu, Kihansi, Mtera), uwekezaji mfano ktk machimbo ya almasi, dhahabu, makaa ya mawe etc, Mbuga za Hifadhi- Mikumi, Udzungwa, Loliondo, Ruaha, Seleous,  NCAA, Mkomazi, Kigoma Malagarasi etc.

Kuwe na gazeti moja la serikali liandikwe kiingereza na Kiswahili kila baada ya miezi 6 litoe taarifa na takwimu nchi nzima. Wasiogope kuorodhesha hata majina ya waliosomeshwa hata wakiwa ni watoto wa madiwani na wabunge list ndefu maana wengine wakiambiwa kuchagua wafaidika wanachagua jamaa zao huku wao ni viongozi au wachaguliwa wawakilishi wa wananchi ila wanajipa wenyewe kipaumbele, kisha wanasaidia kuwatia wananchi hamasa za vurugu kuficha maovu yao. Nani kaenda ziara-aandikwe; kapata scholarship, mikopo, mafunzo ya ujasiriamali etc.

Baada ya wananchi kufanya vurugu kuua wafanyakazi au kuharibu mali zao, kisha watataka kusaidiwa na hao hao wafanyakazi mfano wa zahanati, hospitali, polisi na mahakamani-jee wanaelewa matokeo ya kuchomea watumishi wa GVT au mashirika binafsi mali zao na kisha kuhitaji msaada toka kwao wakiwaendea kazini au shuleni?

Vurugu hizi, zitawapa mwanya wahamiaji haramu kupita, askari toka congo walioadhimia kuja kutukomoa kuja kutujua kutuwekea mbinu za kutuua; majambazi kuingia maeneo kuua na kufanya vurugu maana wanajua chuki iliyojengwa kwa police, FFU, JWTZ hawatofika mapema wakiitwa vijijini kusaidia- hawatokwenda Tunajichimbia kaburi.
Jinsi magari binafsi na nyumba zilivyochomwa ni si jambo la kufurahia kwamba GVt imekomoka, ni la kusikitisha.

Mbona tunachomeana nyumba kila siku na kuuliana familia, kuibiana mifugo kila mwezi na kuuana, kuvamia magulio na kupigana risasi, kuwaficha wakimbizi na kuwapitisha wahamiaji haramu, kupanda na kuuza bangi na kusumbua askari kuzing'oa; kukata viungo albino, kuoza wasichana wadogo kisha tunatoa taarifa amefariki au amehama shule kumbe kapelekwa kwa mume; kumbaka msichana au ma nakisha kumkata viungo na serikali inateseka kutuelimisha na hatuelimishiki. Na NGO zinashindwa kuelimisha wananchi haya yanakotokea ndani ya koo na vijiji ili yaishe. Leo haki hii ipo tu pale GVT inapopambana na wananchi? Sio pale wananchi wanapouana wenyewe kwa wenyewe daily-NO, zinakaa kando? hatuoni kuwachachamalia hao wananchi na kuwazingira kudai haki muuaji na mchomaji nyumba kwa Imani za kishirikina akamatwe na yale magomvi ya Batemi na Loita na kunyonga vitoto vifugaji masuala ya karne before and after independence yaishe maana na huko nako NGO za haki na maendeleo ni kila
kijiji. Excuse me! Ninauliza maana ninaona kama issue hizi za haki na usalama wa raia zinanichanganya.
matumizi ya nguvu nikiangalia TV nchi nyingine wanavyopambana na wananchi na askali kufatua risasi wakaua na kuuana askari na wananchi-ninaona hapa Tanzania nguvu bado kidogo. kama ile ya S.Afrika. walipofyatua risasi chache wananchi-askari wakajibu kwa kuzimimina. Ni hivyo India, Pakistan na wanavyobondana Uk na USA.


Ni tatizo la sisi waafrika kytaka kusifiwa. kama mtu akikupinga maoni na tabia zao-unamfanya adui. Hivyo hata ukiwa unafanya vurugu mwandishi anaona si vizuri asiseme aseme ni vizuri ili usimpige? huu utakuwa utoto yaani daima mwandishi au mtu wa radio akusifie tu ili asije akapigwa? ujinga. kusema mbaya wakati si nzuri ni bora kuliko kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Viwanda Dar vipo vingi Mtwara ndio vitaanza, gas lazima ije Dar, Morogoro, Tanga na Mbeya kuvifufua na kuvipunguzia gharama ya umeme.



--- On Sun, 26/5/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUHUSU MTWARA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 26 May, 2013, 12:34

TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI
WA HAKI ZA BINADAMU KUFUATIA HELE TETE YA USALAMA MJINI MTWARA

 

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
(THRD-Coalition), mtandao pekee unaoshughulikia usalama wa watetezi wakiwamo
wanaharakati wa haki za biandamu na waandishi wa habari, umepokea kwa
masikitiko makubwa vurugu kubwa zilizotokea mjini Mtwara na kusababisha vifo
viwili  hadi sasa kulingana na taarifa zilizotufikia
mpaka sasa. Tunaungana na familia za wafiwa na watu wote waliopata adha
kufuatia vurugu hizo.

 

Baada ya kupata taarifa za vurugu hizo tulimtuma
mwakilishi watu katika Kanda ya Kusini, mkurugenzi wa asasi mwanachama wa
Mtandao, ambaye ametuletea taarifa kwamba miongoni mwa watu walioathirika na
vurugu hizo  ni watetezi wenzetu hususani
waandishi wa habari na wengine ambao japo hawakudhurika lakini wanaendelea
kuitwa kwamba ni wachochezi kwa upande wa serikali na wasaliti kwa upande wa
wananchi.

 

 Miongoni mwa
walioathirika na kadhia hiyo ni Bw. Kassim Mikongolo mwandishi   wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), ambaye amechomewa nyumba yake.

Wengine ni Bw Hassan Simba, mwandishi wa
Habari Leo ambaye pia ni mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mtwara na
vile vile ambaye aliokolewa na Jeshi la Polisi baada ya kupata misuko suko. Na
vivyo hivyo kwa mwandishi wa Uhuru Rashidi Mussa ambaye maisha yake yamo
hatarini.

 

Waandishi waliotajwa wamechukuliwa tofauti
na wananchi na mwishowe kuamua kuwaadhibu kwa kudhani kuwa wanapotosha ukweli
wa madai yao. Hata hivyo mtandao kushirikiana na wanachama wake wanaendelea
kulifuatilia suala hili kwa undani na kujua hali ya sasa kwa waandishi na
watetezi wa haki za binadamu Mkoani Mtwara.

 

Mtandao wetu unaomba wakazi wa Mtwara na
Watanzania wote kwa ujumla wawe watulivu katika kipindi hiki ambapo bado hali
haijaonyesha kumalizika kwa mgogoro huo ambao umechukua miezi kadhaa sasa. Hata
hivyo tunaomba mambo yafuatayo ili kulinda amani na kuwalinda watetezi wa haki
za binadamu waliopo katika eneo hilo.

 

1.      Jeshi la Polisi
na Serikali kwa Ujumla

Mtandao
wa Watetezi wa Haki za Binadamu unapinga vikali matumizi ya nguvu hususani
Jeshi la Polisi katika kutatua migogoro mbali mbali. Tabia hii imeongezeka na
kusababisha madhara makubwa ikiwamo vifo kama ilivyokwisharipotiwa mara kadhaa.
Tunaamini njia muafaka ni ya kutumia ushirikishaji na uwazi katika kufikia
muafaka wa mikataba mbali mbali.

 

2.      Vyombo vya Habari


Vyombo
vya habari vya umma vijue jukumu lao kwamba vinatakiwa kuwatumikia Watanzania
wote bila kujali itikadi zao. Tunaamini kwamba kushambuliwa kwa waandishi hao
kumetokana na kukosa imani kwa wale walioamua kujichukulia sheria mkononi na
kuwashambulia waandishi ambao wao wanaamini wameegemea katika upande fulani.
Tunawasihi waandishi wa habari wa vyombo vya umma siku zote wabakie katikati
hasa inapotokea mgogoro katika ya wananchi na serikali.

 

3.      Asasi za Kiraia


Aidha
tunatumia nafasi hii kuwasihi watetezi, wanaharakati na watendaji wa asasi za
kiraia kuendelea kutimiza majukumu yao bila woga lakini pia kwa kuzingatia
sheria, kanuni na maadili ya kazi zao. Tunaamini wapo wenye lengo la kutumia
matatizo yaliyojitokeza Mtwara ili kuzifanya asasi za kiraia zionekana kwamba
ni za kichonganishi jambo ambalo ni uzushi mtupu.

4.      Wananchi wa
Mtwara

Pamoja
na kwamba madai yenu ni halali, tunawasihi siku zote mjaribu kuwavumilia
watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari mnaowadhania wanapotosha
ukweli wa madai yenu badala ya kuwachomea nyumba na kuwatishia.

 

Kwa zaidi ya siku tatu sasa waandishi wa
habari, watetezi wengine na wanachi kwa ujumla wanaishi katika mazingira ya
hofu kwa kushindwa kujua hatima ya maisha yo iwapo wataendelea kuwa mitaani
kama ilivyozoelweka.

 

Ahadi Yetu

Mtandao unaahidi kutoa msaada kwa waandishi wote
watakaokwamisha katika jitihada zao za kutaoa taarifa juu ya mgogoro huo na mingine
kadhaa. Mtandao kwa kushirikiana na wanachama wake utatoa taarifa kamili baada
ya siku chache zijazo.

 

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa uelewa wenu.

 




 

ONESMO OLENGURUMWA

MRATIBU MTANDAO WA

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU
TANZANIA



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

 

 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment