Thursday 23 May 2013

Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI

MWAKYEMBE,

  hivi ni kwa nini mtu akisimama kudai haki anayoona haipati anaonekana katumwa? kama mikoa mingine haiwezi kusimama na kudai hali nzuri ya uchumi unategemea Mtwara wawasemee? na kama unadai Tanzania tuna tatizo la kiungozi unategemea nani aseme? Mtwara wao wameliona hilo, yale ya Liwale hata kwenye ushahidi wa wazi wa dhuruma walisema wametumwa ina maana wao hawaoni? au ni kwa vile mmewaona watanzania ni mazezeta hawajui kitu? acheni mtwara wadai kile wanachodai kama wao wanaoni ni haki yao wadai

   kule usukumani dhahabu inachimbwa, matani yanapelekwa ulaya wao wanabaki na umasikini hata watoto wao hawana madarasa ya kusomea, hali kadhalika kule nyamongo, hata kule mfindi ambako mbao zinavunwa kwa wingi nako shule hazina madawati kwa nini? hamjiulizi hilo kw nini? watu wa mtwara wanasitahili kunufaika na gesi kwanza ndo na wengine tufuatae hakuna mzazi aliyetoa chakula kwa watoto wa jirani ilihali wakwake walale njaa!!!

2013/5/23 Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
Ezekiel,

Hatuwezi kuhalalisha yanayotekea Mtwara kwa sababu ya kusahauliwa. Ni Watanganyika wangapi waliokumbukwa na hiyo serikali, vipi kuhusu Rukwa ambao pamoja na kutekezwa lakini ndio wenye kuwalisha hata hao wa Mtwara, vipi kuhusu Tabora, Kigoma, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Katavi, Kagera, nk.

Tatizo la umasikini linawakaba Watanzania wote, watu wameingia Mtwara wakatumia udhaufu wa umasikini wetu na kuchochea vurugu, hapana lazima tukatae vurugu.

Tukumbuke hizi vurugu zimeanza baada ya taarifa za kuwepo kwa hizo rasilimali, ni mazingira hayo hayo yanayozifanya nchi kama DRC, Somalia, Sudan, na nyinginezo kuwa katika machafuko miaka yote.

Tanzania tuna matatizo  ya kiuogozi kama taifa, lakini pia tuelewe kuna nguvu kutoka nje zenye lengo la kutugonganisha ili wajichotee rasilimali hizo bila bughudha wakati sisi akili iko kwenye kupigana wenyewe kwa wenyewe.

Felix

2013/5/23 Ezekiel Massanja <ezekielmassanja@gmail.com>
Maelezo yako dada Hilda mazuri sana lakini yana kasoro za msingi. Baadhi ya sababu ulizozitoa unaweza kuzitafiti tena kuona ukweli wake. Watu wa Mtwara wanalilia maendeleo Yao baada ya kusahauliwa kwa MUDA mrefu. Kwa MUDA mrefu pato la taifa halikugawiwa kwa Haki. Naweza kukupa mifano michache tu: Angelia barabara zinazoenda kusini na zile zinazoenda kaskazini, kwa nini miundombinu  Hii muhimu itofautiane kiasi hicho wakati nchi ni moja hii hii. Ni kweli Kwamba hata watu wa Maganzo kwenye almasi maendeleo Yao hayalingani na utajiri ulio jirani hapo. Ni kweli Kwamba tujikita kwenye majimbo wengine ambao hawana HAYO madini na gesi watafanyaje? Basi kile kinachopatikana kigawiwe kwa haki, wote wapate, ndipo hiyo amani iwe ya kudumu.

wasalaam

On Wednesday, May 22, 2013, Hildegarda Kiwasila wrote:

Radio zimeongea vizuri zaidi zimetoa maelezo makini ya kinachoendelea na uharibifu unaofanyika na waandishi wa habari kuwindwa eti wakiongea wanaipendelea serikali. Kwa hali ilivyo Mtwara sasa, wageni ni wengi sana wanaohusika na utafiti na shughuli za miradi ya maendeleo funded by international devemopment organizations. Ni hatari sana kama watawavamia hawa na kuwadhuru.

Ikiwa suala ni Gas ibaki kwao, basi watu wa Kihansi na huko Ruaha-Mikumi Kilombero, Pangani 1 and 2 Tanga; Mtera, Nyumba ya Mungu dam ambao hata kuvua huzuiwa nao waanzae kukata milingoti ya Miti kuzuia umeme Usije Dar na Maeneo mengine? Mungu atusaidie. Mbona mafao ya National park, Madini tunatumia nchi nzima kama sources za hela za nchi ambapo hata wafugaji na wakulima kando ya mbuga hizo kuingia protected areas wanaadhibiwa?

Kwao hao vijiji vingine vyenye vyanzo vya umeme umeme unapita juu angani ya waya za umeme wao wanamulikia mienge ya moto. Hawana benefits na benefit sharing ni mkakati mpya wa sasa kimataifa kuanzia RIO Summit 1992.

Maji yanatoka Ruvu, wami yananywewa mijini kuko vijijini misitu ni protected wasitumie ili maji ya mto yapatikane kwenye intakes yafike e.g. DSM. Tukifanya hivi kwamba kila mwenye ambako resource ipo azuie hatutofika mbali. Issue ni planning for benefit sharing. Wao watafaidikaje? Kuwe na mpango katika aina zote za resources ambazo zinatambulika kama mali ya umma sio binafsi. Hatutatatua matatizo kwa kuharibu miundo mbinu. Kubomoa daraja na mwenye mimba sasa na hofu ya mapambano uchungu utakuja haraka. Jee, utamsafirishaje unapokataza wasitoke nje na kuharibu miundo mbinu? Kweli tunafurahia haya na wengine kuona kuwa ndio faida ya utawala ni wa kifisadi ambapo mafisadi ni waume na ndugu zetu. Wakishitakiwa-tunaweka mawakili wazito. Na wakirudi home hao mafisadi tunawapigia KURA sisi wenyewe wanashinda tena. Jamani tumrudie Mungu.

--- On Wed, 22/5/13, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 22 May, 2013, 12:25

Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA 

Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa) 

Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela

Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake

Ni mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi wala mabomu . 

Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.

 Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.

Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.

Matairi  kila  kona  ya mji  yamechomwa  barabarani  polisi  na  zimamoto   wanafanya kazi ya kuzima na kufukuza wananchi. Kauli mbiu "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"

Kambi ya Upinzani yaukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi

Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani.(habari haijathibitishwa rasmi)

Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari yao,askari wengi waliokuja si wa hapa Mtwara wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora vinalia ovyo ovyo.

watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia

Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari. Vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya. Ili Wananchi wayapate .

 Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu.

Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo.

Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo.

Kituo  kimoja  cha habari  kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)

Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar.

Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika

Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.

Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali.

2013/5/22 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Askari mmoja na raia mmoja amefariki na ofisi ya ccm na kituo cha mafuta vimechomwa moto

2013/5/22 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Nasikia hata Guest Houses walizowahi kufikia askari wakati wa vurugu za mwanzo zinachomwa moto (Not sure).
 
Hali kama hii haifai kabisa kwa Taifa huru kama hili. Wahalifu lazima wasakwe na wakamatwe na wafikishwe mbele ya mkono wa sheria.
 
Naona hii sio gesi tu kuna kitu cha ziada hapa.
 
Tutajua tu.
 
K.E.M.S.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment