Usemalo sawa but it is too long inapoteza meaning yake jaribu kusamarizi mada zako.
Date: Mon, 13 May 2013 05:09:27 +0100
From: khildegarda@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] MLIPUKO ARUSHA TUNAPAPASA TU BADO HATUJASEMA TATIZO HASA NI LIPI
To: wanabidii@googlegroups.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Date: Mon, 13 May 2013 05:09:27 +0100
From: khildegarda@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] MLIPUKO ARUSHA TUNAPAPASA TU BADO HATUJASEMA TATIZO HASA NI LIPI
To: wanabidii@googlegroups.com
Hata kama hakuna kiwanda cha mabomu TZ mabomu yapo Nd shirima. Kumbuka kuna biashara ya chuma chakavu. Ilitokea milipuko ya hand grenades kiwanda kimohawapo mwenge akafa mmoja au kuumia makuli waliokuwa wakipakua mzigo nikiweka kumbukumbu yangu. Hawa walipakia vyuma chakavu vilivyotoka vijijini ambako wananchi waliokota mabomu hayo maeneo ya mazoezi ya majeshi ambayo hukatazwa wananchi kuingia. Maeneo hayo huingiwa na wananchi kuokota kuni, kuchunga mifugo lakini hukatazwa hata mabango huwekwa ila huingia na kuokota vyuma hivyo. hata ukielekea monduli Mjini kuna chuo cha kijeshi utaona wafugaji ndani ya maeneo ya jeshi yasiyoruhusiwa. Ni hivyo maeneo ya Mikumi kuelekea Kilosa-Ruaha. Usiingie, wanaingia na uchao miguu inabaraswa. Iliandika magazetini huko nyuma mzee aliokota bomu la vita kuu za dunia. Jinsi ilivyokaa alidhania ameokota 'tunguri' ya mganga labda aliipoteza huko porini. Akawa anatafuta mteja, akaiweka uvunguni nyumbani kwake. Wakati akiota moto chumbani akaamua aichukue aiangalie vizuri-Likaripuka na moto/joto lile ikampata kisawasawa na kuumiza wajukuu. hii ikala kwake. Yapo mabomu ya mkoloni yanakata watu miguu na kuua. Zipo barudi na hutumika kuripua wakati wa ujambazi-wanapiga kutishia watu pia kubomoa milango. Kimara Baruti ni jina la eneo ambako serikali/jeshi wakiwa na vibanda vya kuhifadhi baruti ambazo hutumika katika upasuaji mawe ya kutengeneza kokoto au mawe ya ujenzi. Hii huenda ilianza ukoloni maana majengo ya Mwarabu, Mjerumani na Mwingereza mijini na miji ya kale (Bagamoyo, ZNZ, Tanga) na maeneo mengi hata DSM posta yalikuwa yamejenga kwa mawe mpaka ghorofa zake na kwa miti migumu dari zake. Majambazi wanatengeneza viripuko kwa kubomoa majuja, safe za hela na kuiba-utaalamu huu wameupata wapi si Uarabuni wala ughaibuni kokote ni humu bongoland. Nchi imeitwa 'Bongoland kutokana na kuta na utaalamu na mbinu za kila aina hasa za ubunifu mwema na wa uovu na uchakachuaji kwa kutumia utaalamu asilia. Gari unaiona nje Ford ya 1962 inatembea ndani engine ya Toyota 1990. Hakusoma shule lakini fundi mjenzi mzuri, fundi magari kutokana na kujifunza kwa vitendo lakini amesoma ana madigrii-Fisadi anaangamiza uchumi wa nchi. anahamasisha uovu lakini familia yake anahamishia ulaya inasoma na kukaa huko. Mengine ni ya Ujinga/Upumbavu bila ya kujali madhara yake. Kwani wachimbaji wadogo wadogo wanaripua mawe kuchimba madini wanapata wapi viripuzi kiasi kwamba ishindikane kutengeneza bomu la misumari au la waya nchini na baruti zipo? Hawa wanaripua miamba mpaka wanajizika wenyewe huko chini wanaporomokewa na udongo. Yaani unachimba chini kwa chini futi mia plus na huna vifaa vya usalama na ukiipata hela hiyo kwa tabu unaishiwa kulewa na ngono si salama!! Ni vibanda vya pombe, video chafu, ngono! Mkorogo wa waya na misumari unaweza kutengeneza bomu unaweza kutengenezwa Mererani, au Nyarugusu, Nyangarata au Kisumu ukaingia Arusha. Bomu linaweza likanununliwa kutoka wahamiaji maharamia kutoka nchi zinazopigana vita-Burundi, Congo. si huuza bunduki na wanaweza kuuza mabomu? Mbona ujambazi nchini umetumia kuripua hand grenades? Majambazi wanavamia nyumba kadhaa vijijini, wanavamia gulio au soko na silaha na vibomu? Wanaona tulivyo wajinga na tamaa, twawakaribisha na silaha, mabomu, wanatuuzia na huwasaidia kuvamia vijiji, mabasi ya abiria, bank, wafanya biashara. Twanakuja mwanya kukata miti, kuchunga mifugo na wana silaha. Tunawalaza lodging zetu. Tulifanya hivyo kwa wasomali Loliondo na hivyo kwa hao toka Burundi na tunawabeba wahamiaji ndani ya magari, pikipiki, container na kufunga silaha kama maiti ndani ya jeneza. Twasafirisha bangi na unga kama mzigo tunafisha ndani ya viroba vya unga, pamba etc na tuna bandari bubu kuanzia Tanga hadi Bagamoyo, DSM, Kisiju, Rufiji, Mtwara kupitia Indian Ocean. Bado Misitu ya kuwapitisha-Rombo, Loliondo, Tarime, Kigoma etc-tatizo gani bomu la aina yoyote lisiingie? Itashindikana vipi mabomu yasiingie? Tuweke kambi za JWTZ, JKT, Prisons mipaka ambayo ni nyeti. Wanaweza hao waovu wa Arusha kutoka mfano nchi jirani kusema 'Tuwaone hao na Arusha yao na Tourism na sasa inazidi kukua na makao makuu ya kila aina na mlima wao na kila kitu chao sasa wanauwezo wa kutangaza kuwa kipo kwao. Vijana wao ktk Tourism sasa wamejifunza sio kiingereza tu bali hata lugha nyingine sasa utalii unahama kwetu upo kwao. Ngoja tuichafue Arusha utalii uhame. Si kuna kiongozi mwakilishi wa Papa? Wacha tukaripue itaonekana ni UDINI kumbe ni kiuchumi au kisiasa kutaka kuichafua CCM na serikali yake kuwa-haiwezi. Yote yawezekana bila ya kujali unaumiza wasiohusika. Kuna wasioogopa kufa kwani-utaona gari/lori la mafuta linatembea (Ubungo-Buguruni Road) na vijana wanafungua tankers kutoa petroli. wanafanya hivyo wakitumia mifuko ya rambo na maguduria. Moto ukiwaka hapo ni DSM yote ukizingatia vifaa vya zima moto duni na mbanano wa nyumba-twapita njiani sote tunawaangalia wakitutengenezea kifo. Twaogopa kuwasema au kuwazuia watoto wetu wenyewe kwa kuogopa kupigwa nondo au kisu. Ila, polisi akikwapuliwa bunduki na majambazi ikafyatuka risasi na kuua mtu-tunaandamana vikali. Hawa-tunawatazama. Ukiwaka moto-serikali haijali usalama wa raia ambao hucheza na petroli na kuiweka majumbani mitaani-kuganga njaa. na huyo wa bomu akiganga njaa pia. Mbongo/Mswahili tabia yake ni maneno mengi, visingiszio vingi, upeo mfupi kutokana na mbinu zake za ubinafsi na kupenda lawama. kujituma ni hadimu hata kama ni kwa maendeleo yake mwenyewe. Kupenda rahisi rahisi cha haraka au chapuchapu bila kujali sustainability-kula leo na kesho na vizazi vijavyo. Desturi na tabia ya uvivu, muono mfupi nakupenda misifa/Sifa inatuumiza na ndio tupo ktk baraza za malumbano badala ya vitendo. Maendeleo hayashuki kama mvua-ni kwa kazi. hakuna GVT itakayotuletea maendeleo bure. Wakati wa bure umekwisha-ule wa kuletewa Uhisani ambapo hela zake zikitoka walipakodi nchi hizo za kutuma uhisani. Bila ya kuzalisha mali kwa faida ili kugharimia maendeleo yetu-tutakuwa watumwa wa kujiripua daima. Bila ya kuwa na utaifa moyoni ukajiona u mzungu ndani ya moyo au mwarabu-tutajimaliza. Adui wako si dini nyingine au rangi ingine, adui wako ni uvivu wako mwenyewe, kutokupenda shule na kujituma kimasomo na kuchangia elimu (kunywa bombe, ugoro, kuoa wake wengi, nyumba ndogo poa!!) ndio tatizo. Hupati ajira na kuweza ujasiriamali uwe na skills kama hutojifunza ukawa na elimu au skills. Elimu ya dini pekee haikupi ujasiriamali na ajira au kujiajiri. Kuna ubaya gani kuwa na Sheikh au Padri ambaye ni fundi makanika? Mwalimu wa sekondari au chuo kikuu cha taaluma? Tatizo nini kuwa na mwalimu wa madrasa ambaye ana cheti cha ualimu wa vidudu ambapo atafundisha dini pia taaluma ya mtaala wa vidudu? Bila kubadili mifumo ya dini third world countries ikawa na taaluma-adui daima atakuwa UDINI. Tutatupiana mabomu, kuuana kama inavyoendelea Somalia, Nigeria, afghanistan. Ifike iwe kama Misri, IRAN-unaongea kiarabu, unasali sala 5 lakini ni daktari unatibu hospitali, unafanya upasuaji na matibabu. Kiarabu ni lugha tu na quran inaijua. Na hivyo ndivyo tanzania inavyokwenda sasa na vyuo vya kidini iwe St augustino, Islamic secondary school or University. Sasa tusirudi nyuma kwenye kupambana KIDINI tena academics na uzalishaji mali. Makanisa yalianza zamani toka yaje. kanisa ina shule na karakana za magari vijana wanajifunza car mechanics, useremala, ufugaji, elimu dunia, kushona, mapishi, kufuma. Padri, Sister ana degree, professor, medical doctor ila padri. Josho la kanisa la RC la 1868 huko Bagamoyo lipo na watumwa waliokombolewa wakristu na waliobaki kuwa waislamu hawakubatizwa wakijifunza skills nyingi na ufugaji. Josho lipo hadi leo na karakana za enzi hizo za 1868. Lakini eneo lililotolewa mahali paitwapo Nchi Pana karibu na Msikiti wa Ijumaa kujengwe chuo cha Kiislamu-kumejengwa jumba la fahari la mtu. Alichokifanya ni kuipa ofisi ya Kata ya chama chenye bendela hapo. Mchawi hapa nani na chuo tegemewa kiliwekwa jiwe la msingi na Mkuu mmojawapo wa dini hiyo? Angalieni haya. Tunajichakachua wenyewe. Watendaji katika NGO-wawe na shughuli za uzalishaji mali sio kutegemea Grants tu toka nje-ndio inabidi uhamasishe visivyo ili uendelee kupata grants. Wana siasa-aonyeshe kafanya nini kwake kijijini na jimboni kwa kutumia raslimali watu na natural resources sio kelele tu? Kuna mito 50 inaingia baharini-jee, umehamasisha traditional irrigation farming? umeshirikiana vipi na distric agricultural officer, chuo cha kilimo kilichopo wilayani/mkoani (Naliendele, Ilonga, Sokoine) na Funding NGO-Aga Khan Foundation, Jane Goodal, CONCERN, SNV waliopo wilayani.Mkoani na ktk vijiji jimboni kwao au jimbo jirani wanafanikisha na kusaidia kilimo? unapiga kelele tu Bungeni hata chuo cha Kilimo jirani yako hujafika???? Mbona halmashauri ina miradi ya kilimo na wahisani wanazalisha value added cassava, dwarf eleucine, millet, sorghum na mbegu za maharage, soya beans etc. wana kituo cha mifugo ya kisasa mbuzi anatoa lita 3 kwa siku ng'ombe 6 kwa siku? umefika? pamoja na hayo kuna chuo cha Afya na hospitali kuu jimbo lako na chuo cha maendeleo-umewatumia wakaweka pilot villages ktk vijiji vyako kufanikisha Kilimo na Ufugaji kwanza? Tutalaumu na kutumia UDINI lakini kitovu vya umasikini kinachohamasisha UDINI na chuki kisiana tunacho wenyewe. Bomu linaweza kununuliwa au kutengenezwa nyumbani utaalamu upo na linaweza likaingizwa nchini mbona yapo na yanatumika ktk ujambazi na tunaona yakionyeshwa ktk TV? Kikulacho kikiwa nguoni mwako Si rahisi kukigundua. na bado makubwa yanakuja-wanyanga'nyeni waliojilimbilizia ardhi za serikali wakajipa hati miliki na kuzungushia kuta; boboeni maghorofa beach maeneo ndani ya uwio wa bahari usio ruhusiwa; bomoeni majumba yaliyojengwa ktk open space na hao wenye hela ambao baadhi yao hudiriki hata kubomoa nyumba ya mtu hata kama kesi ameshinda-ubavu mkubwa huo. Bomoeni mali za hao itupate ya kutupata, yataripuka kote na hapo ndipo tutakapoamini kuwa ndani ya UDINI kuna UGAIDI Kiuchumi na ulafi wa Vyeo Kisiasa kwa visingizio vya UDINI. --- On Sun, 12/5/13, Fratern Shirima <shirima.fratern@yahoo.com> wrote:
|
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment