Saturday 11 May 2013

Re: [wanabidii] MAJI YA KUNYWA BADO NI MACHAFU NZEGA.


Kwa kuchangia,
Maji yanaweza yakawa meupe lakini SIO SALAMA. weupe ni rangi tu ila cha kujiuliza-hayana bacteria au minyoo na wadudu wa aina nyingine yoyote ambao wanaweza kuambukiza maradhi kama kuhara na kutapika, kipindupindu etc? Hayana sumu za aina yoyote?

Maji kuya ya rangi ya udongo haimaaninshi SIO SALAMA. Yanaweza yasiwe wa wadudu wa aina yoyote ni udongo tu usio na madini mabaya wala bacteria na vidudu vingine. Yakitulia, ukachuja ukanywa au ukachemsha ukanywa. Lakini kwa usalama wa maji -chemsha hata kama ni meupe. Unaweka ukajitengenezea mitungi kokoto ya kuchuja maji au ukachuja kwa kitambaa kutoa udongo, majani etc yakatulia ukachemsha.

Hata kama mradi umekamilika-uendelevu wake (sustainability) unategemea sio serikali tu-inategemea umetekelezwa vipi-je, kwa kuhusisha wananchi kwa kuzingatia Sera na Mkakati wa maji vijijini wa kushirikisha wananchi na viongozi wao (community-participation/Stakeholder participation)?, wamechangia na kufungua account ya maji kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo (operation and maintenance or O&M)? Wana kamati za maji na kama ni shared scheme-Water User Association (WUA)? Zinakutana kila mara inavyotakiwa na kama kuna matengenezo viongozi wanamweleza Bwana maji au water technician wa eneo (Kata/Tarafa) na kugharimia matengenezo ya mradi wao eneo lao (inategemea scheme imeharibika level gani) na source ya maji ni nini (Bwana kutememea mvua; msitu maji, mto, ziwa)? Kama ni Bwana, au Msitu, Mto etc wanalindaje mazingira na source ya maji? Wanalima kando ya bwawa, kunywesha na mifugo bwawani sio kwenye cattle trough. hii husababisha michanga kujaa (siltation of water source) ambapo maji hukauka na hayaingii ktk main water pipe from intake na distribution pipes zinakuwa hazina maji. Pump engine ikiwashwa ipandishe maji kwenye tank-inavutatope hivyo bomba zinazima, mashine nayo inayopeleka maji katika sump itaishia. Mategenezo yatakuwa makubwa na matokeo ya kukosa maji ni watu kwenda kunyweshea bwawani kufua na kukoga kugawa na kuambukiza maradhi.

Kupitisha mifugo mazito barabara za kukoto, udongo hurahisisha mmomonyoko wa barabara. Watanzania tuna desturi ya kuchukua kokoto kutoka barabarani inapojengwa, wengine huchokonoa hata zile za lami kuchukua kokoto kujengea au kuuza. Ulinzi shirikishi unahitajika kuwashughulikia wanavijiji kama hao. lakini kutokana na tabia za kulipiziana kisasi, kushambuliana na kutishiana uchawi-hii huachwa ikaendelea hata vijijini. Kwa DSM ukienda kunduchi ambako machimbo na uchimbaji umekatazwa muda mrefu utaona wachimba kokoto wamechimba mpaka kwenye miti ya umeme za simu zile za milingoti (TTCL), wamechimba chini kwa chini ktk barabara ya lami ambapo ni hatari ni kama wale wanaoonekana wakigombea mafuta ya petroli ambapo yanaweza kulipuka yakawaua wakati wowote na yakawasha nyumba zao huko wanakoyaweka. Wakiyauza-kilabuni kuganga njaa ya pombe sio kuanzisha kabiashara. Wanapoharibu mazingira ya Bwawa, watatembea mwenzo mrefu kutafuta maji, inaathiri masomo. Budi wapande miti Maji kuzunguka bwawa, kuweka uzio kuzuia mifugo yao na ya wahamiaji, kuweka ulinzi wa bwawa na mabomba toka bwawa na vijijini na mlinzi ktk pump house wamlipe kwa hela yao ya maji ambayo bei ya ndoo ya maji watapanga wao ili kupata hela ya mlinzi na ya O&M. Sera ya Maji Bure haipo tena ambapo zamani maji Bure yalikuwa funded na donor money hela toka kodi za wananchi wao toka nchi zao. WUA itaangalia mauzo ya maji na makusanyo, O&M issues. Jinsi ya WUA kufanya kazi yake na usimamizi wa miradi ya maji vijijini Sera na mkakati upo wazi na vitini vya mafunzo vya kiswahili vipo. watu wa Tabora wanaweza wakatembelea miradi ya wengine wakaona WUA zinafanyaje kazi wakaiga. Maji yanaweza kuwa yamejaa bwawani yasitoke kutokana na soil erosion na silt iliyojaa ndani ya mabomba makubwa na madogo. Mabomba yanaweza kuwa yameziba na kuzibua kila bomba si mchezo. Inatakiwa wawe wameweka chujio maji yanapoingia bwawani, ktk mabomba makuu ya kupeleka tangini na bomba la kugawa etc na uondoaji udongo (O&M ya bwawa) kufanyika inavyotakiwa na kukarabati machekeshe ya kuchuja maji. water Technicians wa wilaya wanafanyakazi yao? Wananchi wanawajibika na maeneo yao? Sheria ndogondogo (bylaws) zao za maji zinafanyakazi? Sio Serikali pekee mfumo wa Maji unaweka majukumu wazi-ni wote kwa pamoja. Diwani anahusikanaje na kuhakikisha kuwa watu wake Katani wanazingatia, bwana maendeleo na Afya wanatimiza wajibu wao wa community education and organization? Tupeni hiyo kazi tufanye Evaluation tuwape majibu wapi pabovu na nini cha kufanya. Mshiko upo?

Ndio maana mabwawa ya maji kwa mfano Nyumba ya Mungu Dam, Mtera, Pangani hydropower dam na mengineyo shughuli za uchakachuaji mazingira na ndani ya mabwawa zinakatazwa. Kalemawe dam,na mengineyo yanayotegemewa kwa kilimo, uvuvi na unyweshaji mifugo, kunywa;  Mugumu Dam maji ya kunywa etc yote yanatakiwa  kulindwa.

Usishangae kuja kuona kuwa wananchi wanapata matatizo ya matumbo, Kansa ya utumbo, koo hata kama maji hayo meupe kwa sababu yanakuwa na kemikali za kilimo aupesticides ambazo wananchi hutumia bila ya kuzingatia matumizi salama; mifugo hukoga dawa za josho na kuingizwa bwawani ambapo maji hutegemewa na binadamu pia; kuvua kwa baruti na kutumia dawa ya sumu ya panya ya kiasi ili samaki na dagaa wafe wawapate kiurahisi. Kisha kunywa hayo maji, kunywesha mifugo hata kama haifi madhara yake twala ktk samaki, maziwa na nyama. bado wale wanaokoshea madini maji hayo au machimboni na kutiririkia bwawani kutokana na mafuriko au ndio bwawa linategemea maji toka surface ili yajae sio toka mto salama. Ndio maana Weupe wa maji si tija tija yasiwe na kemikali na wadudu maradhi. HK-Mheshimiwa Kingwallah anaijua hii. Ndio maana elimu ya uendeshaji miradi ya maji kuuwianishwa na Elimu ya Afya na Usafi wa mazingira.



--- On Sat, 11/5/13, Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com> wrote:

From: Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
Subject: [wanabidii] MAJI YA KUNYWA BADO NI MACHAFU NZEGA.
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 11 May, 2013, 11:23

Hivi karibuni mheshimiwa Rais JK alifanya ziara hapa Nzega na akafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya parking. JK aliongozana na watu wengi katika ziara yake wakiwemo viongozi wa mkoa na  mawaziri kadhaa akiwemo waziri wa maji mheshimiwa Maghembe na mheshimiwa Pombe  Magufuli  ,pamoja  na mbunge wetu wa Nzega mheshimiwa Kigwangala. Kero kubwa kutoka kwa wananchi wa Nzega ilikuwa ni  kukosekana  kwa maji safi. Mheshimiwa mbunge Kigwangala alisimama na kuielezea kero hiyo kwa umahiri mkubwa na kwamba mhandisi wa maji aondoke na JK akimaliza ziara yake maana ameshindwa kazi,huku akishangiliwa na wanachi wa Nzega kwa makofi na vigelegele. Waziri wa maji alisimama na kuahidi kuikomesha kero hiyo mara moja kwani wizara ina uwezo huo. Na aliposimama mwenyewe JK  alihitimisha kwa kusisitiza kuitokomeza kabisa kero hiyo na hapo furaha na shangwe viliongezeka kwa wananchi wa Nzega. Ni kweli baada ya ziara ile wana Nzega tulipata maji kwa wingi tena meupe kama theluji na  barabara zetu zilichongwa na kuwa safi tukashukuru  ujio wa mheshimiwa JK. Cha kushangaza ni muda mfupi umepita na hivi ninavyoongea pamoja na kwamba mvua zilinyesha kwa wingi sana na kujaza mabwawa yetu tunayoyategemea kwa maji  hadi yamefurika lakini maji hayapatikani, na pale yanapotoka ni kidogo na machafu kama hali ile ile ilivyokuwa mwanzoni kabla ya ziara ya JK. Jamani kulikoni huko idara ya maji? kuna matatizo gani? tumedanganywa sisi wananchi au amedanganywa mheshimiwa JK na mawaziri wake?mheshimiwa Kigwangala una habari? Namuomba JK arudi tena Nzega ili tupate maji safi na barabara zetu zichongwe mana zimeharibika kwa mvua sina hakika kama zitarekebishwa bila JK kurudi Nzega.
Suleiman
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment