Tuesday 9 April 2013

Re: [wanabidii] URAIS 2015 - ZITTO KABWE NDIO CHAGUO SAHIHI KWA CHADEMA

Sina tatizo na jina lolote litakalopendekezwa na kamati kuu ya CHADEMA, nikiamini kwamba watakuwa wamefanya hivyo kwa nia njema na bila ya upendeleo wa aina yoyote, au uzembe wa kufuata umaarufu wa jina la mtu n.k.
Nimesoma mapendekezo ya ndugu aliyeleta mada hii hapa jamvini, ninashindwa pakuanzia kuchangia hasa nikihisisha kipengere ambacho mlela mada amekipa namba "1" na "2", Inakuwaje mtu uje na wazo la udini au ukanda wakati maswala haya yanapigiwa kelele yasistawi? Eti mtu apewe nafasi ya kugombea kwa ajili ya dini au kwa vile hana harufu ya ukanda.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuemisha watu wasihadaliwe na maswala ya ukabila, ukanda wala dini, hawa siyo adui wa maendeleo yao, adui wakubwa ni pamoja na huo udini (adui mpya hasa ukizingatia viongozi waliopo swala hilo wanalipapasa papasa utadhani ni kama kaa la moto), ubadirifu wa mali ya umma, undhaifu wa viongozi, hata uongo wa kuhadaa wananchi ili wawachague, na wakishakalia viti hutasikia wakigusia baadhi ya vitu walivyovipigia kampaini.
Nakumbuka kulikuwa na kauli hii kwenye uchaguzi uliopita, ili kuwatoa wazee majimbani mwao waende kwenye vituo vya kupoigia kura kwamba "Tuanaangalia uwezekano wa kuanza kulipa wazee pesa za kijikimu bili kujali walishawahi kufanya kazi au laa".
Sisemi waliahidi wataanza kulipa, lakini kauli ya namna hiyo inawapa moyo wazee, hasa ukizingatia wengi wao hawana uhakika wa mlo wa siku.
Zitto au mtu mwingine yeyote yule anaweza kupewa hiyo nafasi, lakini swala la udini lisije kikawa kigezo hata siku moja, kwa kusema hivyo kunakumpa mtu dhamana kubwa ya Taifa kwa sabau zisizo za kimsingi, narudia tena, jama tujitahidi kuotokomeza huo ugonjwa wa udini, au chama kimoja kisije kikawa kinapika kampaini kikishiriki kusitawisha chuki kwa wananchi kwa kuzungumzia mambo ya ujimbo au ukabila, sisi sote ni Watanzania.




From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, 9 April 2013, 14:59
Subject: [wanabidii] URAIS 2015 - ZITTO KABWE NDIO CHAGUO SAHIHI KWA CHADEMA

Kwanza poleni na kazi za hapa na pale katika pilikapilika za kutafuta na kuendesha maisha.

Mimi ni mwanachama halali wa CHADEMA mwenye kadi namba 0333673 ya uana chama. Ningependa kuwashirikisha jambo lifuatalo.

ZITTO Z KABWE NDIO CHAGUO SAHIHI KUWA MGOMBEA URAISI KWA CHAMA NA WATANZANIA MWAKA 2015.

Ndugu zangu, viongozi wa chama na wanachama! Kama kweli tuna taka kuchukua nchi hii basi Zitto Z Kabwe ndio chaguo sahihi kwa nafasi ya uraisi kwa chama chetu. Nina sababu chache zifuatazo.

1. Tukubali au tukatae CHADEMA hatukubaliki maeneo yenye waislamu wengi kama mikoa ya Pwani naTabora kwa sababu ya dhana hii ya udini. Iwapo Zitto Z Kabwe atasimama basi lazima hata wale waliokuwa hawataki kutuchagua kwa sababu ya udini basi kura zao tutakua nazo.

2. CCM wanatumia dhana ya ukanda. Iwapo Zitto atasimama basi hawatakua na ajenda yoyote katika kampeni zao dhidi ya hoja hiyo. Hakika huo ndo utakua mwisho wao.

3. Zitto ni kielelezo cha democrasia bungeni na mtaani. Ni Kijana aliye ibuo hoja nyingi sana nzito na ni kijana aliyeamsha vijana wengi sana usingizini. Zitto hajachoka kuwatetea vijana pamoja na kejeli zote anazozipata.

4. Zitto ni kijana na anamvuto kwa vijana wengi sana . Vijana sasa wamechoka sana na wangependa kupata mkombozi wa kweli. Zitto is a right guy in this. Zitto atavuta hata vijana wasio penda kupiga kura na wao washiriki kuongeza ushindi.

5. Zitto hana kashfa yoyote ile ndani ya chama na nje ya chama. Zitto amejiweka safi katika kashfa hizi ukiondoa propaganda chache zisizo na macho. 

6. Zitto ameishi umaskini. Anajua nini adha ya kuwa na shida na anajua uchungu wa kuwa maskini. kwani ametoka katika familia maskini sana na mkoa maskini sana. Kwa ufupi ana uchu wa maendeleo.

7.Zitto sio mdini kama viongozi wengine wa kiislamu walivyo. Zitto hajawahi kujiingiza katika mgogoro wowote wa udini na hana mpango huo kwani kwa mtazamo wangu yeye ni public figure.

Mwisho, najua wengi tungependa Dr Slaa agombee tena urais. Lakini amini nawambieni kama kweli nchi hii tunaitaka basi Dr. Slaa sio chaguo la ushindi. Kwani hana vigezo vingi ambavyo zitto anavyo.

Pia najua Zitto kasema hataongelea tena urais lakini hakusema sisi wanachama tusiongele huo urais. Ningependa sana Dr. agombee lakini mwisho wa siku hatuta shinda kwa mgawanyo wa kura.

Mimi sio mfuasi wa Zitto. Mimi ni mfuasi wa CHADEMA na mpenda mabadiliko. Naongea kitu halisi, kama mtaona nimeandika vyema asante lakini kama mtaona nimeandika vibaya, subilini mwaka mmoja na nusu uliosalia halafu muone yatakayotokea.

JJB,UDSM

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment