Tuesday 9 April 2013

Re: [wanabidii] Uchambuzi Wa Habari: Viboko Shuleni Au La, Ni Mjadala Wa Aibu!

Mimi naunga mkono matumizi ya viboko kwa kuwa nidhamu kwa wanafunzi imeshuka sana, ilimradi tu walimu wasitumie hii fursa kwa lengo la kuwakomoa wanafunzi kwa kuwapiga bakora hata kwa makosa ya kipuuzi.. Ni dhahiri kwamba mwanafunzi asiyekuwa na nidhamu hawezi kujali masomo wala hana morali na utayari wa kujifunza. Nidhamu kwa mwanafunzi imepungua sana kwa sababu serikali imefuta adhabu ya viboko kwa wanafunzi. Kwa upande mwingine utovu wa nidhamu umechangiwa na wazazi ambao huwa wakali sana pindi watoto wao waadhibiwapo kwa kuchapwa bakora na walimu.
 
Hili ni kosa kubwa sana. Uliona wapi wanafunzi wanafundishwa nidhamu kwa maneno matupu bila kutumia viboko? Viboko kwa wanafunzi ni kama askari na bunduki au kuku na yai. Mimi nawashangaa sana hawa waliopendekeza kufutwa kwa viboko mashuleni bila kujali umuhimu wake kwa wanafunzi na ufaulu wao katika masomo!
 
Utovu wa nidhamu, unaotokana na kutochapwa bakora, sio tu kwamba unachangia matokeo mabaya tu lakini pia unawafanya wanafunzi wajisikie huru zaidi na kuiona shule kama mahali pa kwenda kustarehe na kupoteza muda! Matokeo yake wanafunzi hujiingiza katika matendo ya ajabu kama ngono na uvutaji bangi, hivyo kujikuta wakipotea zaidi kimaadili pamoja na kupata mimba za utotoni (teenage pregnancies) ambazo huwafanya wafukuzwe shule.



From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, April 9, 2013 10:59 PM
Subject: [wanabidii] Uchambuzi Wa Habari: Viboko Shuleni Au La, Ni Mjadala Wa Aibu!



Ndugu zangu ,

Moja ya habari kubwa leo ni hii;

"Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ilisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji.

"Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi..." alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa." ( Mwananchi, Aprili 9, 2013)

Nionavyo;

Tunarudi nyuma miaka 50 badala ya kwenda mbele. Kuna wengi kama mimi tusioamini, kuwa, kumchapa mwanafunzi bakora ni kumsaidia kujenga nidhamu na kujituma.

Kinyume chake, kama ni nidhamu, utamjengea nidhamu ya woga na kufanya yale ambayo anadhani unataka ayafanye na si kuwa ayafanye kwa faida yake na jamii hapo baadae.

Viboko vinamfanya mwanafunzi asijiamini na hata akose uwezo wa kudadisi. Bado nakumbuka, kuwa nikiwa Darasa la Tano ilinitokea nikachapwa bakora darasani kwa kosa la ' kumdadisi sana mwalimu'. Mimi nilitaka kupata ufahamu zaidi lakini mwalimu aliniona nimekosa nidhamu.

Habari hiyo ya kwenye Mwananchi inazungumzia mpango wa kurudisha sheria ya adhabu ya viboko wakati kimsingi watoto wetu wanachapwa viboko mashuleni kila kukicha.

Wanafunzi kukosa nidhamu na kutokufanya vizuri kwenye masomo inachangiwa na mambo mengi. Tuanze kuyaangalia hayo kwanza kabla hatujawahamasisha walimu wakate bakora za miti ya mipera kuwachapa watoto wetu.

Na kwa Waziri mwenye dhamana kuonyesha kushabikia watoto kuchapwa bakora si kitu kingine bali ni jambo la kusikitisha sana. Na mjadala wa kama watoto tuwachape bakora au la, katika wakati tulio nao, ni mjadala wa aibu- A shameful debate!

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0788 111 765
http://www.facebook.com/l.php?u=http%3A%2F%2Fmjengwablog.co.tz%2F&h=YAQH9aSj_&s=1
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment