Ahsante kijana, kweli kabisa usemayo. Sheria msumeno. Hata hakimu aliacha simu yake wazi ikalia akiwa katika kusoma hukumu, akajisomea hukumu mwenyewe akajikabidhi polisi alipomaliza kikao, akatoa faini na kuingia ndani kwa masaa yaliyohitajika. Wachawi wa maendeleo yetu ni sisi wenyewe. Unasoma gazeti la Kulikoni unaambiwa kampuni ya Grumeti Reserve Company imeloa 4 million 1 au TAS 1.6 bilion kwa mwaka kwa Ikona Wildlife Management Area asilimia 10 (10%) ya mafao yao kwa mwaka lakini hazijulikani zimefanya nini. wakili alihusika kusaini mkataba hela na kuna NGO inahusika kuona kuwa inasaidia maendeleo ya vijiji 5 hivyo husika lakini hakieleweki. sasa NGO ipo, wakili yupo, District Council ipo kinachoshindikana kunyoosha kisichoeleweka ni nini? matokeo wananchi wanaweza wakaacha ulizi wakavamia watalii na kampuni husika kumbe alae ni mtanzania msomi kabisa. Kwa nini wasifanye auditing na performance evaluation wa WMA hiyo kuleta ufanisi katika utendaji? Bado ile ambapo nyumba imejenga kuta mpaka barabarani, kuta imewekwa X lakini anaendelea kujenga halibomolewi. Bado unakuta gari trela limesimama barabarani limeharibika na pilice anapita hapo anaiona hiyo hatari hachukui sheria. Mwananchi Boston kaona damu kuelekea boat yake akapiga simu police wakaja kumshughulikia. Sisi hapa tungeandamana kuangalia chama na udini hata kama walivamia na kumomoa mali za mtu-tunatetea na kuweka mawakili ghali kuangalia udini. Wenzetu sheria msumeno na mzazi akasema hapa wasisingizie dini au uislamu wala nini ajitokeze mwenyewe. Ukiangalia yale magari ya police katika mtandao (mfano daily mail uk) utashangaa kuwa police wa kule wana magari ya namna hiyo kama vile ya Jeshi lao kuu mfano kama JWTZ yetu. Huyo police alivyovaa na vifaa vyake tofauti na hawa wa kwetu. Wananchi wanawashangilia na kuwasaidia sio kuwarudhia mawe wanapoingia nyumba hadi nyumba. Camera kila mahala na zimetumika kiinteligensia. Sisi kwetu hadi leo hatujawapata waliomuua padri ZNZ na hata kama yupo nyumbani tunamficha na akienda mahakamani tunajaa dunia nzima kutaka kuleta vurugu na hata kupiga sala hapo nje na kunyoosha vidole vya ushindi ndani ya mahakama kudharau mahakama. Tu punda milia -wenye rangi mchanganyiko tunataka haki na huku tunavunja sheria. Fikiria hata kutaka kumpiga speaker-sijui kwa vile ni mwanamke? Mbona speaker wengine hawakuvamiwa kutaka kupigwa. hii ni gender humiliation. Kweli tuna haja ya kujifunza kutekeleza wajibu na sheria. Kuwapa vifaa vya kisasa askari wetu. Kujitahidi tuweze kujituma kujiletea maendeleo yetu wenyewe. Ajabu-Afrika ni vita daily na kubaka awtoto, wamana na hata wanaume kwa sasa, kuwatia vilema watu mbio daima halafu unataka uchaguliwe uwe kiongozi wa nchi. Nchi nzima 90% HIV positive kutokana na vita na ubakaji-wazungu wanatucheka vita daily vikaragozi tunakubali kutumika. Nina kijana nyumbani kwangu ninamsaidia age 23. mama yake kafariki ameacha nyumba ina vyumba 8 na mabanda huko Tanga. mjomba wake anamdhulumu. hana pa kula wala kulala. Ana shangazi masikini. Kesi mahakamani tanga inachukua muda. Mjomba anadai nyumba ni yake, wosia umeandikwa unamtaja yeye mrithi. Kesi mahakama ya Ardhi Wilaya Handeni anasema ya Mjomba-tayari amekula fedha. Hivyo inakwenda Mkoani. Ni usumbufu. Kisha wakamfanyia njamna yeye mjomba na watoto wake wakiume walamfanyia uchafu kumkomoa-sodomy. Mjomba yupo nje hajakamatwa-si ana hela ila watoto wake wapo ndani. Sasa huyu mtoto atapata wapi hela ya kuhonga-rushwa. Mimi ninamsaidia kutokana na kukutana naye kwenye study ya mashoga ambapo sana ninapata tabu kuwajua wenye shida wapo mgongoni daima kuomba msaada. Mwafrika mtanzania-mwanasheria anadiriki kumtesa mtoto kama huyu kutokana na hela za rushwa. jee hao wengine? Tunarudisha nyuma jamii yetu wenyewe na maendeleo yetu-wachawi sisi wenyewe pamoja na external factors zipo ila tunazibeba. Mungu atusaidie. --- On Sat, 20/4/13, salum mkango <salumkango@yahoo.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment