Friday 19 April 2013

Re: [wanabidii] BUSARA ZA MZEE RUKHSA NA UPUMBAVU WA “WAFIA DINI”

Binafsi nimemuelewa vizuri Fakhi, anachojaribu kusema hapa ndo kitu ambacho wengi tumekwisha kisema mara nyingi potelea mbali udhaifu wa mifano aliyotumia. Amemnukuu Mzee mwinyi kama ifuatavyo " kila mtu ana haki ya kuchinja au kunyonga kitoweo chake iwe paka,nyoka, panya, kuku, mbuzi, ng'ombe n.k "  Sina uhakika kama ni kweli mzee mwinyi alitaja vitu kama paka na nyoka. Maana hawa wanyama kama ukiamua kuwachinja au kuwanyonga na kuwala sidhani kama utakutana na upinzani wowote hapa Tanzania sana sana watu watakukimbia. Mifano kama hiyo ni dhihaka kwa umma.

Si jambo la busara kuanza kutengana kwa sababu ya imani zetu ila nijuavyo mimi hizi harufu za ubaguzi wa kidini tunazoziona ni kwa sababu ya umaskini na ni tatizo kwa nchi maskini ambapo mtu anashindwa kutambua vizuri chanzo cha matatizo yake na badala yake anategemea miujiza ili kuishi. Tunachanganya mambo yote kwenye imani zetu tulizorithi toka kwa wazungu na waarabu. Unakuta mtu huyo huyo anayejitia ni msimamo mkali wa imani fulani ya kidini (dini za kigeni) ni huyo huyo anayeshinda kwa waganga wa kienyeji kutafuta utajiri na mambo mengine nisiyoweza kuyaandika hapa.

Tunachotakiwa kujali ni afya zetu kwanza kwamba huyo mnyama kachinjiwa na kuuziwa kwenye mazingira yaliyo safi na salama kwa afya zetu kama sheria ya uchinjaji wa nyama unavyosema habari ya imani ndo ifuate. Sitegemei kama tutaacha kuumwa na pengine kufa kama mnyama mwenye magonjwa atachinjwa na mtu wa imani yoyote bila kukaguliwa vizuri na wataalamu. Tunagombania kuchinja je mazingira na wanyama wanaochinjwa tunayajua? Nafikiri tuanze na hilo hili la imani lifuate.

Technolojia hapa duniani inakwenda kwa kasi kubwa na dunia imekuwa kama kijiji inawezekana baada ya miaka michache ijayo tukaanza kuagiza nyama toka Botswana au kwingineko maana kama tunaagiza hata sindano tutashindwa vipi kuagiza nyama kama hapa kwetu haipo? Sina uhakika kama tutakuwa tunajua nani amechinja nyama hizo huko zitokako. Hata leo tunapokwenda Supermarketi sijui kama tunajua kwa uhakika nani kachinja wale kondoo, mbuzi, kuku nk. Tujaribu kuona mbali zaidi na tuyashughulikie yaliyo matatizo ya msingi ili tuweze kusonga mbele badala ya kuendelea kuwa soko la wazungu na waarabu kwa kila kitu


2013/4/19 isack mchungu <isackmn1965@gmail.com>
MZEE Fakhi Karume
  
Kwa nini unafikiria mpango wa kugawana mabucha ilihali vitabu vitakatifu vinasema mnyama anatakiwa kuchinjwa ili atoe damu ndo anapaswa kuliwa asiliwe bila kutoa damu lakini haikusemwa nani mwenye stahili ya kumchinja huyo mnyama ili atoe damu tayari kwa kuliwa, kumbe tunapaswa kula ilimradi awe amechinjwa bila kujali nani kachinja, utamaduni wa muislam kuchinjwa kitu kilichozoeleka tu matokeo yake ikawa kama sheria, kama wasemavyo waswahili KAWAIDA NI KAMA SHREIA.


2013/4/18 Fakhi Karume <fkarume@gmail.com>
Rais mstaafu wa awamu ya pili  wa serkali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,  na wa awamu ya tatu  ya Serkali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ), Mzee Ali Hassan Mwinyi, almaarufu Mzee Rukhsa leo aliamua "
kukata jongoo kwa meno".

Mzee Rukhsa pamoja na kuwa ni mwanasiasa lakini ni mjuzi wa dini ya
kiislam pia, naweza kumuita sheikh Ali Hassan Mwinyi. Lakini katika
hili sakata la kuchinja, Mzee Rukhsa aliamuwa kuongea kama mwanasiasa
na rais mstaafu na si kama sheikh au muislam! Aliongea kwa busara
kubwa sana, huku akiepuka kuegemea upande wowote, aliongea akiwa
anajuwa kwamba jambo analoliongelea ni "tete", alichaguwa maneno,
lakini hakuogopa kumkata jongoo kwa meno.

Mzee Rukhsa aliweka wazi kabisa kwamba, kila mtu ana haki ya kichinja
au kunyonga kitoweo chake iwe paka,nyoka, panya, kuku, mbuzi, ng'ombe
n.k. Lakini ukishachinja, kula mwenyewe na watu wako au kikundi chako!
Akaeleza,  ikiwa utaamuwa kuchinja kwa ajili ya biashara watakayo
nunuwa watu wadini mbali mbali (jamii), basi utaratibu uliokuepo tangu
wakati wa mjerumani, kisha mwengereza na sasa zaidi ya miaka 50 ya
uhuru ufuatwe, kwani ndio unaofaa kwa taifa letu. Ingawa tuwaTanzania
wamoja lakini tuna dini tofauti,  lakini katika hili la kuchinja  dini
moja haina udhuru katika, lakini dini moja ina udhuru katika hilo. Kwa
vile tumekuwa tukivumiliana, kukubaliana na kushuriakiana katika
mengi,  mbali na tofauti ya dini zetu, Mwinyi anashangaa, hili la
kuchinja leo hii limetoka wapi? Mbona zaidi ya miaka 50 haijaonekana
kasoro kuchinja muislam kwa nyama ya biashara?!!! Anasema tukianza
kukagawana mabucha, hatutaishia hapo tu, tutagawana na mitaa….Temeke
watakaa hawa na Buguruni watakaa wale!

Mimi (Ally Mahadhy), naongezea ya Mzee Rukhsa, tukishagawana mitaa,
tutagawana vyombo vya usafiri (dala dala), maana kuna "dala dala"
zimeandikwa "Allah akbar" , aya za Qur'an au zina ishara za uislam
kama kuepo kwa tasbih n.k. Leo hii twajipandia tu  bila kujali ni
muislam au mkristo! Lakini tutakapo maliza kugawana mabucha, mkristo
atajiuliza kwanini apande "dala dala" ya aina hiyo wakati yeye haamini
katika hayo, kwa mujibu wa mafundisho hamtambui Allah wala haamini
chochote juu ya Qur'an! Upande mwengine, kuna "dala dala" zimeandikwa
"Yesu ni  Mungu" Yesu ni njia na uzima, zina "rozari"  ndani
zinaning'inia n.k, tunavyovumiliana, sote twapanda, haijalishi ni
mkristo au muislam! Lakini tutakapo maliza kugawana mabucha, muislam
atajiuliza kwanini nipande dala dala inayomkufuru Mungu (kwa mujibu wa
mafundisho yake)?!! Hapo ndipo "wafia dini" watakaposema tena, kuwe na
"dala dala" za waislam na wakristo!

Hatutaishia hapo, tutagawana na sikukuu zakupumzika! Hvi sasa ikifika
Christmass au Pasaka, bila kujali imani zetu, wote tunashiriki kwa
kutokwenda vibaruani.. tukishagawana mabucha, waislam watasema,
kwanini tushiriki kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu au kusulubiwa kwa
Yesu wakati hatuamini katika hayo! Hapana, christmass au pasaka ofisi
ziwe wazi! Vivyo hivyo, mpaka naandika haya ikifika Eid au "Maulid
day", kwa kuvumiliana kwetu, sote kwa umoja wetu, iwe muislam au
mkristo twafunga ofisi zetu (hatwendi vibaruani) tunasherehekea kwa
pamoja! Lakini tukishagawana mabucha, mkristo anasababu ya kujiuliza
na atajiuliza, kwanini asherehekee kuzaliwa kwa mtume wa uwongo (kwa
mujibu wa mafundisho yake) au Eid kwa kufunga ofisi! Hapana siku ya
eid au maulid ofisi ziwe wazi…hapo tena "wafia dini" watasema basi
tugawane sikukuu, waislam wapumzike zao na wakristo wapumzike zao….!

Hilo halitokuwa kikomo, tutaendelea kugawana kwa mujibu wa "wafia
dini" …tutagawana Ijumaa, Jumamosi, Jumapili, kila dini ipumzike siku
yake, kisha tutagawana  shule, vyuo vikuu, ofisi, nafasi za kazi,
nafasi za uongozi, bara bara, mpaka tutatamani na tugawane na hii
hewa, ili hewa  wanayuvuta wakristo isichanganyike  na ile wanayovuta
waislam…hapo sasa itabidi tuchinjane, ili wabaki wa dini moja tu
wavute hewa isiyonajisiwa na wa dini nyengine! Si eti eeh!

MzeeRukhsa anasema atakuwa mtu wa mwisho kusema watu wagawane mabucha
kwa misingi ya imani zao…! Mimi (Ally Mahadhy) na muuliza mzee Rukhsa,
hivi wahindu nao wakigoma MUNGU wao (NG'OMBE) asichinjwe hayo mabucha
mutagawana ili muchinjane wenyewe?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment