Friday 5 April 2013

Re: [wanabidii] ARCHIVES : DISEMBA 10 SIKU ADHIMU KWA WAZANZIBARI

Huwa hainiingii akilini kusheherekea mapinduzi bila uhuru wa zanzibar.
Nikweli sultan aliendelea kuwepo lakini nchi haikuwa koloni tena.
Watanzania kuna mambo kwa makusudi tumefichwa hasa bada ya uhuru wa
zanzibar kuna vitu vingi viliendelea ndani ya afrika mashariki wenye
kuijua historia wamenyamaza au wamenyamazishwa lakini matatizo
yataendelea kujitokeza kila siku.

On 6/24/12, Lufingo Sadiki <lufingos@gmail.com> wrote:
> or this is 1964!
>
>
> 2012/6/25 Lufingo Sadiki <lufingos@gmail.com>
>
>> I must be dreaming........!
>>
>>
>> 2012/6/24 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
>>
>>> Wazee wetu, Ndugu zetu,
>>>
>>> Assalaam Alaaykum, UMOJA NA UHURU
>>>
>>> SIKU ADHIMU KWA WAZANZIBARI
>>> Kwa Wazanzibari Disemba 10 ni siku adhimu katika taarikh ya nchi yao,
>>> ni
>>> siku inayoishi katika nyoyo zao kwa fakhari na machungu. Disemba 10
>>> inaishi
>>> kwa fakhari nyoyoni mwa Wazanzibari kwa kuwa ndio siku ya Uhuru wa
>>> nchi yao.
>>> Siku ambayo Wazanzibari waliirejeshea nchi yao - Zanzibar - Uhuru wake
>>> baada
>>> ya juhudi zao mbali mbali na kwa kujitolea kwa hali na mali. Disemba
>>> 10
>>> inaishi katika nyoyo za Wazanzibari kwa machungu na huzni kwa vile
>>> Uhuru wa
>>> Zanzibar na Zanzibar huru haikuishi zaidi ya siku thalathini na tatu,
>>> bali
>>> ilivamiwa na kumezwa na Dodoma chini ya kisingizio cha muungano. Huo
>>> ukawa
>>> ndio mwisho wa Zanzibar na mwanzo wa masaaibu yote ya Zanzibar. Kwa
>>> munasaba
>>> huu adhimu, yaani leo kufika miaka 37 tangu ile Disemba 10, 1963;
>>> tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na tunawaombea dua wazee wetu na
>>> ndugu
>>> zetu waliotangulia mbele ya Haki na waliopo ulimwenguni kwa juhudi zao
>>> hizo,
>>> Mwenyezi Mungu awajazi kila la kheri duniani na Akhera - Amin. Dua
>>> zetu
>>> vilevile ziwafikie wazee na ndugu zetu waliouliwa mashahidi katika
>>> ghasia za
>>> Juni 1961 na katika mavamizi ya Januari, 1964 na mashahidi wetu wote
>>> wengine
>>> wa kabla na wa baada – Mwenyezi Mungu awarehemu na awatie Peponi kwa
>>> Rehema
>>> Zake – Amin. Kwa munasaba huu, munasaba wa furaha ya wiki chache na
>>> munasaba wa msiba na masaaibu yanaoendelea mpaka hii leo, Umoja wa
>>> Wazanzibari – Zanzibar Organization - kwa hishima unaleta mbele yenu
>>> humu
>>> barazani haya yafuatayo ili tushirikiane katika kuzingatia na tufikiri
>>> kwa
>>> pamoja namna ya kutengeneza kwa maslaha ya Zanzibar ya leo na ya
>>> kesho.
>>>
>>> DOLA HURU YA ZANZIBAR
>>> Kwa Rehma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na juhudi za Wazalendo wa
>>> Kizanzibari
>>> wazee wetu katika uwongozi wa "Umoja wa Wazanzibari" (ZNP/ZPPP),
>>> manamo saa
>>> sita na dakika moja za usiku wa kuamkia taarikhi 10 Disemba 1963;
>>> waliirejeshea Zanzibar Uhuru wake na kuwa ni Dola Huru Kaamili
>>> miongoni mwa
>>> dola za ulimwengu. Katika kutekeleza jambo adhimu hilo, bendera
>>> nyekundu
>>> iliteremsh-wa kutoka kwenye mlingoti wake na Bendera ya Dola Huru ya
>>> Zanzibar yenye karafuu mbili (zikimaanisha visiwa viwili vya karafuu,
>>> Unguja
>>> na Pemba) ilipandishwa na kupepea katika mlingoti uliokuwepo kwenye
>>> ardhi ya
>>> Zanzibar katika uwanja wa Mivinjeni (Coopers Insititute). Kwa vile
>>> Zanzibar
>>> haikuwa koloni ya Muingereza, basi haikuwepo bendera ya Kiingereza
>>> kuteremshwa, kwa sababu haikupatapo kupepea juu ya ardhi ya Zanzibar.
>>> Japokuwa Zanzibar ilitiwa kwa mbinu za Waingereza chini ya himaya ya
>>> Kiingereza, haikuwa koloni kama vile koloni nyenginezo za
>>> Kiingereza.
>>> Zanzibar haikusita kuwa Dola kwa muda wote iliokuwa chini ya himaya
>>> ya
>>> Muingereza, iliendelea kuwa Dola na kila lake na chake. Zanzibar
>>> imesita
>>> kuwa Dola baada ya kuvamiwa na kutiwa chini ya makucha ya Dodoma pale
>>> 1964.
>>>
>>> SHEREHE ZA UHURU
>>> Wananchi wote wakubwa na wadogo, wanaume na wanawake, waliupokea Uhuru
>>> wa
>>> nchi yao kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa furaha na
>>> bashasha
>>> kubwa. Mji ulikuwa ukin'gara kwa mapambo ya namna mbali mbali.
>>> Tamasha hizi
>>> na zile zilifanywa na wananchi kwa kufurahikia Uhuru wao. Sherehe na
>>> mapambo
>>> hayakuwa Mjini tu, bali mashamba kote. Na huko Pemba nako kulifanywa
>>> sherehe
>>> kama za Unguja, tangu mijini mpaka mashamba. Wazanzibari walijaa tamaa
>>> na
>>> matumainio ya kwamba baada ya juhudi na kazi ngumu ya kuleta Uhuru wao
>>> na
>>> kwa kuondoka mtawala Muingereza sasa wataweza kushirikiana Wazanzibari
>>> wote
>>> bila ya ubaguzi wa aina yoyote ile katika kazi ngumu na ndefu ya
>>> kujenga
>>> nchi yao kwa masalah ya nchi yao. Tamaa na matumainio haya yalitokana
>>> na
>>> imani yao Wazanzibari juu ya uwongozi wa umoja wao - "Umoja wa
>>> Wazanzibari"
>>> - uliojengeka katika misingi ya uadilifu wa haki sawa kwa wote. Haya,
>>> yaani
>>> uadilifu wa haki sawa kwa wote yalithibitishwa kwa vitendo kama vile
>>> alivyotueleza Sheikha Ali Muhsin katika kitabu chake: "Conflicts and
>>> Harmony
>>> in Zanzibar", yeye katueleza haya yafuatayo:
>>>
>>> ZNP/ZPPP FOR ALL PEOPLE.
>>> Our very restricted resources compelled us to have our diplomatic
>>> offices in
>>> New York also accredited to Washington, in London accredited to the
>>> rest of
>>> Europe, in Cairo to cover the rest of the Arab world, and in due
>>> course
>>> Indonesia, which was importing the greatest share of our clove
>>> production,
>>> to be the base for the rest of Asia.
>>>
>>> While we made certain that the ambassador and the counsellor (his
>>> second in
>>> command) were our political nominees, being supporters of the ZNP/
>>> ZPPP
>>> alliance, we appointed the first secretaries by virtue of merit
>>> irrespective
>>> of their political affiliation. Thus the first secretary to the UN
>>> embassy
>>> happened to be Khamis Hassan Ameir, to the Cairo embassy was Ali
>>> Khamis
>>> (once speaker to the Zanzibar House of Representatives), and the would-
>>> be
>>> first secretary to Indonesia was to be Ali Hassan Mwinyi. (he later
>>> became
>>> President of Tanzania.) All three were known to us as supporters of
>>> the
>>> ASP. Professionally they had the capacity to fill the posts, and that
>>> was
>>> all that mattered to us. It was not very easy to convince everybody in
>>> our
>>> party's national executive of the fairness and wisdom of making these
>>> appointments, but I did manage at last to get unanimous support by
>>> reminding
>>> my colleagues that ours was, from the very beginning, a vanguard
>>> party
>>> working for the whole nation and not for a segment of the population.
>>>
>>> Such and other measures began to have a telling effect on the more
>>> thinking
>>> section of the opposition, particularly the younger educated elements
>>> aspiring for higher things in the future. They were pleasantly
>>> surprised to
>>> find that the ZNP/ZPPP government was being fair and just, and that
>>> it
>>> assessed people according to merit irrespective of their political
>>> connections. There was even some talk about their joining the ruling
>>> alliance en masse. This was a threat to the semi-literate leadership
>>> of the
>>> ASP, the newly created Umma party and their common boss across the
>>> channel.
>>> The longer the government stayed in power the more popular it was
>>> bound to
>>> make itself, and the more likely the opposition would be losing
>>> support.
>>> Thus was it imperative that the rebellion had to take place as soon
>>> as
>>> possible. And thus it was that after the general massacre of the
>>> thousands
>>> of the ZNP/ZPPP supporters Karume and his immediate thug supporters
>>> began
>>> murdering one by one the educated elements in the ASP whom they had
>>> always
>>> suspected of considering changing their allegiance. Othman Sharif,
>>> Kasim
>>> Hanga, Mdungi Usi, Twala, Jaha Ubwa and many others were liquidated.
>>> Dr.
>>> Kingwaba was disgraced. From being a successful qualified medical
>>> officer he
>>> was put in charge of the post office. Dr. Ahmed Rashid, a veterinary
>>> officer made into a Director of Economy, had to flee for his life. He
>>> died
>>> in Britain.
>>> (Conflicts and Harmony in Zanzibar – page 216)
>>>
>>> "Umoja Wa Wazanzibari" katika misingi yake kuwa ni Umoja wa
>>> Wazanzibari wote
>>> ulitekeleza mipango yake yote katika misingi hio. Wazanzibari
>>> walitambua
>>> vyema kuwa baada ya hivi kupatikana Uhuru kulikuwa na kazi kuu mbele
>>> yao,
>>> yaani kujenga nchi ni kazi ndefu na ngumu sawa au zaidi kuliko ile ya
>>> kuleta
>>> Uhuru. Juu ya hivyo, walikuwa tayari kubeba jukumu hilo kwa azma na
>>> shajaa
>>> kwa sababu imani yao ni kwamba utumishi wa nchi ni wajibu wa kila
>>> mwananchi
>>> na ni wenye kuhisabiwa na kulipwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
>>>
>>> ZANZIBAR INAJIUNGA NA UMOJA WA MATAIFA
>>> Baada ya kupata Uhuru wake Zanzibar, taarikh 14 Disemba, 1963
>>> ilijiunga na
>>> Jumuia ya Umoja wa Mataifa (UNO) ikiwa ni mwanachama kamili wa Jumuiya
>>> hio
>>> ya kilimwengu. Kwa munasaba huu nina inukulu hapa (tena) khutuba ya
>>> Waziri
>>> Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Muhammad Shamte katika Umoja wa Mataifa
>>> (UNO)
>>> taarikhi 16 Desemba, 1964 ikikaribishwa Zanzibar kuwa ni mwanachama
>>> wa
>>> Jumuia hii muhimu ya kilimwengu.
>>>
>>> A REMINDER SPEECH
>>> Prime Minister Muhammed Shamte Hamad (as Head of Government of the
>>> independent and Sovereign State of Zanzibar) delivered the following
>>> historic speech on the historic day of 16th December, 1963 to the
>>> General
>>> Assembly of the United Nations Organization in New York.
>>>
>>> Mr. President!
>>> It is a very great honour and a very great pleasure for me to be here
>>> as
>>> Zanzibar's representative at the moment when Zanzibar's application to
>>> join
>>> the United Nations Organization has been accepted by the General
>>> Assembly.
>>> Zanzibar's entry to this great Organization is to my mind of special
>>> significance, and this is that there is no country so small and so
>>> modest in
>>> its means that it cannot be represented here in equal terms with the
>>> great
>>> nations of the world. There are some people who consider this scheme
>>> of
>>> things to be wrong. But I consider it to be a source of strength to
>>> this
>>> Organization, and that one that will inspire Zanzibar to use its
>>> privileges
>>> with a sense of responsibility and dedication to the ideals which
>>> prompted
>>> the establishment of the United Nations.
>>>
>>> To our many friends throughout the world who have done so much in
>>> supporting
>>> our struggle towards national liberation, to the Decolonization
>>> Committee
>>> which has contributed so much in speeding up our march to
>>> Independence, and
>>> to this august Organization of the United Nations to which we owe so
>>> much, I
>>> would like to convey my country's deep gratitude. To them we continue
>>> to
>>> look for aid and support in the upliftment of our people so that we
>>> may also
>>> be able to contribute our humble share towards the solution of the
>>> world's
>>> problems. To the distinguished delegates in the Security Council and
>>> in this
>>> General Assembly who paid tributes to the struggle and achievements of
>>> my
>>> country I would like to convey the sincere gratitude of my
>>> delegation. To
>>> all those who have sponsored our application, and to all the
>>> distinguished
>>> delegates who have unanimously voted us into membership of the United
>>> Nations, I say: Thank you.
>>>
>>> Mr. President. Political problems tend to hit the world headlines,
>>> but it
>>> is not generally known, for instance, that malaria which a few years
>>> ago
>>> used to cause as much havoc as any war, is now almost wiped out from
>>> Zanzibar, as a result of an intensive joint effort on the part of
>>> WHO,
>>> UNICIEF and the Government and people of Zanzibar. It is also not
>>> known
>>> that quietly but determinantly we are trying with the aid of the ILO
>>> and FAO
>>> to do away with the curse of under-employment. There are many other
>>> ways in
>>> which individual countries and international organizations have been
>>> co-operating with us in solving our problems. We are grateful to them
>>> all.
>>>
>>> Now that the energies of our people are unleashed by the restoration
>>> of our
>>> national pride and sovereignty we can look forward with confidence to
>>> greater and more comprehensive assistance from every quarter.
>>> Zanzibar is
>>> one of the smallest nations in terms of population and size to be
>>> accepted
>>> for membership. This in itself entails sacrifices for Zanzibar,
>>> sacrifices
>>> which are of little significance to nations of great wealth, but are
>>> of very
>>> great concern to us of slender means. These sacrifices we are very
>>> glad to
>>> make. If we are not rich in numbers, in territory, in material wealth
>>> we do
>>> not count ourselves poor in values of life which are so inestimably
>>> more
>>> important; and it is because of this that we feel we can contribute,
>>> even if
>>> only modestly, in the affairs of this Assembly.
>>>
>>> We have a long and honourable history and civilization behind us.
>>> Like so
>>> many of the great peoples of the world our roots are sprung from many
>>> different sources, from Africa primarily, but also from Arabia, from
>>> the
>>> civilization of Asia, Persia, from India and from many others. The
>>> Europeans in their great voyages of exploration found succour and
>>> sustenance
>>> on our shores. And men of many races found rest and stability in our
>>> islands from where to organize the exploration and development of
>>> Central
>>> and Eastern Africa It is due to these roots established over
>>> centuries, the
>>> mixing of so many cultures, that make us proud of our reputation for
>>> moderation and friendliness. While in the modern world we do not
>>> intend
>>> looking back to our past, it is this tradition on which we intend to
>>> build
>>> our future.
>>>
>>> Zanzibar is a constitutional monarchy founded on liberal and
>>> democratic
>>> traditions, governed by a Prime Minister and a Cabinet of elected
>>> Ministers,
>>> with collective responsibility and answerable to a National Assembly
>>> elected
>>> on the basis of universal adult suffrage. The Fundamental Human
>>> Rights to
>>> personal liberty and protection against discrimination are entrenched
>>> in
>>> Zanzibar's Constitution. Our overall aims are peace and progress at
>>> home
>>> and abroad. The chief object must be to help create a political
>>> atmosphere
>>> in the world in which man's real enemies of hunger, ignorance and
>>> disease
>>> can receive full attention so that resources and time are not wasted
>>> on
>>> fruitless matters of dissension. Zanzibar's general policy is one of
>>> benevolent and positive neutrality without discrimination against any
>>> country on grounds of race, creed, culture or ideology. It supports
>>> all
>>> measures of peace in the world on the basis of international
>>> cooperation. On
>>> the achievement of its independence Zanzibar has freely elected to
>>> remain a
>>> Member of the Commonwealth of Nations, and it is fitting and
>>> pleasurable to
>>> pay tribute to the continuing harmonious relations which have
>>> obtained
>>> between Zanzibar and the United Kingdom. We believe in the
>>> Commonwealth as
>>> a large number of equal and sovereign states of many peoples and
>>> cultures
>>> who have voluntarily and democratically joined together and are
>>> dedicated to
>>> the furtherance of peace, co-operation and prosperity throughout the
>>> world.
>>>
>>> It is the object of Zanzibar to strengthen the many ties it possesses
>>> with
>>> both Africa and the East. To this end we subscribe to the principles
>>> of the
>>> Bandung Declaration of 1955 and of the Charter of the Organization of
>>> African Unity framed at Addis Ababa this year. Zanzibar has
>>> particularly
>>> close relationship with the other territories of East Africa, and it
>>> is our
>>> intention to continue this in friendship and co-operation, whether
>>> inside or
>>> out of a form of an East African Federation. In this respect I am
>>> particularly glad that Kenya with which Zanzibar has so many close
>>> connections is being welcomed into this Assembly at the same time. At
>>> this
>>> proud moment in our history I may be permitted to quote Shakespeare
>>> and say:
>>> "We are two lions littered in one day."
>>>
>>> Sir, In submitting the application for membership for Zanzibar I have
>>> made a
>>> solemn declaration in common with that made by other nations
>>> represented
>>> here today that on behalf of my government I have accepted the
>>> obligations
>>> contained in the Charter of the United Nations, and have undertaken
>>> to
>>> fulfil them. This solemn declaration is a very real one for me, and I
>>> pray
>>> that this indeed will be so, and that Zanzibar in future will honour
>>> it to
>>> the full. Thank you, Sir.
>>>
>>> MAVAMIZI YA JANUARI 12, 1964
>>> Ole wetu! vitumishi vilikuwa vimeshawekwa tayari na mabwana zao
>>> kuufisidi
>>> na kuuvuruga Uhuru, bali kuivuruga Nchi na wananchi wake. Sherehe
>>> hazikuwahi kumalizika, wala majasho hayakuwahi kukauka mwilini
>>> kutokana na
>>> juhudi na mbio za kugombea Uhuru wetu, bali ghafla tulijishitukia
>>> katika
>>> msiba, tushavamiwa. Na huo ulikuwa ndio kuanzia kwa maafa ya Zanzibar
>>> na
>>> kupotea kwa kila kheri yake na kumezwa Dola ya Zanzibar na kutiwa
>>> chini ya
>>> makucha ya Dodoma kwa kisingizio cha muungano.
>>>
>>> Mafisadi wachache kwa ajili ya maslahi ya nafsi zao hawakutahayari
>>> wala
>>> hawakuona vibaya hata kidogo kuchan-ganyika na wageni waliokuwepo
>>> ndani ya
>>> nchi na walioletwa kutoka nchi za jirani kwa makusudio khasa ya
>>> kuivamia
>>> Zanzibar na kuiondoa Serikali ya wanan-chi na kuimeza Dola ya
>>> Zanzibar.
>>> Wananchi mafisadi hao walikubali kuongozwa na wageni, John Okello
>>> aliyetoka
>>> kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka kwao
>>> Tanganyika, kuivamia nchi yao katika siku wa manane wa kuamkia
>>> taarikh 12
>>> Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao
>>> hawakuhisi uchungu wala fedheha kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza
>>> roho za
>>> wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha
>>> huyo
>>> aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John
>>> Okello,
>>> amesema kuwa watu waliokufa (waliouliwa) katika 'mavamizi' hayo ni
>>> 13,000.
>>> Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja yeye.
>>>
>>> Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi vilivyokuwa
>>> na
>>> ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi
>>> waliokuwa
>>> wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia
>>> yametokea
>>> Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'. Ilifika hadi,
>>> siku hiyo
>>> ya 'mavamizi' majahil na makatili hao ku-wanajisi maiti wa kike.
>>> Kitendo
>>> hicho hakijapa-tapo kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye
>>> ubinaadamu na ustaarabu wake.
>>>
>>> MWALIMU NA MAVAMIZI YA ZANZIBAR
>>> Sote tunakumbuka uzuri maneno ya Mwalimu aliposema, "Lau kuwa nnaweza
>>> basi
>>> ningali viburura Visiwa hivi (Zanzibar) hadi katikati ya Bahari ya
>>> Hindi".
>>> Na hivyo ndivyo alivyokuwa akifanya Nyerere mpaka kuondoka kwake
>>> ulimwenguni
>>> na ndivyo wanavyofanya warithi wake hadi hii leo, wamo kuviburura
>>> Visiwa
>>> vyetu kuelekea baharini. Tafauti iliyopo baina ya jana na leo ni kuwa
>>> hii
>>> leo vuta-ni-kuvute baina ya Dodoma na Wazalendo wa Kizanzibari imezidi
>>> kuwa
>>> kubwa kwa vile kila siku upande wa wananchi unazidi Umma na
>>> unazidi
>>> nguvu. Umma unazidi kufahamu madhila ya kutawaliwa na haja ya
>>> kurejesha
>>> Dola yao Huru ya Zanzibar ili warejeshe ubinadamu wao na waweze
>>> kuishi
>>> kibinadamu.
>>>
>>> KUMEZWA DOLA YA ZANZIBAR
>>> Sote tunafahamu ya kwamba mara baada ya mavamizi ya Januari 1964,
>>> mwaka huo
>>> huo; mwezi wa Aprili Zanzibar ilitiwa chini ya makucha ya Dodoma kwa
>>> kisingizio cha muungano. Kutokana na "Articles of Unions" Zanzibar
>>> ilipoteza
>>> Dola yake na kuwa ni koloni la Tanganyika. Mengi yamesemwa juu ya
>>> suala
>>> hili, ya hivi karibuni ni haya waliosema wao wenyewe, katika kitabu
>>> chake
>>> "The Political Plight of Zanzibar", Profesa Maliyamkono katika ukurasa
>>> wa
>>> 198-199 ametueleza haya kukhusu huu unaoitwa muungano:
>>>
>>> "Defining Union Matters
>>> One of the thorniest problems facing the Union has been that of
>>> deciding on
>>> the formula for the relative contribution of each part of the Union to
>>> the
>>> fiscal requirements of the Union. This requires first a decision or
>>> what
>>> government activities should constitute Union matters.
>>> Constitutionally, the
>>> Union matters have their history in the "Articles of the Union",
>>> signed by
>>> the two founders of the Union, Mwalimu Julius K. Nyerere, on behalf
>>> of
>>> Tanganyika, and Sheikh Abeid Karume, on behalf of Zanzibar.
>>>
>>> The Interim Constitution based on the Articles of the Union, stated
>>> that the
>>> issues for which the Union Government and Union Parliament had direct
>>> responsibility were these:
>>>
>>> 1. The Constitutions and Government of the United Republic
>>> 2. External Affairs
>>> 3. Defence
>>> 4. Emergency Powers
>>> 5. Citizenship
>>> 6. Immigration
>>> 7. External Trade and External Loans
>>> 8. The Public Service of the United Republic
>>> 9. Income and Corporate Tax, Customs and Excise Tax
>>> 10. Harbous, Civil Aviation Post, and telegraphs
>>>
>>> It is however, debatable whether all the above 10 areas are
>>> exclusively
>>> Union matters as the Interim Constitution may have intended them to
>>> be.
>>> Obvious queries arise with regard to 7 & 8, for example. With regard
>>> to No.
>>> 7, Zanzibar runs its own external trade and even keeps its own
>>> statistic on
>>> foreign trade and payments. As for No. 8 the implication is that there
>>> is a
>>> Union Service Commission.
>>> There is none.
>>>
>>> The list of Union "matters" was increased to 21 when the Constitution
>>> of the
>>> United Republic was published in 1997. These were:
>>>
>>> 11. All Banking and Currency Matters
>>> 12. Industrial Licences and Statistics
>>> 13. Higher Education
>>> 14. Petroleum Natural Resources
>>> 15. National Examination Council
>>> 16. Air Transport and Communication
>>> 17. Research
>>> 18. Meteorology
>>> 19. Statistics
>>> 20. United Republic Court of Appeal
>>> 21. Registration of Political parties
>>>
>>> Again it is doubtful that all these additional activities are
>>> exclusively on
>>> effectively Union Matters
>>>
>>> The Shellukindo Committee (see below) expanded the scope of the Union
>>> based
>>> on the argument that most ministries in SMT have some Union element.
>>> Thus
>>> the Presidency is to a certain extent a union matter. Every ministry
>>> in the
>>> SMT which deals with international agencies on behalf of the entire
>>> United
>>> Republic is involved in a "Union" activity. This is the widest
>>> definition
>>> of Union matters and the definition in the Interim Government is the
>>> narrowest."
>>>
>>> Ndugu zangu, huu ndio muungano; muungano ambao tangu ulipoundwa
>>> ulikwisha
>>> ipoteza Dola ya Zanzibar kwa kunyang'anywa Zanzibar mambo 10 ambayo
>>> ndio uti
>>> wa mgongo wa Dola. Baadae polepole ndio 11 mengine kuongezwa na hapa
>>> kuimaliza Zanzibar. Yote haya ni kizungumkuti, hapana lenye
>>> kufahamika; ni
>>> kuzongwazongwa tu, lakini haya maneno: "Thus the Presidency is to a
>>> certain
>>> extent a union matter", ndio zaidi hayafahamiki. Jee Raisi wa
>>> Zanzibar ana
>>> uwezo gani? Kwa kumaliza muandishi ametwambia kuwa: "This is the
>>> widest
>>> definition of Union matters and the definition in the Interim
>>> Government is
>>> the narrowest". Kweli ilioje! Kweli ikidhihiri uwongo hujitenga.
>>>
>>> Wazee wetu, ndugu zetu, Wazanzibari huu ndio "muungano" na hivi
>>> ndivyo
>>> ilivyofikishwa Zanzibar ndani ya huu "muungano".
>>>
>>> Matumainio yetu sote ni kwamba sisi ni watu wazima na wenye fahamu
>>> kamili,
>>> sio watoto wadogo wala sio tusiofahamu. Mwenye macho haambiwi
>>> tizama. Nini
>>> la kutenda hili ndio suala muhimu, lakini la kutenda ni lazima
>>> Wazanzibari
>>> waamue na kwa haraka kwani kila tukichelewa ndio khatari inazidi.
>>> "The
>>> list of Union "matters" was increased to 21 [when the Constitution of
>>> the
>>> United Republic was published] in 1977." Hapa haioneshi kuwa hii
>>> constitution inayosemwa kuwa ilizungumzwa na kukubaliwa na kila upande
>>> -
>>> Zanzibar na Tanganyika - kisha ndio ikawa "published". Msiba ni
>>> kwamba
>>> inawezekana wakati wowote ule hii constitution ikawa "published" na
>>> kuongezwa orodha nyengine, kama kiko bado ambacho hakijachukuliwa na
>>> kutiwa
>>> ndani ya huyu jini anaeitwa "Union matters".
>>>
>>> DHULMA NI MOTO USIOKUWA NA BWANA
>>> Kutokana na fisadi na fitina zilizokuwa zikiongozwa na Nyerere na
>>> kusaidiwa
>>> na mabwana zake pamoja na vibaraka vyao, Zanzibar ilivamiwa na kutiwa
>>> chini
>>> ya utawala wa Dodoma kwa kisingizio cha muungano. Yote haya ni
>>> kuendeleza
>>> vita vya msalaba dhidi ya Waislamu. Walimwengu mbali mbali kwa
>>> kusikiliza
>>> fitina hizo - ambazo zilipandikizwa kuwa ati iliopinduliwa Zanzibar
>>> ni
>>> serikali ya Kisultani na Kiarabu - walisherehekea maovu yote yale
>>> yaliotendewa Zanzibar. Wengi wa walimwengu walikuja Zanzibar
>>> kusherehekea
>>> mauaji, kunajisiwa binadamu – wake kwa waume, wakubwa kwa wadogo;
>>> kunyang'anywa watu haki zao, tujazwa magerezani mamia ya binadamu bila
>>> ya
>>> kosa na bila ya kupelekwa mahakamani, kuwabidi mamia ya binadamu
>>> kuihama
>>> nchi yao bila ya kujuwa wanakimbilia wapi. Walimwengu walisherehekea
>>> na
>>> kuyakiri maovu hayo, walimwengu hao wakiwemo Waislamu walikiri
>>> kutendewa
>>> binadamu dhulma. Dhulma hii walifanyiwa Wazanzibari, lakini walisahau
>>> kuwa
>>> dhulma ni moto, moto hauna mipaka wala hauna bwana. Moto huu wa
>>> dhulma
>>> ulienea ghafla Afrika nzima, kuanzia Afrika Mashariki na kwengineko.
>>> Serikali kadhaa wa kadhaa zilipinduliwa na watu kupata kila maafa,
>>> wengi
>>> iliwabidi wazihame nchi zao ili kukimbia maovu waliokuwa wakitendeana
>>> wenyewe kwa wenyewe. Mnyonge kudhiliwa ilikuwa ndio mtindo wa kila
>>> siku.
>>> Haya yote ni kwa sababu ilipotokea dhulma Zanzibar hapana alieinua
>>> sauti
>>> yake kuiteta, kinyume chake, wengi waliikiri na kuisherehekea, kwa
>>> sababu
>>> Nyerere kawaambia kuwa waliofanyiwa hivyo ni kina sultani – kwahivyo
>>> wanafaa
>>> kudhulumiwa. Walisahau kuwa dhulma ni moto, hauna mipaka wala hauna
>>> bwana.
>>>
>>> HATUTENGENEKEWI MPAKA TUONDOE DHULMA
>>> Wazanzibari tusitaraji kupata Nusra ya Mwenyezi Mungu mpaka kwanza
>>> tutake
>>> toba ya kweli, hapo tena ndio tuombe Nusra ya Mwenyezi Mungu ambayo
>>> ndio
>>> pekee itakayo tuvua na maafa na balaa hii tunayoishi nayo tangu pale
>>> tulipoingia katika dhulma. Toba ya kweli ina shuruti zake, miongoni
>>> mwa
>>> shuruti hizo ni kujuta kwa tuliotenda na kuazimia tusirejee tena
>>> kutenda
>>> maovu hayo. Vilevile shuruti zake ni kutenda mema kwa kuondoa dhulma
>>> na
>>> kuleta haki na kumpa kila mwenye haki yake haki yake. Haiwezekani
>>> kujenga
>>> haki na uadilifu juu ya dhulma, ni lazima kwanza tuondoe dhulma ndio
>>> tuweze
>>> kujenga haki na uadilifu. Huwezi kupanda mmea ndani ya biwi la moto.
>>>
>>> TUME YA KUCHUNGUA DHULMA
>>> Kwa makusudio ya kutengeneza na kutafuta Nusra ya Mwenyezi Mungu kwa
>>> kuondoa
>>> dhulma na kujenga haki na uadilifu tunamuomba Bwana Aman ateue tume
>>> maalumu
>>> ichungue juu ya dhulma zote tulizotendeana na kupangwa njia ya
>>> kuziondoa
>>> dhulma hizo na kujenga haki na uadilifu badala yake. Kitendo hichi ni
>>> cha
>>> dharura ili tuweze kupata Nusra ya Mwenyezi Mungu na tuweze kutarajia
>>> kuokoka kutokana na haya maafa tunayoishi nayo tangu pale tulipojitia
>>> katika
>>> dhulma kwa mikono yetu.
>>>
>>> SERIKALI YA UMMA NDIO HAJA YA UMMA
>>> Matokeo ya uchaguzi wote uliofanywa Zanzibar tangu wa 1961 na mpaka wa
>>> 1963,
>>> wa 1995 na huu wa leo 2000; yote inaonesha na kuthibitisha haja ya
>>> Umma wa
>>> Zanzibar kuwa haja yao ni "Serikali ya Umma". Umma wa Zanzibar
>>> haukubali
>>> kugawika mafungu mafungu, hata kama vitaletwa vyama zaidi ya
>>> ishirini. Umma
>>> wa Zanzibar uamuzi wao ndio ule ule, tangu mababu, mababa na hata
>>> watoto, na
>>> ndivyo itakavyokuwa hata kwa wajukuu na vilembwe. Umma wa Zanzibar
>>> ushaamua
>>> na maamuzi yao ndio ya mwisho, haja ya Umma wa Zanzibar ni Serikali ya
>>> Umma.
>>> Wazanzibari hawataki kuzidi kufarikishwa kwa kugawiwa vifungu
>>> vifungu.
>>> Waliokuwa ZNP/ZPPP ndio weshakuwa na waliokuwa ASP ndio weshakuwa. Ni
>>> wajibu
>>> wa ndugu zetu walioko katika uwongozi waikubali hali ilivyo na kwa
>>> ilivyo
>>> ndivyo twende, kutaka la muhali ni muhali; kutaka Wazanzibari
>>> wabadilike ni
>>> muhali na kwenda kinyume na matakwa ya Umma ni kutaka muhali. Umoja
>>> wa
>>> Wazanzibari muda wote huo ulikuwa daima unalingania kuundwa Serikali
>>> ya
>>> Umma, kwa vile kufahamu umuhimu wake na kwa kutambuwa matakwa ya
>>> Wazanzibari. Umoja wa Wazanzibari uliendelea na unaendelea kulingania
>>> Serikali ya Umma mpaka hii leo.
>>>
>>> SERIKALI IMEFANYA MWANZO MWEMA
>>> Alhamdulillah serikali chini ya uwongozi wa ndugu yetu Bwana Aman
>>> Abeid Aman
>>> imeanza kwa kuleta ishara njema za kutaka kuleta umoja wa Wazanzibai
>>> kwa
>>> hivi kuchaguwa Baraza la Mawaziri ambalo linamathili zaidi uwananchi.
>>> Hii
>>> ni khatuwa njema ambayo ni busara kuipa mwega zaidi na kuiombea kheri
>>> na
>>> mafanikio. Lakini basi, itakuwa ni busara na kheri zaidi iwapo Sheikh
>>> Aman
>>> atachukuwa khatuwa zaidi na kuwataka ndugu zetu CUF kuingia katika
>>> serikali
>>> kwa kuundwa Serikali ya Umma. Hapana shaka kuwa na ndugu zetu CUF
>>> kwa
>>> maslaha ya nchi yetu wataipokea khatuwa hio kwa moyo mkunjufu na
>>> kushirikiana na kufungua ukurasa mpya. Kama inavyoaminiwa na wengi
>>> kuwa CCM
>>> na CUF wanao kiasi ya 90% ya Umma wa Zanzibar na kiasi ya 10% ndio
>>> sehemu ya
>>> Umma ambo kwa ilivyo ni kuwa wao hawana chama maalumu. Wote hawa ni
>>> wananchi
>>> na wana Haki na Wajibu sawa ambao ni lazima kutekelezwa kwa
>>> kushirikishwa
>>> katika serikali yao, hivyo ndivyo itakavyofanya hio "Serikali ya
>>> Umma",
>>> serikali ya wananchi wote.
>>>
>>> MASHAURI JUU YA HIO SERIKALI YA UMMA
>>> Kukhusu hio "Serikali ya Umma" tunapenda kutoa raia kuwa iwe ya muda
>>> wa
>>> miaka sita badala ya miaka mitano, na kila upande upate fursa ya kuwa
>>> katika
>>> uwongozi wa Serikali hio kwa kipindi cha miaka mitatu. Hivi kwa maana
>>> miaka
>>> mitatu ya mwanzo kwa mfano CCM ndio watakaochagua Rais na CUF
>>> watachagua
>>> Waziri Mkuu. Na baada ya miaka mitatu watabadilisha, CUF watachagua
>>> Rais
>>> na CCM watachagua Waziri Mkuu. Vilevile, ikiwa hio Serikali ya Umma
>>> ina
>>> mawaziri 14, basi sita iwe kutoka katika CCM na sita kutoka katika CUF
>>> na
>>> wawili kutoka katika huo Umma wa 10%. Hali hii itawafanya wananchi
>>> wote
>>> kupata kushirikishwa katika serikali ya nchi yao bila ya ubaguzi
>>> kutokana na
>>> fikra za kisiasa au ubaguzi wowote ule.
>>>
>>> KAMATI ZA UTENDAJI
>>> Badala ya Waziri, ni kuundwa Kamati ya Utendaji, kamati hizi zitakuwa
>>> badala
>>> ya Waziri; kwa mfano badala ya Waziri wa Fedha itakuwa ni Kamati ya
>>> Fedha.
>>> Kwa mfano kila Kamati itakuwa na wawakilishi watano, wawili kutoka
>>> katika
>>> CCM na watatu kutoka katika CUF na Kamati nyengine itakuwa na
>>> Wawakilishi
>>> watatu wa CCM na wawili wa CUF, na kadhaalika. Wawakilishi watano
>>> hawa
>>> wanne watakuwa ni wanachama wa hio kamati yao na mmoja wao kati ya hao
>>> wanne
>>> atakuwa ni mwanachama na Katibu wa Kamati yao na watano wao ndie
>>> ataekuwa
>>> Mwenyekiti wa Kamati. Nyadhifa hizi zitakuwa kwa kubadilishana kwa
>>> baada ya
>>> kila muda. Mpango huu licha ya kuwa utawapa Wawakilishi nyenzo ya
>>> kuthibitisha uwezo wao katika kutekeleza dhamana walizotwika na Umma
>>> waliowachaguwa, Umma unaotarajia upate utumishi wa Wawakilishi wao,
>>> bali
>>> zaidi utaondoa uwezekano wa ubadhirifu wa mali ya Umma na utumiaji
>>> muovu wa
>>> wadhifa na uzorotaji wa utendaji na utekelezaji. Zaidi ya haya,
>>> mpango huu
>>> utaleta utaratibu wa kuwepo "collective responsibility and
>>> accountability"
>>> juu ya wote watakaoshiriki katika utumishi wa serikali. Ikiwa ni sifa
>>> ni
>>> sifa ya wote, na ikiwa upungufu ni wote ndio wenye kuhisabiwa kwa
>>> upungufu
>>> huo.
>>>
>>> SERIKALI YA UMMA HAIMUONDOI WA ZAMANI
>>> Kwa maumbile yetu, na kwa ilivyofanywa; kufika katika madaraka
>>> imekuwa ni
>>> njia ya kipato na njia ya kujijengea fakhari na kiburi. Kutokana na
>>> hali
>>> hii, wengi wetu tunataka "kufa kupona" lakini nifike katika utawala
>>> (na
>>> nisitoke katika utawala) ili niweze kupata chochote na niweze kuwa
>>> bwana
>>> mkubwa, niweze kutenda ninavyopenda bila suala wala jawabu. Niweze
>>> kuchuma
>>> (kwa njia ya haramu) kwa upesi kama nitakavyo weza kabla ya kuondoka
>>> kwenye
>>> utawala. Nihakikishe kuwa sitoki katika utamu na raha hizi. Hali hii
>>> haiwezi
>>> kufutika nyoyoni mwetu leo au kesho, itachukuwa muda; muda ambao
>>> utalazimu
>>> uwe na mfunzo ya kuendelea na kudumu juu ya "UWONGOZI NA DHAMANA
>>> ZAKE".
>>> Inahitaji tumjuwe na tumche Mwenyezi Mungu katika dhamana ya uwongozi,
>>> hapo
>>> ndipo tutakapoweza kupata waongozi wa kheri, waongozi waaminifu.
>>> Safari ni
>>> ndefu kufikia huko, lakini penye nia pana njia – Inshallah tutafika –
>>> Amin.
>>> Kwa hivi sasa ni busara kuwa bwana wa zamani awepo asipigwe pute mkate
>>> wake
>>> na bwana wa leo nae asinyimwe fursa ya mkate – madhali Umma
>>> umewachaguwa.
>>> Ilivyo ni kwamba Serikali ya Umma haimtoi wa jana wala hamzuilii wa
>>> leo
>>> kuingia katika utawala. Sote tutakuwemo, kila mmoja atapata sehemu
>>> yake.
>>> (kila mmoja atabeba mzigo wake – mzigo wa dhamana za uwongozi –
>>> hesabu
>>> Kesho). Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atusaidie tuweze
>>> kujisaidia
>>> katika utekelezaji wa dhamana za uwongozi – Amin.
>>>
>>>
>>> KUTENGENEZWA KATIBA
>>> Kwa kujikinga na uwovu wa uwezo (power) ni muhimu ziwepo kanuni
>>> madhaubuti
>>> za kuwahifadhi na kuwahisabu mabwana wanaokuwa katika madaraka.
>>> Tusisahau
>>> kuwa sisi ni binadamu na binadamu ni mwingi na mwepesi wa kughurika
>>> na
>>> tusisahau kuwa: "power corrupts and obsulute power corrupts
>>> obsulutely".
>>> Kutokana na hali hii ni dharura tuwe na Katiba ambayo ina hifadhi haki
>>> za
>>> mwongozwa na haki za mwongozi. Katiba ambayo itabainisha na kuhifadhi
>>> "Haki
>>> na Wajibu" wa kila mmoja wetu kwa uadilifu kabisa. Katiba ambayo
>>> haitaruhusu
>>> yeyote yule kuwa juu ya kanuni, kanuni ndio itakayokuwa juu ya kila
>>> kitu.
>>> Katiba ambayo kwa haraka kabisa itazifuta zile Sharia Ovu Arubaini
>>> zilizo
>>> orodhishwa katika tume ya Jaji Nyalali na kuhakisha kuwa hazitaletwa
>>> tena
>>> katika kanuni za nchi kanuni kama hizo au za mfano wake.
>>>
>>> Kwa kumaliza, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ajaalie hii dhamiri na
>>> nia
>>> ya kuundwa "Serikali ya Umma" ithibiti na itekelezwe kwa salama na
>>> amani kwa
>>> manufaa ya vizazi vyetu na jamii ya binadamu – Amin, Amin.
>>>
>>>
>>> WA BILLAH TAWFIQ
>>>
>>> Umoja Wa Wazanzibari
>>> Disemba 09, 2000
>>>
>>> --
>>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>>
>>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>>> ukishatuma
>>>
>>> Disclaimer:
>>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and
>>> facts
>>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that
>>> you
>>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and
>>> Guidelines.
>>>
>>>
>>>
>>
>>
>> --
>> Lufingo Sadiki
>>
>> Dodoma.
>> The United Republic of Tanzania.
>>
>>
>>
>>
>
>
> --
> Lufingo Sadiki
>
> Dodoma.
> The United Republic of Tanzania.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment