Wednesday 17 October 2012

[wanabidii] Utata Wa Kifo cha Mwalimu Nyerere - Mwanzo

Madaraka Nyerere azungumza

Madaraka Nyerere, mmoja wa watoto wanane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, amezungumza na kusema ingawa haafiki kuanza uchunguzi wa kifo cha babake, lakini kuna viashiria fulani fulani vinavyotia shaka.

Viashiria hivyo, kwa mujibu wa Madaraka, ni namna alivyoanza kuikosoa Serikali kwa mambo mengi, jambo analosema inawezekana halikuwafurahisha wengi.

Katika mahojiano yake na JAMHURI wakati huu wa maadhimisho ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa, Madaraka ambaye kwa kawaida ni mpole, ameeleza yafuatayo:

"Binadamu wengi wanapenda sana kuamini kuwa kila jambo likitokea, basi kuna mkono wa mtu. Na hivi karibuni kifo cha Mwalimu Nyerere kimehusishwa na njama mahususi za kumuua. Kwa desturi za Kizanaki, hakuna mtu anayekufa kwa sababu ya ugonjwa au uzee, lazima yuko mtu miongoni mwa wale waliobaki hai ambao wamesababisha kifo chake kwa njia za uchawi. Kwa mfano, Bibi Christina Mugaya wa Nyang'ombe, mama mzazi wa Mwalimu Nyerere, mara baada ya kifo cha mume wake, Mtemi Nyerere Burito, tarehe 30 Machi 1942, alitimuliwa Butiama na kuhamia kwa ndugu zake katika kijiji jirani cha Muryaza, baada ya kutuhumiwa kuwa alisababisha kifo cha mume wake.


http://wotepamoja.com/archives/9015#.UH7HC1tTnZE.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment