Wednesday 17 October 2012

Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?

Mkuu samahani huu ujumbe uliniponyoka.

Hapana kule ubayani nilisharudi niko kijijini miaka saba saba kwa hiyo kidogo nimekuwa mzoefu wa maswala ya hapa, ila tuu labda kwa vile sisi bado ni washamba tu. 

Daktari nakusikia ila usijali sana upinzani wanasema nini kama sio la kweli au hayawafai Watanzania. Jali zaidi yale ya ukweli wanayosema. Na haswa yale maovu yanayosemwa vile vile na WanaCCM wengine. Kwa mfano, CHADEMA walitaja orodha ya mafisadi wakuu wala rushwa na watumiaji wabaya wa madaraka ambao wote ni wana CCM. Wote walisema wangekwenda mahakamani. Miaka kadhaa imepita hakuna cha mahakama hakuna cha kwa kadhi. Hao watu una shida gani kujitenga nao na kuwasuta hadharani. (By the way nilisikia Makongoro alitaja magamba yote makuu kwenye mkutano wa Halmashauri kuu, na jana kadondoshwa kwa msaada wa yale yale Magamba. Nape Nnauye dawa yake ipo jikoni).

Mpinzani anayeiombea kifo mara moja CCM hajatafakari madhara yake. Ningependa chama chochote tawala kiwe na upinzani unaoweza kuchukua madaraka (credible alternative). CCM wangekuwa ni wapinzani wazuri kwani wanajua mianya yote ya wizi, ubadhirifu na mbinu zote za matumizi mabaya ya mamlaka. Besides, wako wanaCCM wengi tu ambao hawakuoza na wenye kulitakia taifa hili mema. I should know - I am one of the founding members.

Ndugu Kafumu unasikia wagombea wa CCM wenyewe wakisema uchaguzi wa Chama unaoendelea nchi nzima ni MNADA. Au una shaka lolote kuwa kuna nafasi inayogombewa hadi sasa ambayo ilifanyika bila rushwa? Malalamiko yetu sisi wananchi makubwa ni ufisadi na matumizi mabaya ya raslimali za umma. Kama chaguzi zote za kuunda vyombo vya kukiongoza CCM kwa miaka 5 ijayo ZOTE zinafanywa kwa misingi ya rushwa, kwa nini sisi tuamini kuwa CCM itapiga vita rushwa kitaifa? NEC iliyochaguliwa kwa kuhonga wajumbe ni jopo la watoa rushwa, imeasisiwa kifisadi wazi wazi na itasimamia mfumo na serikali ya kifisadi. Wewe una shaka lolote kuhusu ni nani watachaguliwa kwa ngazi za juu za Chama pamoja na mgombea wake wa 2015 (kati ya wale waadilifu na wale mafisadi wenye fedha za kununua kura)? Hata kama jina hujui, ni kwamba jopo la waizi litasimika kinara wa wizi kuongoza uporaji wa pato la taifa kwa manufaa binafsi na ya kundi lililomweka madarakani.

Hapa utasema nimekwenda mbali mno bila ushahidi. Mie nitakuuliza kama unaamini kweli kuwa rushwa inayotolewa wazi wazi na imezungumzwa na wagombea na wajumbe wenyewe ingeweza kutolewa bila ya mtoa rushwa hata mmoja kukamatwa na TAKUKURU au polisi? Tukiona hivyo tunajua kuwa kazi ya vyombo hivi sio kushughulikia ufisadi wa kimfumo ila hakimu mmoja mmoja wa mahakama ya chini na bwana ardhi aliyekula mwenyewe huko wilayani. Ili taasisi hizi zishindwe kukamata hata mtu mmoja tocken, basi inakuwa wazi hii ni amri toka juu yao, au moja kwa moja au kwa kuelewa matakwa ya mkubwa wako wa kazi. Kwa mantiki hii ni vigumu kuamini kuwa CCM na uongozi ulioko na unaosukwa sasa hivi una nia ya dhati ya kutokomeza ufisadi. Kama unadhani ufisadi ulishamiri chini ya Mtandao1.0 fikiria ni wapi Mtandao2.0 utapeleka hii nchi.

Labda utasema nchi inaweza kuendelea ikiwa na kiwango fulani cha ufisadi. Mimi nakuhakikishia kwa hapa tulipofika, bila kuupiga vita ya kiukweli na kuupunguza sana sana Tanzania haiwezi kusonga mbele. Ukisoma takwimu zake zinatisha. Pesa zaidi ya dola billioni 12 ziko kwenye taasisi za fedha za nje, haswa magharibi. Na hii ni kabla ya ugunduzi wa gesi asilia na mafuta na Uranium nk. Hakuna nchi iliyo nyuma kama hii inayoweza kuendela kwa wizi wa kiwango hiki, na zaidi ya yote bila itikadi. Its no wonder religion is quickly filling the ideological vacuum.

Kwa hili daktari kama unaipenda hii nchi wale watu kama wewe ni lazma muwe tayari kuchukiwa na kuteseka kwa kusema ukweli unaoujua hadharani. Kuusemea ndani ya CCM inawezekana lakini huko ndio kwenye jopo. Unamkumbuka Kolimba? Je Mwaikambo? Huko mmezidiwa kete na huna blanketi la kukulinda kama Mwenyekiti hajaamua kwa matendo kuwa upande wa wapiganaji vita dhidi ya rushwa na ufisadi.  Angalau ukiwa nje ya chama uko na wengi wanaowasemea ubaya wao na kwa kiwango fulani utalindwa na taasisi hizo pamoja na wananchi wanaopenda mabadiliko. Na hata kama haikuwezekana, historia itakuenzi kwa kuwa mgombea ukombozi wa taifa lako mithili ya kina Mkwawa, Sykes, Jafet Murilo na Mwalimu Nyerere. And I am not saying this lightly.

Uzuri na ubaya wa kiongozi kama wewe, unajua mengi kwa vile tu ulikuwa huko karibu na jiko haswa hili jiko la nishati na madini. Mara nyingine nakusikitikia kwani the stakes are too high and you have more than your life to think about! The best I can do is to pray for you and hope that this way or the other when God wants to use you to lead his people out of Misri, you will be ready and at the right place. Do not wait until it is comfortable.

Daktari samahani kwa kiswahili murefu. I got to run.

mchilyi7.0

Willy Makundi
wrlmakundi@aol.com

-----Original Message-----
From: Peter <kafumu@yahoo.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tue, Oct 16, 2012 9:59 am
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?

Makundi

Asannte kwa ujumbe wako, bado uko majuu? Kama ndivyo sisi tuliorudi nchi yetu kuhudumu, haya ndiyo tunakutana nayo, mambo ya matusi, masingizoo, chuki tukiongozwa na siasa za kimagharibi za vyama vingi. Lakini hatujakata tamaaa, bado tutafika tunakotarajia...

Unajua mkakati wa upinzani ni kututaka watu wote tutoke ccm na tukikataa wote twaitwa mafisadi.. Hiyo siyo sawa. Na wakati wote nimejaribu kueleza kuwa pamoja na kuonekana uwepo wa ufisadi unaptokana na kutumia madaraka vibaya, bado imani na visions za ccm ni zilezile za kuamini katika usawa wa binadamu, kupinga rushwa, na mengine mengi kama yalivyoelezwa kwenye imani ya ccm na hata azimiao la arusha. Kurekebisha uovu si lazima utoke waweza kubadilisha pale ulipo ili mradi uteseke kuishi katika ubaya huo kwa uadilifu ukilenga kuleta mabadiliko ya kweli.

Ufisadi upo kila sehemu cdm wamejaa mafisadi wenye mali na makasri ya ajabu. Wengi wamepata mali hizo kwa dhuluma na biashara haramu, katika nchi ambayo usimamizi wa biashaara ni hafifu. Hwa kwa macho ya upinzani wa kisiasa ni malaika ilimradi tu wapo nje ya ccm na utawala.

Huwa ninasikitika sina nikiona siasa za tanzania zinazoendeshwa na upnzani ni siasa za matusi na kusingiziana. Kila wakati na kila kijana wa cdm - angalia vijana wa JF wakielezea kuhusu kafumu utadhani wanamfahamu. Wanasema fisadi huyo aliingia mikataba mibovu ya madini. Huu ni uzushi mkubwa na uongo uliojaa ushabiki ulio tayari kuua. Mimi nimekuwa kamishna wa madini kuanzia oktoba 2006, wakati huo mikataba yote ya madini ilishaingiwa tena na waziri wala siyo kamishna kulingana na sheria ya madini ya mwaka 1998, iliyotungwa na bunge la vyama vingi. Nilikuwa kamishna wa madini kusimamia sheria hiyo, wala siyo kuingia mikataba. 

Katika kipindi cha miaka mitano ya kuhudumu nafasi hiyo nilishiriki kuishauri serikali kurekebisha sheria hiyo na serikaliilitunga sheria ya madini ya mwaka 2010, yenye masharti na maelekezo ya kuitaka jamii ya watanzania kushiri zaidi katika sekta ya madini qqna hususan tasnia ya uchimbaji wa madini.

Mzee Makundi, tulipokuwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa igunga vijana wa cdm wakiongozwa na kijana mnyika walipita kila kona ya nyumbani kwetu kwa ndugu zangu wakisema huyu mtoto wenu amekuwa kamishna wa madini kwa miaka 18 ametunga sheria mbaya ya madini na ameingia mikataba mibovu. Nayasema haya kukuoanesha kuwa siasa zetu ni za propaganda mbaya iliyojaa uongo wenye nia ya kuamsha hasira ya wananchi. Hii siyo sawa.

Nionavyo mimi tunahitaji kuajifunza kushiriki kwenye siasa hizi kwa ukweli na uwazi, aliyekosa, au aliye fisadi asongwe, asontwe ili aadhibiwe na jamii, lakini siyo kila aliyeccm ni fisadi hata raia wa kawaida kijijini.

Siala la kuwa na fedha uswiss hata mafisadi waliopao cdm wanazo fedha huko, kwa vile wao hawahusiani na utawala basi wao malaika hii siyo sawa. Willy, nashukuru kwa ushauri wako, wa kuwasonta na kuandama mafisadi pale nilipo, kwanza kabla hujafanya hivyo ani lazima kuishi maisha ya mateso maisha ya kuwa mwadilifu katikati ya uozo ili uwe taa na mfano wa wazi wa kushindana na maovu. 

Tumekubali kuteseka ndani ya ccm ili Mungu atutumie kuleta mabadiliko ya kweli yasiyo na uwezekano wa kumwaga damu. Tunaitwa mafisadi wakati hatuhusikin kama unavyosema, tunanuka na mafisadi, lakini tutashinda tu. Uasi wakati mwingine siyo jibu la kusahihisha mambo.. Goberchev alibaki ndani na akausanbaratisha ukomunisti wa urusi. 

Nawaomba vijana waache kutukana kila mtu.

Unisamehe kwa makala ndefu.

Mungu akubariki

DPK Ng'wizukulushilinde

On 12 Oct 2012, at 23:56, Willy Makundi <wrlmakundi@aol.com> wrote:

Daktari naomba kusema neno..

CCM kuna mafisadi na watumiaji madaraka vibaya, vile vile kuna watu wema. Wakubwa wa ufisadi wametajwa hadharani na upinzani na hata baadhi ya wanaCCM. Kumbuka NAPE na kampeni ya kujivua gamba. Tunachowaomba wale wema ni kuwataja na kujitenga na wale mafisadi hadharani. Muanze kupigana kuwaondoa kwenye nchama, na kama ikiwezekana kuwachukulia hatua za kisheria.

Vile vile tungeomba wanaCCM wanaowajua mafisadi wa upinzani wawataje hadharani, na tutegemee upinzani kuwafukuzia mbali. Kwa namna hii wale wema wa CCM na wa upinzani wanaweza kuaminiana na kuwa wapinzani wenye lengo la ustawi wa taifa.

Kwa sasa, alimradi waizi wa EPA, MEREMETA, Import Export Fund, IPTL, Richmond/Dowans, Radar, Ndege ya Rais, pesa za Swiss Banks, viongozi wenye mabilioni na makasri, nk wako huru na tena kwenye nafasi za uongozi wa CCM, wale wema wananuka pamoja na hao mafisadi. Unashangaa nini nyote mnaonekana muozo hata kama binafsi nakufahamu kwa unadhifu wako?

Daktari, huna choice ila ile ya kuwaaibisha hadharani na kusema yale maovu wanayofanya. Mwisho wa siku wale wema wa CCM na Upinzani watarithi hii nchi, au kwa zamu au kwa kujiunga. Lifikirie.

mchilyi7.0

-----Original Message-----
From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Fri, Oct 12, 2012 10:22 pm
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?

Selemani,
 
Nakubaliana nawe sana kuwa ccm kuna mafisadi wakubwa lakini siyo sote. Nasema tena cdm nako kuna mafisadi wengi tu, waliojilimbikizia mali na watanzania wengi wakilala na njaa, wanaendesaha magari mahammer kutoka marekani lakini hawa ni malaika. siyo kweli. Lakini pia cdm wapo waadilifu wa kweli. Naomba nawe uwe objective usimchukie lila aliye ccm, ni kujenga chuki.
 
Nw'izukulushilinde

--- On Fri, 10/12/12, Leonard E. Mboera <lmboera@nimr.or.tz> wrote:

From: Leonard E. Mboera <lmboera@nimr.or.tz>
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
To: wanabidii@googlegroups.com, "Selemani Rehani" <srehani@hotmail.com>
Date: Friday, October 12, 2012, 9:47 AM

Tukumbushane tu kuwa: Na hata siasa za Chama Kimoja si utamaduni wa Kiafrika. Swala si vyama vingapi, bali ni uzalendo na maadili ya kiongozi mkuu na viongozi wenzake wa nchi.
On Fri, 12 Oct 2012 08:22:31 +0000
Selemani Rehani <srehani@hotmail.com> wrote:
>
> Kafumu,
>
> Kama kawaida yako mtazamo HASI uliopindukia juu ya vyama vya upinzani na hasa Chadema. Inastajabisha sana na hasa kwa msomi kama wewe. Chuki haziwezi kuondoka kwa mitazamo kama yako; hasa unapoamua kuyaona ya upande mmoja tu, yaani yale yanayofanywa na Chadema. Yale maovu yanayofanywa na CCM unaamua kujenga upofu na kuamua kutoyaona. Vitendo hivyo vinafanywa hata na wanachama wa CCM pia, mbona hilo hulisemi!! mbona upo biased sana kiasi hicho? Jaribu kuwa fair na objective ndio tutaweza kutatua tatizo hilo.
>
> Dr. ni muhimu ukajiuliza kwa nini CCM inahusishwa na ufisadi kiasi hicho? kwa nini? jaribu kuwa objective na nina hakika utayapata majibu. Hivi unataka tuseme vipi? je tukisema TLP ndio mafisadi ni sawa? au CUF? au Chadema? ni sawa? je kesi zilizopo mahakamani za kutumia madaraka vibaya au za ufisadi zinawakabili wanachama na viongozi wa chama gani? Jamani huu upofu ni wa kustajabisha sana. Inaoenekana ukiingia CCM hata ukiwa msomi namna gani, haijalishi, baada ya muda kidogo tu unajenga upofu na fikra kongwe za ajabu kabisa. Hivi kweli Dr unashindwa kuelewa kwa nini CCM inahusishwa na ufisadi? angalia kinachoendelea katika changuzi zake za ndani? hizo pesa za kuhongana na kutoleana bastola ni kwa ajili ya nini? wanazipata wapi? kama si ufisadi?
> Vyama vingine havina access ya raslimali za Taifa, vyama vingine havina uwezo wa kuamua kandarasi na kushughulika na kodi za wananchi, vyama vingine havina power wala mamlaka ya kuwatishia wafanya biashara ili wavichangie wala haviwezi kuwaahidi kuwa vitawapa kandarasi. Ufisadi upo CCM na hata viongozi mbalimbali ndani ya CCM wanaliona hilo na wanalisema, Waziri Mkuu mstaafu amelisema. Philip Mangula aliwahi kusema kuwa itafikia muda ili kupata viongozi ndani ya CCM itabidi watangaze zabuni na mwenye hela nyingi ndio atashinda na kuwa kiongozi. Ni Ufisadi mtupu. Inasikitisha umeshindwa kuona hilo. Ni juu yenu kuamua kubadilika au kuendelea na vitendo vya ufisadi na kukosa maadili.
>
> Selemani
>
>
>
>
> Date: Fri, 12 Oct 2012 00:58:42 -0700
> From: kafumu@yahoo.com
> Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
>
>
>
> Anael wa Nzega
>
> Pole, siasa za vyama vyingi siyo utamaduni wa mwafrika, ni jinamizi kutoka kwa wakoloni mamboleo, tunavyolikumbatia kiasi cha kuwagawanya watu wetu ni hatari kwa amani na ustawi wa nchi yetu.
> Huwa niashangaa ninapoona viongozi na vijana wenye imani kali ya cdm wanapomwita kila mwanaccm hata kama anaatoka kijiji cha Karitu (nzega) kuwa ni fisadi kwa vile ni mwanachama wa ccm ni kitu cha kutisha,
> Ninapoona mara nyingi mama wa ccm kavaa kitenge chake cha ccm anatukanwa na kupigwa mawe na vijana wa cdm ninashangaa. Hali hiyo inajenga uhasama miongoni mwa wananchi wa kawaida na uhasama huo utakapokolea na wananchi wakaanza kubaguana kwa kufuata vyama hatutapona.
> Wakati wote ninawaomba wenzangu ndani ya ccm na ndani ya cdm ninao marafiki, tujitahidi kuujenga mfumo huu bila chuki ili tuweze kubadilisha utawala wakati ukifika bila kumwaga damu. Chuki na matusi kwa sababu ya vyama havifai, vitalibomoa taifa letu...
>
> Anael ubarikiwe
> Nitakuletea kitabu nzega, Niarifu namba yako ya simu nitamtuma mtu akuletee
>
> Kitabu ni katika llugha ya kingereza na bei yake ni sh 15,000 tu
>
> Asante sana
>
> Ngw'izukulushilinde
>
> --- On Thu, 10/11/12, Anael Macha <kowiri@hotmail.com> wrote:
>
>
> From: Anael Macha <kowiri@hotmail.com>
> Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Thursday, October 11, 2012, 8:07 PM
>
>
>
>
> Dr. Kafumu,
>
>
> Nitakinunua kitabu, tafadhali kifikishe nzega.
>
>
> Unasema upinzani kuwa wanajenga chuki, sawa ila ccm unataka kujitenga nao. Wewe msafi ila wao walisema/walifanya. Ccm wanajenga nn? Kazi ipo, siasa zinawenyewe bana.
>
>
> Ok, nashukuru na ubarikiwe nawe pia
>
> AM
>
> On Oct 11, 2012, at 21:43, "Dr Peter D Kafumu" <kafumu@yahoo.com> wrote:
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> Bw. Nkumbaro.
>
> Nilishawahi kusema kwenye mabadiliko, cdm imejaa watu wema na pia mafisadi, kwa sababu hao ni binadamu wenye damu na nyama. Pia ccm imejaa wema na pia mafisadi kwani nao ni watu. Maandishi yako yanaonesha wewe sasa umegandamana na siasa za upinzani, zenye chuki na hasira iliyokithiri na ushabiki unaoona kuwa CDM malaika CCM mashetani.
> Katka uchaguzi mdogo wa Igunga mimi mgombea sikutoa rushwa yoyote, sikutukana mtu yoyote na sikukiuka kanuni zozote za uchaguzi. Hukumu imetolewa dhidi yangu kwa tuhuma siyo za rushwa bali za maneno ya watu wengine siyo mimi. Lakini pia kulikuwa na tuhuma zilizotolewa na washitaki kuhusu kutolewa kwa rushwa na baadhi ya wanccm (siyo mimi) lakini jaji alizikataa akasema hazina ushahidi.
>
> Kwa maoni ya jaji; maneno ya wengine yalitosha yeye kuhukumu alivyohukumu. Maneno yako yamejaa ushabiki na hasira dhidi ya ccm na wanaccm. Huo siyo utamaduni wa ushindani wa vyama vingi tunaotarajia kuujenga Tanzania, utamaduni wa kuita watu wote wa ccm au chama kisicho chako kuwa waovu na wazuri wote wako cdm.  Sipendi kulumbana nawe kwa sababu sitaki kujenga chuki dhidi ya mtu yoyote.
> Nakushukuru kwa mchango wako.
>
> Mungu akubariki
>
> Ngw'izukulushilinde
>
> --- On Thu, 10/11/12, John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com> wrote:
>
>
> From: John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com>
> Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Thursday, October 11, 2012, 2:21 PM
>
>
>
>
>
>
> Dear Kaka Kafumu,
> Kaka  HK anaandika kuwa, hakukuwa na tuhuma za rushwa kwako wala kiongozi yoyote wa CCM ama serikali aliyetuhumiwa na kukutwa na hatia ya kutoa rushwa kule Igunga.
> Definitely Kaka HK hajui nini rushwa. Kwake yeye labda ukikutwa unatoa pesa ndio unaweza kutuhumiwa na hatia ya rushwa. Rushwa, Kaka Kafumu, is any dishonest act committed in return for personal gain. Hata yule aliesema kuwa daraja halitomalizwa Igunga kama CCM haitoshinda – nae pia alitenda kitendo cha rushwa kwa upande wako.
> Mahkama Kuu imegundua kuwa dishonest acts (yaani rushwa) zilitumika na ndio maana ikapinduwa ushindi wako.
> Kaka HK nae anaeleza kuwa yumo katika kuandika kitabu chake pia. Hili ni jambo zuri sana na ninampongeza kama ninavyokupongeza wewe, kwani 'vizazi na vizazi vitapata kusoma na kujifunza',
> lakini sijui kitabu chake kitakuwa kuhusu nini – most probably his book will be titled - How fast a Cowboy draws his  gun on his enemy.
> Hapa netini, mimi nilikuwa katika watu wa mwanzo kukupa hongera baada ya ule ushindi wako na nilikuwa peke yangu nilie-withdraw hongera zangu baada ya kufahamu nini kilitokea Igunga na kuwa kumbe ulishinda kwa mazonge na rushwa. Ninastaajabu, vipi mtu anaandika kitabu kuhusu ubaya na extent ya rushwa nchini na huku anakuenda kugombania ubunge kupitia CCM na sio Chadema. Are we serious? The only CCM member ambae alikuwa free of rushwa kwa bahati mbaya amefariki tokea 1999. Sidhani kama yupo mwengine. Mwengine ambae tungelimdhania juzi aliadhirika Kisutu kuenda kudai kodi zake alizotapeliwa. Sisi tulimpa usukani ndugu yetu kumbe mwenzetu alikuwa busy kujenga nyumba za kukodisha katika kila corner ya DSM. Kama ni mimi nisingelikuenda Kisutu kujiadhirisha na ningelimuachia tu huyo mwizi hicho alichochukuwa – kama vile na yeye amechukua chake mapema kutoka kwangu!
>
>
> http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/mzee-sio-muachie-tu-raia-wako.html
>
>
>
> Anyway, najua mpo wengi hapa ukumbini (Tony, HK, etc) na kwahivyo bora nikimbie kwa haraka!
>
>
> //Nkumba.
>
>
>
>
>
>
>
> From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com Sent: Wednesday, October 10, 2012 3:55:48 PM
> Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
>
>
>
>
>
>
>
> Waungwana
>
> Nawaomba mnunue kitabu kwanza msome, na kufanya "a book review" na mjadili na kutoa maoni yenu. Kitabu ni cha kingereza mwandishi wa gazeti kajaribu kutafsiri - ni vizuri kusoma mwenyewe. Tuwasiliane mpate kitabu. Kinauzwa Shs 15,000 tu. Karibuni..
>
> Ng'wizukulushilinde
>
> --- On Wed, 10/10/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
>
>
> From: mngonge <mngonge@gmail.com>
> Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Wednesday, October 10, 2012, 5:05 PM
>
>
> Mimi siyo Kafumu na wala sijabahatika kusoma kitabu chake lakini kwa
> kuiangalia sehemu uliyonukuu "...kwamba kuishi kwa uaminifu katika
> jamii iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki
> aliyejeruhiwa baharini" unaweza kutoa tafakari.  Maneno hayo ni ya
> kiswahili yanayoweza kueleweka kwa wasomaji japo mwandishi anaweza
> kuwa na tafsiri zaidi.
>
> Kwa vile katuandikia wasomaji ili tusome kitabu chake na bila shaka
> kuelewa ujumbe anaokusudia tuupate. Binafsi namuelewa kwamba si rahisi
> kuuona uaminifu wa mtu au watu waaminifu wachache wanaoishi na jamii
> kubwa isiyokuwa na uaminifu (wala rushwa). Kwa kufafanua
> anachokimaanisha akafananisha mchango wa mtu mwaminifu na tone la damu
> ya samaki baharini.
> Kwa ufupi kama mada inahusu rushwa na tukiamua kujielekeza katika
> tukio lililompata mwandishi wa kitabu hicho tunaweza kupata maana
> zaidi. Yeye Kafumu amevuliwa ubunge kwa sababu ya ukiukwaji wa
> taratibu za uchaguzi yumkini ikiwemo rushwa.
>
> Maana pana zaidi tunayoweza kupata ni kama waziri mstaafu (Sumaye)
> alivyosema juma lililopita kwamba rushwa inanuka katika chaguzi za
> CCM. Inawezekana Kafumu alianza kudaiwa rushwa tangu kuteuliwa na
> chama chake hadi kwenye uchaguzi wenyewe. Hivyo anavyosema mtu
> mwaminifu hawezi kutokea kwenye kundi la wala rushwa maana
> hawatampitisha na hivyo hawezi kuonekana au kueleweka kwa namna
> yoyote.
>
> Lakini pia Kafumu anaweza kuwa na maana pana zaidi ya kwamba
> watanzania kwa ujumla wetu tulikofikia ni mwendo wa kutoa chochote ili
> uchaguliwe "Toa kula nikupe kura"
> Kwamba nchi imekuwa ya watu wasiokuwa waaminifu na hivyo mchango wa
> mtu mwaminifu hauwezi kuonekana kwa namna yoyote. Nafikiri Kafumu hana
> mpango wa kuomba radhi bali ameamua kuanika alichokiona ndani na nje
> ya CCM
>
> Naamini Kafumu mwenyewe atatueleza nini hasa alichokimaanisha ili
> tuweze kununua na kukisoma kitabu chake kwa uelewa zaidi
>
> 2012/10/10 Said Issa <saidissa100@yahoo.com>:
>> Hi All,
>> Nd. Peter Kafumu ameandika kitabu kuhusu rushwa nchini kinachoitwa "Sauti
>> Inayolia-Tafakuri Binafsi" (a Crying Voice-personal reflections).
>> Maelezo yake ya mbio mbio yananipa fikra kama huyu Mhe anatubia labda kwa
>> kushinda kule Igunga kwa kupitia mambo ya rushwa na sasa anaomba radhi.
>> Anyway, kila mtu atafahamu kivyake, lakini mimi ninamuona kama anaomba
>> radhi, hasa pale alipoandika kuwa...."...kwamba kuishi kwa uaminifu katika
>> jamii
>> iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki aliyejeruhiwa
>> baharini".
>>
>> Najua Mhe Kafumu yupo hapa ukumbini. Ningelimuomba atupe briefing ya kitabu
>> chake ambacho kidogo hakifahamiki - yaani haeleweki kama anai-expose
>> rushwa au anaomba radhi kwa rushwa iliyotendeka Igunga mpaka akashinda?
>>
>>
>> http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/peter-kafumu-alishinda-kutokana-na.html
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
> -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
0 comments:

Post a Comment