Tuesday 23 October 2012

[wanabidii] TAMKO LA IYDU KUPINGA UKANDAMIZWAJI WA CHADEMA, MAUAJI YA WAFUASI WAKE NA WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA - Mwanzo

Wakati Chama cha kisoshalisti CCM nchini Tanzania kikiwa kinapoteza mvuto , Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) ambacho vijana wake (BAVICHA) ni mwanachama wa Umoja wa Vijana wa Kidemokrasia Duniani (IYDU) kimeendelea kuwa nguvu  ya  kuhamasisha na kuwaunganisha  wananchi wa Tanzania katika ngazi za chini kupitia kampeni yake ya  Vugu Vugu la Mabadiliko (M4C)

Programu ya M4C ilizinduliwa na kuanza rasmi mwezi Mei 2012 na imekuwa tishio kwa Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake inayohaha kuendelea kuwa na mamlaka  ya kisiasa nchini Tanzania.

Katika jitihada za kuidhibiti programu ya M4C, serikali ya CCM imekuwa ikitumia jeshi la polisi, usalama wa taifa na vyombo vingine vya serikali kama ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuinyamazisha CHADEMA

Matukio ya utekaji nyara na mateso makali kwa wale wote wanajitokeza hadharani kuipinga serikali ya CCM na kuhamasisha watanzania wengine kudai haki zao za msingi yamekuwa yakiongezeka.

Mfano halisi wa utekaji nyara na utesaji ni ule wa Dkt Stephen Ulimboka  uliotokea mwezi Juni 2012 baada ya kuwaunganisha madaktari wenzake wa Tanzania kugoma kuishinikiza serikali kuboresha huduma ya afya Tanzania. Tukio la utekwaji wa Dkt Ulimboka lilifuatiwa na ufungiwaji wa gazeti la MWANAHALISI lililochapisha habari za kuhusisha utekwaji huo na idara ya usalama wa taifa ya Tanzania.


http://wotepamoja.com/archives/9585#.UIa-7nSI0QI.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment