Sunday 14 October 2012

[wanabidii] Taarifa ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Oktoba 13, 2012 - Mwanzo

VURUGU ZILIZOTOKEA MBAGALA

Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa na matukio yaliyotokea Mbagala, jijini Dar es Salaam, tarehe 11 Oktoba 2012. Chama cha Mapinduzi kinalaani kitendo cha kukojolewa kwa kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislam, yaani Kuran. Vilevile, Chama cha Mapinduzi kinalaani vitendo vya vurugu na kuvamiwa na kuchomwa moto makanisa.

Vitendo vyote hivi havifanani na mila na desturi za Watanzania. Kitendo cha kukojolea kitabu kitakatifu cha Waislamu hakikubaliki. Na kitendo cha kuvamia na kuchoma moto nyumba za ibada za Wakristo na kufanya vurugu pia hakikubaliki. Tanzania ni nchi inayofahamika na kusifika kwa amani na utulivu na kwa umoja na mshikamano wa watu wake wa kabila, rangi na dini zote. Chama cha Mapinduzi kinawasihi wananchi wawe na subira na uvumilivu yanapotokea matukio kama haya na waviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.


http://wotepamoja.com/archives/8723#.UHrstmgaNBA.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment