Wednesday 17 October 2012

[wanabidii] RE: ADHABU YA KIFO NI LAZIMA KATIKA SHERIA ZETU

Siamini kama maandiko hayo uliyoyanukuu yana maana ya moja kwa moja kama ulivyoweka.

Maandiko yanataka uunganishe maandiko ya sehemu nyingine ili upate ujembe uliokusudiwa. Amri ya Mungu inasema usiue na maandiko mengine yanasema usilipize kisasi. Kwa maneno mengine mkristo haruhusiwi kuua wala kushabikia mauaji.

Lakini hata kama si muumini wa Ukristo, fikiria kidogo. Suluhisho la kisheria si siku ni asilimia 100 sahihi, inategemea zaidi uwezo wako/mawakili wa kujieleza na ushahidi utakao tumika hata kama si wa kweli. Hapa mtu anaweza kuuawa hata kama hana hatia. Ukitazama kwa haraka makosa yaliyo wazi utasema wanyongwe lakini mwisho wa siku hawata nyongwa, badala yake wasio na pesa ndio watakao nyongwa. Jiulize ni wangapi wenye makosa makubwa japo wamefungwa tu?

-----Original message-----
From: Godfrey Ngupula
Sent: 17/10/2012, 13:52
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] RE: ADHABU YA KIFO NI LAZIMA KATIKA SHERIA ZETU


Mimi naitaka sana adhabu ya kifo,kwani ni moja ya njia nzuri ya kumtimizia Bwana nyapo zake. Imeandikwa,auaye kwa upanga atauawa kwa upanga.Yeye amwagaye damu isiyo hatia,naye damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu.Natamani maongezi haya yangelenga kuuliza jinsi ya kuweka sheria itayoweka time limit ya any ruling president to impliment adhabu ya kifo.I propose three month since hukumu mtu awe alisharamba adhabu yake. It is critically unfair,mtu aliyemwaga damu ya mtu mnyonge anapelekwa gerezani anakokaa na kulishwa kama mfalme kwa kodi ya wananchi. Kwa nini mtu huyo asigeuzwe mbolea ili nchi istawi? Ngupula...



________________________________
From: LENGAI OLDOINYO <lengai2000@yahoo.co.uk>
To: info@butmaninternational.com; sematangotours@cybernet.co.tz; serenacarhire@habari.co.tz; sgresort@yahoo.com; sss@habari.co.tz; tours@albatros.co.tz; mia@albatros.co.tz; info@chadema.or.tz; rassingida@pmoralg.go.tz; mhariri@habarileo.co.tz; advertising@dailynews.co.tz; jennie@albatros.co.tz; shidolya@yako.habari.co.tz; sssafaris@cybernet.co.tz; s-s.kolowa@web.de; worldtourstanzania@hotmail.com; wanabidii@googlegroups.com; unasemaje@radiofreeafricatz.com; mwananchipapers@mwananchi.co.tz; globalpublishers@dar.bol.co.tz; educate@intafrica.com; costech@costech.opc.org; info@satif.or.tz; info@satf.org; eotf@raha.com; eotf@cats-net.com; zitto@chadema.or.tz
Sent: Wednesday, 17 October 2012, 11:37
Subject: [wanabidii] RE: ADHABU YA KIFO NI LAZIMA KATIKA SHERIA ZETU


 
Mimi
ni Mtanzania wa kwanza kukubali adhabu ya kifo iwepo kwenye katiba ya nchi yetu
na itekelezeke kisheria japokuwa naogopa kufa. Hii inatokana na tabia ya watu
kuchukua sheria mikononi mwao. Itasaidia pia Polisi kuacha tabia za kuwaua raia
wasio na hatia hovyo. Polisi anatakiwa ampekele mshitakiwa kwa Hakimu lakini
hawafanyi hivyo wao wanachukua jukumu lisilo lao kutoa adhabu. Ikiwepo sheria
ya kuhukumu kifo kwa anayeua mwenzake watakoma kutumaliza na risasi.
 
Watanzania
wamekuwa na kiburi sana
hasa wanapoona kuwa hata wakichuna wenzao ngozi, au wakiua kwa makusudi bado
Rais atawatetea kwa kuwafutia adhabu hiyo.
Kwa
nini Rais asiwafutie adhabu ya Kifungo cha Maisha gwiji la Muziki wa dansi
Nguza (Papi Kocha) sijui na wanawe kama anayo huruma sana. Kesi yao haikuwekwa bayana na pia adhabu yao haikuwa wazi kulingana na kosa
walilolitenda. Hii ni kutokana na kesi yao
kufanyika kwa mda mfupi ukilinganisha na kesi zingine. Watu tuliitilia mashaka
Ikulu kuhusika na kesi hii. Sasa kama Rais anaona kuua ni dhambi kwa nini
asione kifungo cha maisha kuwa pia ni dhambi.
 
Katika
nchi zingine kama China
adhabu ya kifo ni jambo la kawaida. Ukikutwa na kosa lenye adhabu ya kifo
lazima utahukumiwa kifo. Nchi za Kiarabu wanazo adhabu za Kifo tukichukua mfano
mdogo tu. Mwanamke aliyezini anahukumiwa kupigwa mawe mpaka kufa kwani hiyo sio
adhabu. Nchi ikiwa na sheria kali na zinazotekelezeka watu wanakuwa waoga
kufanya makosa. Siku hizi Tajiri anachukua Bastola Serekalini na ukiingiza
mifugo kwenye shamba lake kwa bahati mbaya hangoji
Polisi akukamate upelekwe mahakamani bali anakuhukumu kwa kukupiga risasi na
Serekali haichukui hatua zozote sasa hii ni nchi au danguro. Watu wanajenga
nyumba za kuishi na kulaza wageni magirili kila mahali nchi nzima nyumba
zimekuwa kama magereza. Hii inaonyesha wazi
wazi kuwa Watanzania hatuaminiani. Nyumba za Biashara grili, nyumba za kulala
girili, nyumba za mahabusi girili, nyumba za wafungwa girili, Mochwari girili,
hii ni nchi au ahera kusikorudi watu.
 
Lazima
ifikie mahali sasa tuachane na Siasa zilizopitwa na wakati tuijenge Tanzania yenye
amani kwa kutunga sheria kali za kuwabana wahalifu wa aina zote na sheria
tukitunga ziwe zinatekelezeka. Ndugu zetu wa Kenya wananifurahisha jambo moja.
Wakitunga sheria ukavunja unawajibika. Walitunga sheria ya kutokojoa hovyo
inatekelezeka, walitunga sheria ya kutokuvuta sigara hadharani ni kweli
usijaribu, wakatunga sheria ya kutoongea na simu ukiendesha gari inafanya kazi
barabara. Sasa wametunga sheria hakuna kuuza Simu bandia Simu zote zimeletwa Tanzania na
wafanya biashara wakijua hiki ni kisiwa cha uhalifu. Pita madukani utakuta
wafanya biashara wa Kenya
wameleta Simu kuziuza kwa wafanyabiashara wahalifu wa Tanzania. Hivi
viongozi wetu kwa nini mko kama masanamu
Serekalini. Kwa nini mnaifanya Tanzania
iliyokuwa na heshima enzi za Mwalimu kuwa kichaka cha uhalifu. Tunataka
mabadiliko ya haraka sana Tanzania.
Mkereketwa
Lengai Ole Letipipi
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment