Sunday 14 October 2012

[wanabidii] Rais wa Mauritania apigwa risasi-BBC Source

Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, anapelekwa Ufaransa kwa
matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa alipopigwa risasi.

Kabla ya kuondoka kuelekea Paris, Rais Abdel Aziz alisema kwenye
hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni kutoka hospitali, kwamba
ameshafanyiwa upasuaji ambao ulifanikiwa.
Wakuu walisema rais alijeruhiwa wakati wanajeshi wa serikali waliokuwa
kwenye doria, walipofyatulia risasi msafara wa rais.
Inaarifiwa kuwa maafisa wawili wa jeshi wamekamatwa.
Jenerali Abdel Aziz, ambaye anaonekana na mataifa ya magharibi kuwa
anasimama dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika eneo hilo,
alichaguliwa mwaka wa 2009, mwaka mmoja baada ya kupindua serikali.

Source:
http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2012/10/121014_mauritania_president.shtml
--
Ipyana Lwinga

Email: ipyanalwinga@gmail.com
Mob: +255 757 065577
Skype: ipyana.plwinga

"Mpende Jirani yako kama nafsi yako..."

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment