Wednesday 24 October 2012

[wanabidii] HATUMUOGOPI MTU - SMZ!!!

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitamuonea haya wala kumuogopa mtu yeyote ambae atabainika kuhusika na uvunjifu wa amani baada ya Serikali kuvumilia vya kutosha, uvumilivu ambao umefikia kikomo.
Kauli hiyo imetolea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiufunga mkutano wa Tisa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema pia...."si vyema kwa baadhi ya vikundi vya Wananchi kuendelea kutoa matamshi yanayochochea chuki, uhasama na vurugu kwa kisingizio cha kuukataa Muungano". 


0 comments:

Post a Comment