Saturday 27 October 2012

[wanabidii] CHADEMA: Arusha – Wajeruhiwa katika kampeni; Yaunda tume kuchunguza ufisadi, migogoro; Shinyanga – Wanne mbaroni kwa tuhuma za kumchoma mkuki Mwenyekiti - Mwanzo

Wanne mbaroni tuhuma za kumjeruhi Mwenyekiti kwa mkuki

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewatia mbaroni watu wanne wanaodaiwa kumjeruhi kwa kumchoma mkuki  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la Mwawazo katika Manispaa ya Shinyanga, Bundara Katunge (39).

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Evarist Mangala, aliiambia NIPASHE jana kuwa watu hao wamekamatwa juzi baada ya polisi kufanya msako siku hiyo.

Alisema msako unafuatia kutokea kwa tukio hilo, ambalo linahusishwa na mitafaruku ya kisiasa.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Bundara Masanja (27), Benjamini Kanena (17), Maghembe Makonda (22) na Martin Mashimbi (27), ambao wote ni wakazi wa Kata ya Mwawazo, manisapaa hiyo.

Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani Jumatatu ijayo na kwamba, msako wa kuwapata watuhumiwa wengine unaendelea.

Kamanda Mangala alisema katika uchunguzi wa awali, wamebaini kuwa kuchomwa mkuki kwa mwenyekiti huyo wa Chadema kuna uhusiano na masuala ya kisiasa, ambapo katika kata hiyo kunafanyika uchaguzi mdogo wa udiwani.

Awali, taarifa, ambazo NIPASHE ilizipata kutoka eneo la tukio, zilieleza kuwa mwenyekiti huyo alichomwa mkuki na watu anaowafahamu, ambao walimvamia nyumbani kwake majira ya usiku.

Chanzo cha habari kutoka eneo hilo kinaeleza kuwa siku ya tukio, mwenyekiti huyo wa CHADEMA alisikia kishindo cha kuvunjwa mlingoti wa bendera uliopo nje ya nyumba yake majira ya saa 5:00 usiku.

Baada ya kusikia hali hiyo, alitoka nje na ghafla alivamiwa na kundi la watu, ambao walianza kumshambulia na katika kujihami, alikimbilia ndani, lakini kabla hajaingia, ulirushwamkuki, ambao ulimchoma tumboni upande wa kushoto karibu na mbavu.

Taarifa zinaeleza kuwa Bundara baada ya kujeruhiwa, alianza kupiga kelele kuomba msaada na kabla wasamaria wema hawajafika, alijitahidi kuchomoa mkuki na watu waliokwenda kumsaidia walimchukua na kumpeleka hospitali.

Mwenyekiti huyo amelazwa katika chumba maalum cha uangalizi wa wagonjwa (ICU) katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga .


http://wotepamoja.com/archives/9779#.UIwitslDbls.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment