Saturday 27 October 2012

Re: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja - Lipumba - Mwanzo

Ngupula usijekuta hao wake iunaodai mmoja wao akawa mama yako mzazi!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

-----Original Message-----
From: Godfrey Ngupula <ngupula@yahoo.co.uk>
Date: Sat, 27 Oct 2012 17:00:46
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: Re: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja - Lipumba - Mwanzo




Naafiki binadam wote kutendewa haki mbele ya vyombo vya dola. naafiki pia uhuru wa mahakama.Lakini siafiki hata kidogo serikali kuacha shughuli zake na kulipa umuhim wa kipekee suala la ponda.Mahakama iachwe ifanye shughuli zake kwa uhuru na raha zake.Although ponda look to be a hero to others,also is just like a devil to the country's peace and prosperity.So,hakuna umuhim wowote wa yeye kupewa kipaumbele.na wanaosema sijui amani ya nchi itatetereka,sentence kama hizo wakaongee na wake zao nyumbani.The country is much more safe in the absence of ponda.Ngupula


------------------------------
On Sat, Oct 27, 2012 6:28 PM EEST frank John wrote:

>Huyu Ponda amekuwa mdomoni mwa watu muda sasa akileta vurugu sio tu kwa chuki dhidi ya Ukristu bali pia hata ndani ya BAKWATA kiasi cha kuhoji uraia wake! Mimi binafsi sioni kama anastahiri chembe ya kupewa HAKI ingekuwa China jela maisha ama shaba tu asituharibie maisha yetu na mausiano yaliyopo! Hatutaki another Nigeria hapa! 
>Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom
>
>-----Original Message-----
>From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
>Date: Sat, 27 Oct 2012 15:23:01
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Subject: RE: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja - Lipumba - Mwanzo
>
>
>
>Mwalimu Lwaitama,
>Kwanza nikushukuru kwa kutetea haki. Nchi yetu haina haki na ni muhimu tujitetee. Pili, niseme tu kwamba ni hakika kuwa kati ya watu wanaomtetea Ponda ili apate haki ya dhamana, wewe ndiwe unazungumzia HAKI tofauti na wengine ambao shida yao ni siasa tu, ushabiki, hasira ama dini ya Ponda tu. Ndiyo, baadhi wanasumbuliwa na dini ya Ponda na si haki, kwa maana kwamba kama leo Ponda atatangaza huko huko lupango kwamba ameacha uislamu na watu hawa nao watabadili msimamo wao wa kumtetea. Wewe nina hakika unazungumzia HAKI. Safi kabisa!

>Kama sheria ndiyo inayostahili kufuatwa, basi ni kweli kwamba ukikamatwa ni lazima ufikishwe mahakamani katika muda wa masaa 24. Baada ya kutinga kizimbani hakimu atauuliza upande wa mashitaka iwapo una kipingamizi chochote dhidi ya haki yako ya dhamana. Swali hili linaulizwa iwapo tuhuma zako zinaangukia katika haki hiyo na kama kosa unalotuhumiwa nalo haliruhusu dhamana basi hakimu hatauliza ila atatoa maelezo kwa nini huna haki ya dhamama, na kimsingi hata wakili wako kama ana akili timami hatajisumbua. Upande wa mashitaka una haki ya kubishana na upande wa utetezi kuhusu dhamana na mwisho hakimu anatoa uamuzi.

>Kwenye suala la Ponda upande wa mashitaka ulikubali kwamba ameshitakiwa kwa makosa ambayo dhamana si mgogoro na wakili wake aliomba dhamana LAKINI polisi ikauomba upande wa mashitaka uweke pingamizi kwa kuwa upepelezi bado unaendelea na kwamba unaweza ukamjumuisha yeye na wenzake kwenye makosa ambayo hayana haki ya dhamana. Ndipo hakimu alipokubali na Ponda na wenzake wakarejea lupango na wakili wake akabakia ameduwaa.

>Kisheria, wakili wake anapaswa kupeleka shauri hili mahakama kuu kupinga hoja ya polisi na upande wa mashitaka. Kama hakufanya hivyo, basi tusiilamumu polisi wala ofisi ya mashitaka wala mahakama. Akina Lipumba wanacheza siasa tu na hawajali iwapo haki imetendeka ama la! Sisi tuangalie sheria inasemaje na inatoa haki gani. Hoja ya polisi ina mantiki au haina? Wakili wake amefanya linalostahili au bado?

>Asante,
>Matinyi.

>
>
>
>----------------
>From: kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Subject: RE: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja - Lipumba - Mwanzo
>Date: Sat, 27 Oct 2012 01:01:19 +0000
>
>
> Matinyi na Tony,
> Mniwie radhi maana ni wachangiaji ninaopenda kusoma  michango yenu humu. Naomba kwa unyenyekevu mkubwa mnielewe tafadhali ndugu zangu. Polisi waimizwe wakamilishe upelelezi na ibainike kama mtuhumiwa anatuhumiwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambao hauna dhamana au la. Mtu yoyote si vizuri  eti apelekwe rumande kwa  zaidi ya  saa 24, sasa ni zaidi ya siku kadhaa, wakati polisi eti wanatafuta  ushaidi wakumtuhumu  kwa kosa  lipi jamani. Leo nii Sheikh Ponda anafanyiwa hivi kesho inaweza ikawa Matinyi. Mimi  nilidhani  walau polisi wanampeleka mahakamani mtu  walio tayari na ushaidi wa kumtuhumu kosa fulani maalumu  si  eti wampeleke mahakamani halafu waseme hasipewe  dhamana vile bado wanachunguza kama  kosa wanalomtuhumi ni lenye dhamana au la. Vile mtu hupendi hoja anazotoa Sheikh Ponda  kwenye maswala ya mgogoro wa uongozi wa Waislamu hususani uongozi wa sasa wa Bakwata hisiwe sababu yakutojali kama ametendewa haki
 kama binadamu yeyote au la. Ilo tu jamani.
>  
> TANU ilituaasa kusema "nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko"!!! Labda kama tunakubaliana na serikali ya CCM kuwa matukio ya kuchoma makanisa Mbagala tayari tuanjua mchawi wetu na kuwa  ni matokeo ya uchochezi wa Waislamu wenye siasa kali hawa hawa ambao waliopo  sema  kwenye uchanguzi wa 2010 tumchangue mgombea  Muislamu aliyekuwa na nafasi kubwa ya kushinda  serikali hii   hii haikuona umuhimu wa kuwaita Waislamu  hawa hawa wakina Sheikh Ponda eti Waislamu wenye siasa kali?  Chonde chonde  wote tumuunge mkono Prof Lipumba ( hata kama inadhaniwa anazo sababu  zake nyingine za kisiasa zilizo nyuma  ya pazia!!!)  katika kushauri kuwa polisi wasimkamate mtu na kumpeka mahakamani bila  ushaidi wakutosha wa kosa analotuhumiwa nalo halafu waiambie mahakama eti  hasipewe dhamana vile hawajakamilisha uchunguzi kuhusu kosa gani wanamtuhumu na mahakama iridhie hoja hii ya ajabu kimantiki ya polisi . Matinki  yake hii  haieleweki
 ki haki za binadamu!! Leo ni Sheikh Ponda  je mtindo huu ukizoeleka kesho akakamatwa Matinyi tutaanzia wapi kuhoji kulikoni.
>  
> Tutulizane jamani, tuhoji hoja si kuangalia sura ya mtu  iwe kupenda au kutompenda  kwetu. Kama Sheikh Ponda anatuhumiwa kosa la  unyanganyi wa kutumia  nguvu  (kosa lisilo na  dhamana) basi polisi wa harakishe waiambie mahakama hivyo na wapenzi wa Sheikh Ponda nao wapate kujua kuwa ilo ndilo kosa anatuhumiwa mpendwa wao, basi! Sheria ichukue mkondo wake hiwe ni  pamoja na polisi kutompeleka mtu mahakamani halafu wakasema bado tunachunguza kama tutamtuhumu kosa lisilo na dhamana. Tusifanye mtindo huu wa kubinya haki za msingi za mtu uzoeleke jamani vile  tu bado  tumekasirika juu ya yaliyotokea Mbagala ya kuchomwa makanisa!!! Kama  ambavyo tunawasihi  ndugu  zetu Waislamu wasiendekeze hasira zao za haki  juu ya kudhihakiwa maandishi  matakatifu yao na kijana Mkrito  kuwasukuma kuchoma makanisa,  basi wote pia tuwashauri, kama  alivyoshauri Prof Lipumba, polisi  na mahakama  wamtendee haki Sheikh Ponda kwa kuwahimiza polisi
 wasizoee kumpeleka mtu mahakamani halfu waimbie mahakama  eti bado wanachunguza wamshitaki kwa tuhuma  gani yule  wanayesema hasipewe dhamana.  Na mahakama zisikubali kutumiwa na polisi kwa njia hizi zisizo na haki.  Narudia : 'Sheria ichukue mkondo wake iwe ni  pamoja na polisi kutompeleka mtu mahakamani halafu wakasema bado tunachunguza kama tutamtuhumu kosa lisilo na dhamana'.  Hapana, hii siyo haki  hata kama tunamchukia Sheikh Ponda kwa mambo mengine yawayo!!!
> Mwl. Lwaitama
>
>
>
>----------------
> To: wanabidii@googlegroups.com
>From: matinyi@hotmail.com
>Subject: Re: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja - Lipumba - Mwanzo
>Date: Fri, 26 Oct 2012 15:17:30 -0400
>
>Kamanda Suleiman alishaeleza vizuri, kwamba dhamana haikutolewa kwa kuwa polisi bado inachunguza, hivyo yeyote kati ya wote waliomo ndani anaweza kuingizwa kwenye makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambao hauna dhamana. Mchocheaji na mnyang'anyi wote ni kundi moja tu. Tunachotakiwa kufanya sisi ni kusubiri polisi ikamilishe upelelezi. Zaidi ya hapo basi ama hatujui tusemalo au ni ushabiki, siasa au hata udini.
>Matinyi.
>
>
>
>
>T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
>
>----- Reply message -----
>From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Subject: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja - Lipumba - Mwanzo
>Date: Fri, Oct 26, 2012 2:03 pm
>
>
>Azaveli,
>
>Hivi sisi hapa tunaweza kushawishi mahakama akapata dhamana hata kama hoja zetu ni sahihi? Ninachokiona ni kwa Prof lipumba kutaka ku-influence mahakama kufanya maamuzi ya kukidhi matakwa yake ya kisiasa. Anaingilia uhuru wa mahakama. Polisi hawana say baada ya kufikisha kesi mahakamani; ni DPP na Mahakama ndio alfa na omega kwenye hili!
>Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
>Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
>
>-----Original Message-----
>From: Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com>
>Sender: wanabidii@googlegroups.com
>Date: Fri, 26 Oct 2012 17:57:52
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
>Subject: RE: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja - Lipumba - Mwanzo
>
>
>
>Ndugu zangu wote,
>Polisi wenyewe walisema kuwa She

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com <http://www.mwanabidii.com>
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com <http://www.kazibongo.blogspot.com>
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com <http://www.patahabari.blogspot.com>

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment