Saturday 6 October 2012

Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Paul,
Niko kwenye furaha ya mwisho wa wiki na familia yangu. Nitarejea baadaye. Narudia tena, kama Kenya inahusika na Kiswahili kwa nini ilibidi Kenyatta asaini amri ya kidikteta mwaka 1973 kulazimisha kitambulike? Kwa nini kinawashinda nyie hadi hotuba rasmi za taifa zinakuwa kwa Kiingereza? Siyo kioja hiki?
Matinyi.





T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network

----- Reply message -----
From: "Paul Liyai" <pauliyai@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
Date: Sat, Oct 6, 2012 3:21 pm




Ndugu Matinyi,
Mbona huonyeshi mapungufu yangu katika Kiswahili? Jambo ninalolikataa katakata na sitalikubali asilani ni kuwa eti Watanzania ni mabingwa wa Kiswahili.. Hilo nakataa abadan Katan. Nenda juu chini ikiwa utalizua tena nitapinga nakupinga hadi utakaponyamaza. Lengo langu kuu nikukuonyehsa kuwa Kiswahili ni cha Afrika ya kati.
Paul


>________________________________
> From: "kimdr53@gmail.com" <kimdr53@gmail.com>
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Sent: Saturday, October 6, 2012 6:35 PM
>Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
>
>Kweli Maurice nimeteleza neno sahihi ni MJADALA na si MJADARA. Pia na wewe nikusahihishe katika thread ya Lake Malawi saga, neno ni SUALA na si SWALA!
>Idriss Mussa
>Sent from my BlackBerry® smartphone from Orange Botswana
>
>-----Original Message-----
>From: Maurice Oduor <mauricejoduor@gmail.com>
>Sender: wanabidii@googlegroups.com
>Date: Sat, 6 Oct 2012 03:46:18
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
>Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
>
>Kim,
>
>Eti Mjadara? Ama ulimaanisha Mjadala?
>
>Hapo ndugu si nawe umeteleza tunavyoteleza sote mara kwa mara?
>
>Courage
>
>
>
>On 10/6/12, kimdr53@gmail.com <kimdr53@gmail.com> wrote:
>>  Paulo
>>   Nadhani tumekuelewa sana, na inavyoelekea hatutakubaliana hapa. Hata
>> Kiswahili chako unachokiandika kinaonyesha dhahiri mapungufu uliyonayo
>> katika kukitumia Kiswahili. Kwa heshima na taadhima nakushauri mjadara
>> ufungwe!
>>
>>    Idriss Mussa
>> Sent from my BlackBerry® smartphone from Orange Botswana
>>
>> -----Original Message-----
>> From: Paul Liyai <pauliyai@yahoo.com>
>> Sender: wanabidii@googlegroups.com
>> Date: Fri, 5 Oct 2012 21:33:32
>> To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
>> Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
>> Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
>>
>> Ndugu Matinyi,
>> Nimekuelewa. Sasa bwan Matinyi, kosa hili la Mkenya mmoja au wawili linaleta
>> hoja ya Kusema kuwa Watanzania ni mabingwa wa Kiswahili? Je kosa hili ni
>> ushahidi kuwa Wakenya wote wanamakosa haya? Hakuna nchi yoyote ile inayoweza
>> kusema kuwa wao ni mabingwa wa Kiswahili kwani Kiswahili ni Lugha yetu sisi
>> watu wa Afrika Mashariki na Dunia nzima.
>>
>> Tanzania kuna Jamii nyingi mno, Wamasai, Wazaramo, Wanyakyusa, Wangoni,
>> Wasukuma, Wachaga na wengine wengi ambao hata wao wanakitumia Kiswahili kama
>> lugha ya Pili. Huwezi kupinga jambo hili. Nilikwambia kuwa nilikuwa na
>> Mwalimu aliyenifundisha Fasihi ya Kiswahili kutoka Dar-Salaam ambaye kwa
>> kweli alikisema tu Kiswahili lakini Kufundisha hakuweza kwani alikuwa
>> ametimuliwa kutoka katika Shule nyingine kwa sababu ya kutoweza kufundisha.
>> Siwezi kuliandika jina lake hapa.
>>
>> Nimesoma na Watanzania wengi katika Chuo na wao pia walikuwa na shida nyingi
>> mno za kisarufi, mambo kama sarufi hawakuyazingatia hata kidogo.
>>
>> kakuku kadogo badala ya kuku mdogo au kikuku kidogo, tunaendaga badala ya
>> sisi huenda, tunakulaga badal ya sisi hula. Hata hivyo hii si kusema kuwa
>> watanzania wote huyafanya makosa haya. Wala sisemi kuwa watanzania si mahiri
>> katika kukitumia Kiswahili, la hasha- Kiswahili kimeendezwa na Watanzania
>> kuliko Wakenya. Kinatumiwa zaidi na Watanzania kuliko Wakenya. Utafiti na
>> kazi zote za Usomi wa Lugha ya Kiswahili ni za hali ya juu na katika kiwango
>> cha juu zaidi kuliko Kenya. LAKINI WATANZANIA SIO MABINGWA WA KISWAHILI.
>> Paulo
>>
>>
>>
>>
>>>________________________________
>>> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
>>>To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
>>>Sent: Saturday, October 6, 2012 1:42 AM
>>>Subject: RE: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
>>>
>>>
>>>
>>>Paul,
>>>
>>>Kwenye hoja yako ya kutohoa nahisi ulidhani tatizo langu na yule bibiye wa
>>> Kikenya ilikuwa kusema ama kujumuisha neno "wikiendi". Hapana, si hili, na
>>> mimi natambua kwamba siyo Waswahili tu waliotohoa neno hili bali hata
>>> Wafaransa husema hivi hivi na kuandika hivi hivi kama kwenye Kiingereza
>>> --- week-end. Purukushani ilikuwa kwenye msemo mzima-  "wikiendi bora."
>>> Haiwezekani huu msemo ukabeba maana ya wikiendi njema kwa kumaanisha have
>>> a nice week-end.
>>>
>>>Nadhani nimekujibu.
>>>
>>>Matinyi.
>>>
>>>
>>>
>>>________________________________
>>> Date: Fri, 5 Oct 2012 10:53:42 -0700
>>>From: pauliyai@yahoo.com
>>>Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
>>>To: wanabidii@googlegroups.com
>>>
>>>
>>>Bwana Masuki,
>>>Asante kwa mchango wako ingawaje mada yenyewe ni nzito kwako kidogo kwani
>>> hujui utomvu wenyewe uko wapi. Sababu ya mimi kuutolea mfano wa Krapf si
>>> kuonyesha kwamba ndiye mtu wa kwanza kuandika Kiswahili la hasha, hoja
>>> yangu ilikuwa kumwonyesha Mwenzangu Matinyi kuwa Kamusi ya kwanza
>>> iliyoandikwa na Krapf iliandikwa kwa msaada wa wakalimani Wakenya si
>>> Watanzania. Matinyi anapasuka kinywa kwa kusema kuwa Kiswahili kina asili
>>> yake Tanzania na hiyo si kweli. Kiswhaili chimbuko lake ni pwani ya Afrika
>>> Mashariki na nilimnukulia ramani rasmi inyoonyesha kuwa si Tanzania tuu..
>>>
>>>
>>>Matinyi alikuwa ameshaanza kuvunda kinya kwa kusema kuwa Kenya hakuna
>>> waandishi wa vitabu vya Kiswahili ndio sababu wanafunzi wakenya
>>> wanatahiniwa kwa tamthilia na Riwaya kutoka Tanzania. Watu kamaProf.
>>> Kyallo Wadi Wamitila
>>>
>>>Ireri Mbaabu, Abdala Mwasimba ni wakenya wala si Watanzania.  Matinyi
>>> katika waraka wake alitohoa neno pointi (  Unatakaje?
>>>Kila pointi niliyokuwekea hapo ina maana yake) Yeye akitohoa ni vyema
>>> Mkenya akitohoa kama yule Mhadhiri aliyemtakia mwenzie wikendi njema
>>> anakivuruga Kiswahili.
>>>
>>>Wacha nikuketishe chini nikuelemishe kidogo. Wewe ni kama Watanzania
>>> wengine wanofungua vinywa bila kufikiri kwanza. Sheng si Kiswahili
>>> kilichotoholewa kama ulivyodai, Sheng ni lugha inayochipuka na kunyauka
>>> majira na misimu inavyoendelea kubadilika. Sheng ni mchanganyiko wa lugha
>>> nyingi zikiwemo Kikikuyu,Kijaluo, kiingereza, Kiswahili, Kiarabu, kihindi,
>>> kiGujarati, na lugha nyingine nyingi. Mfano wa maneno ya Sheng ni kama
>>> Kusorora kutazama au kuona, Ashu-kumi, keja -nyumba n.k tazama video hii
>>> http://www.youtube.com/watch?v=YrquMdHlJn4
>>>Jambo la kutazama hapa ikiwa wewe ni mwana taaluma ya isimu ya lugha, Sheng
>>> ni kama 'slang' na sheng inayosemwa Nairobi, ni tofauti na ile inayosemwa
>>> Nakuru au miji mingine ya Kenya. Hata Nairobi pekeyake, kuna lugha nyingi
>>> za Sheng kulingana na wingi wa mitaa iliyoko Nairobi. Lugha hizi
>>> zinakiathiri Kiswahili lakini wanafunzi wengi wanaweza kuzitumia lugha
>>> zote mbili kwa umahiri na huwezi kupata wakichanganya katika mitihani yao.
>>> Wakati wangu ningeweza kusema sheng ya wakati huo na kuandika insha zangu
>>> za Kiswahili bila mwingiliano wowote. Sheng niliyokuwa nikisema si sheng
>>> iliyoko sasa na huwezi kuandika kamusi ya sheng.
>>>
>>>
>>>
>>>Tunalosema hapa kuwa Watanzania sio wenye Kiswahili wala wao si mabingwa wa
>>> Kiswahili. Jambo ninaloweza kuliona katika maandishi ya watu kama Matinyi
>>> nikwamba wanawaonea ghere Wakenya ambao wana shahada za juu katika
>>> Kiswahili na Kiswahili chao labda nikile kilichoathiriwa na lugha za
>>> kwanza. Kumbuka kwamba katika kutahiniwa kwa Kiswahili na hata kiingereza,
>>> watu hawatahiniwi kusikiliza na kuongea, hutahiniwa kuandika na kusoma.
>>> Utampata Mkenya anayesema mbora badala ya bora na akiandika ataandika
>>> tahajia sahihi.
>>>
>>>Paulo
>>>
>>>
>>>>________________________________
>>>> From: Kenneth Masuki <kennymasuki@gmail.com>
>>>>To: wanabidii@googlegroups.com
>>>>Sent: Friday, October 5, 2012 7:50 PM
>>>>Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
>>>>
>>>>
>>>>Sasa wewe Paul, ukisoma historia unaambiwa kuwa Rebman alikuwa mtu wa
>>>> kwanza kugundua Mlima Kilimanjaro na ukisoma hivyo unaamini hivyo? Kwani
>>>> kabla Rebman hajaja Kilimanjaro wenyeji hawakuuona huo Mlima? Basi
>>>> vilevile kwa hili Kama Krapf ndo alikuwa wa kwanza kuandika kamusi na
>>>> akawahusisha watu wa Rabai kumpa tasfiri haina maana kuwa Warabai ndiyo
>>>> walioanzisha kiswahili. Rudi kwanye makataba ukachimbe zaidi uje na hoja
>>>> yenye mashiko. Na vile vile wewe kujua maana ya utohozi haikufanyi wewe
>>>> kuwa bingwa wa kiswahili kwa sababu kiswahili cha kikenya ni cha kutohoa
>>>> zaidi lakini mbaya zaidi kwa kuharibu na kukipa jina la "Sheng"
>>>>
>>>>
>>>>
>>>>
>>>>
>>>>2012/10/5 Paul Liyai <pauliyai@yahoo.com>
>>>>
>>>>Bwana Matinyi,
>>>>>wajua utohozi nini? Je wewe unaujua msamiati wote wa Kiswhili? Kama kuna
>>>>> mtu hat mmoja anyeujua msamiati wa lugha yoyote ile hatungekuwa na maana
>>>>> ya kuziandika kamusi.
>>>>>
>>>>>
>>>>>
>>>>>
>>>>>
>>>>>
>>>>>>________________________________
>>>>>> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
>>>>>>To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
>>>>>>Sent: Friday, October 5, 2012 4:18 AM
>>>>>>
>>>>>>Subject: RE: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
>>>>>>
>>>>>>
>>>>>>
>>>>>>
>>>>>>Paul,
>>>>>>Sijaelewa unachokitaka.
>>>>>>Si ulijitetea kwamba hukufanya makosa ya kisarufi bali ni makosa ya
>>>>>> uandikaji tu? Sasa unataka nikwambieje?
>>>>>>Kama Wakenya wameandika vitabu vingi vya Kiingereza, sasa inaua vipi
>>>>>> hoja yangu, kimsingi hata hoja haifi hapa. Unatakaje?
>>>>>>Kila pointi niliyokuwekea hapo ina maana yake - kwa ufupi nilikuwa
>>>>>> nataka kukata ngebe zako. Juzi mwalimu mmoja wa Kiswahili Mtanzania
>>>>>> hapa Marekani amekutana na profesa wa Kiswahili Mkenya hajui maana ya
>>>>>> msamiati "magonjwa sugu." Mwalimu mwingine wa Kiswahili Mkenya mwenye
>>>>>> shahada ya uzamivu (PhD) nimemkuta anawafundisha Wamarekani kusema eti
>>>>>> "wikiendi bora" akimaanisha: "...have a nice weekend!". Hii ni nini?
>>>>>> Halafu unabisha kitu gani?
>>>>>>Angalia hapo chini umeweka Kiswahili cha Kikenya: "....majivuno isiyo
>>>>>> msingi."
>>>>>>Angalia pia herufi kubwa na ndogo zinavyogongana kwenye Kiswahili chako
>>>>>> - uthibitisho kwamba unakijua vizuri sana Kiswahili.
>>>>>>Galagabaho hivyo hivyo.
>>>>>>Matinyi.
>>>>>>
>>>>>>
>>>>>>________________________________
>>>>>> Date: Thu, 4 Oct 2012 14:07:44 -0700
>>>>>>From: pauliyai@yahoo.com
>>>>>>Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
>>>>>>To: wanabidii@googlegroups.com
>>>>>>
>>>>>>
>>>>>>Ndugu Matinyi,
>>>>>>Nakuonea huruma wewe. Pole sana. Nikweli wewe hufahamikiwi kwani
>>>>>> unatapatapa hapa napale. Nilikuuliza unionyeshe nivipi ninakivuruga
>>>>>> Kiswahili, umeruka umekwnda Kwa Nyerere, msumbiji sijui nini,....
>>>>>> Nilikwambia kwamba wakenya wameviandika vitabu vingi katika Kiingereza,
>>>>>> kuandika vitabu hakuwafanyi Wakenya kuwa mabingwa. Soma hii profile
>>>>>> ujionee mwenyewe
>>>>>> http://www.ku.ac.ke/schools/humanities/images/stories/docs/prof_mbaabu.pdf
>>>>>> Tena mtafute bewana huyu Meja Mwangi aliyeandika Vitabu kama the
>>>>>> Cocroach Dance, Carcase for hounds na vingine vingi. Hapa chini Orodha
>>>>>> ya Watanzania walioandika Vitabu mbali mbali. Je idadi yao ni sawa na
>>>>>> ya wakenya? Ujibu swali hili wacha kutapatapa na majivuna isiyo msingi.
>>>>>> Mimi Kiswahili ni lugha yangu ya Kwanza. Si KAMA UNAVYO FIKIRAI WEWE..
>>>>>>
>>>>>>Tanzania
>>>>>>    * Agoro Anduru (1948–1992), short story writer.[Killam & Rowe]
>>>>>>    * Mark Behr (1963– ), fiction writer also connected with South Africa.
>>>>>>    * Chachage Seithy Chachage ( –2006), sociologist and Swahili
>>>>>> novelist.[146]
>>>>>>    * Abdulrazak Gurnah (1948– ), novelist and critic.[Gikandi] [Killam &
>>>>>> Rowe]
>>>>>>    * Ebrahim N. Hussein (1943– ), playwright, essayist, poet and
>>>>>> translator.[Gikandi] [Gikandi & Mwangi] [Killam & Rowe]
>>>>>>    * Euphrase Kezilahabi (1944– ), novelist, poet and scholar.
>>>>>>    * Jacqueline Kibacha, poet.[147]
>>>>>>    * Aniceti Kitereza (1896–1981), novelist.
>>>>>>    * Amandina Lihamba (1944– ), playwright.[148]
>>>>>>    * Ismael R. Mbise, novelist and academic.[Gikandi]

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment