Fahamu kuwa upo ktk taifa la mchanganyiko sio kama kwa wengine. Jee, iwapo askari naye ni wa dini hiyo na anakubaliana na hayo wasemayo atakwenda mapema kukamata? Jee, kama walikwisha kuwahi kuua askari wakamkata kichwa na anayekwenda anakwenda kwa gari inayopita barabarani sio helikopta si ataogopa petroli, mawe na magogo atauawa na umma nao wapo wachache? Askari mmasai au mkurya atakwenda kukamata wa makabila hayo ambao ni wezi wa mifugo wanaoua watu? Ilibidi yale mauaji ya Serengeti-mkoa wa Mara na mapigano yaliyozagaa mpaka kufikia kuteka vituo vya polisi kuvivamia ili wenzao watolewe kufanyike kazi ya ziada. Mwaka 1993-1994 walipeleka askari Mugumu na maeneo mengine huko na hao askari walitolewa Zanzibar kwani jeshi la Tanganyika bara ni watu wa Mkoa wa Mara kama si 80% enzi hizo basi ni 50%. Na mkoloni alifanya hivi ili kupunguza mapigano, wizi wa mifuko na vurugu nyingine ambazo zilionekana kuathiri productivity na wamasai akatengeneza Maasai resrrve kutoka humo ni kwa kibali kuelekea kokote kule (soma Colonial District Books National archives). wapigane Wanyanjali na askali ni Mnyanchali kutakuwa na ufanisi? Hata akina Suleiman Kova au rais akikemea ataambiwa tayari amekwisha kubatizwa. Lawama zitakuwepo na ni hivyo wakimuwinda na kumtishia Kadhi kwa vile labda hakubaliani nao mambo fulani. Kama ni Mafuta na Gas-bara ni mengi Mtwara, Songosongo, Mafia labda na maeneo mengine. Kwa sasa Mtwara si ile tena ya zamani wamejaa sasa hivi karibuni itakuwa another capetown. Mafia wapo busy wafaransa baharini miaka wakichimba na mpaka meli ya uchimbaji ikavamia miaka ya karibuni na wasomali wakitaka kuiteka. Ujenzi wa bandari Mafia na ujenzi wa International Airport Mafia wanauona na kuusikia. Gas na mafuta yanachimbwa kabla hawajagundua yao, mbona sisi hatukufanya vurugu kusema hatuwataki kwa vile tumegundua hiki au kile? Viongozi wa dini na wanasiasa wahusike kuelimisha jamii sio kuangamiza na kuchochea-tujifunze kutoka kwa wenzetu tunaona ktk TV. Mbona hata huko ktk dini moja kubwa ya aina moja (Somalia, Syria, Afganistan, Misri, Libya, Mali etc) vikianza haviishi wenyewe kwa wenyewe hakuna usalama wanapigana tu. Hivi hapa petu suala ni dini ya Kiislamu kweli kuwa inaonewa na wakristo hili ni la ukweli kweli. Ugomvi kidogo kuchoma makanisa-yamekosa nini? Huko Mafia 2008 wavuvi tika ZNZ walipokuwa wanavua ndani ya Marine Park Mafia na jamaa zao wa kule na kutakiwa kuondoka wakaenda na petroli kama silaha ikawa vurugu ya ki-dini kumbe hoja ilikuwa kuvua ndani ya conservation area ya samaki. Serikali haikujibu mapigo yao ya mabomu ya petroli, iliweka patrol tu na askari ikiwatazama na mitutu mkononi. Huku kutazama tu kutatuponza. Mfano wakiingia shule mojawapo ya kanisa na kuchoma wanafunzi itakuwaje? Jee, wakristu wakiamua kulipiza kisasi-tutafika? Hebu kuwekwe kongamano zirushwe na radio na TV kuelimisha. God Bless us. . --- On Thu, 18/10/12, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
|
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment