Thursday 18 October 2012

Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA

Salum,
 
Mi nikuombe labda utusaidie kutupa au kutoa suluhisho ili maaskofu wetu waweze kujipanga vizuri.
 
William

From: salum mkango <salumkango@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, October 18, 2012 5:17 PM
Subject: RE: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
 
Baada ya kusoma hili tamko kwa makini nimegundua watanzania bado hatuna amani mioyoni mwetu. Na busara za viongozi wetu wa dini bado kabisa. Si wakiislamu wala Wakikristo. Misamaha ya kweli mioyoni mwetu haipo. Tunasamehe mdomoni lkn mioyoni mwetu tunavisasi vilivyojificha. Hatuangalii tulipojikwalia bali tunaangalia tulipoangukia. Hatutatui chanzo cha tatizo bali ni matokeo yake. Tunachanganya vyanzo vingi kwa matokeo ya chanzo kimoja cha tatizo. Mafundisho yetu ya dini yamejaa kasoro nyingi ikiwemo visasi na chuki badala ya busara na amani. Kwa mwenendo huu BADO SANA KUFIKA KWENYE SULUHU. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
SM.
--- On Thu, 10/18/12, Monica Malle <moninaike@hotmail.com> wrote:

From: Monica Malle <moninaike@hotmail.com>
Subject: RE: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
To: "Wanabidii googlegroup" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, October 18, 2012, 6:49 AM

Wewe ulitaka wawapongeze wachomaji haoooooo?
 
Date: Thu, 18 Oct 2012 16:34:36 +0300Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISAFrom: oldmoshi@gmail.comTo: wanabidii@googlegroups.comMaaskofu nao wanajiingiza kwenye siasa kutetea maslahi ya kanisa wakati uhalifu hauna dini wala rangi na uhalifu ni uhalifu tu na watuhumiwa wenyewe wako mahakamani kwahiyo wanataka kulazimisha nini ?
2012/10/18 Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM.

Wapendwa Katika Bwana,
Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla.

Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina.

Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu:
  1. Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33).
  2. Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini.
  3. Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya. Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini.
Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:
  1. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe.
  2. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini.
  3. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake.
Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga.

Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo:
  • Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa "mfumo Kristo", na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili.
  • Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa.
  • Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania
  • Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi.
  • Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama:

  1. Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi?
  2. Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini.
  3. Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini
  4. Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria.
  5. Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma,
  6. Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini
Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni "wana harakati", tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii.

Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema "sasa basi" pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo.

Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu?

Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.

Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine.

Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).

Daima tukumbuke kuwa, "KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO" (Waefeso 6: 12).

Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu,
  1. Askofu Dr. Alex G. Malasusa – Mkuu, KKKT na D/Mashariki na Pwani
  2. Askofu Dr. Stephen Munga –Mkuu, D/Kaskazini Mashariki
  3. Askofu Dr. Martin Shao – Mkuu, D/Kaskazini
  4. Askofu Dr. Thomas Laizer – Mkuu- D/Kaskazini Kati
  5. Askofu Dr. Benson Bagonza- Mkuu, D/Karagwe
  6. Askofu Isaya J. Mengele – Mkuu, D/Kusini
  7. Askofu Levis Sanga – Mkuu- D/Kusini Kati
  8. Askofu Elisa Buberwa – Mkuu –D/Kaskazini Magharibi
  9. Askofu Andrew Gulle – Mkuu, D/Mashariki ya Ziwa Victoria
  10. Askofu Michael Adam –Mkuu, D/Mkoani Mara
  11. Askofu Renard Mtenji – Mkuu, D/Ulanga-Kilombero
  12. Askofu Dr. Israel-Peter Mwakyolile – Mkuu, D/Konde
  13. Askofu Job Mbwilo – Mkuu, D/Kusini Magharibi
  14. Askofu Dr. Owdenburg Mdegella- Mkuu, D/Iringa
  15. Askofu Jacob Ole Mameo- Mkuu, D/Morogoro
  16. Askofu Zebedayo Daudi – Mkuu, D/Mbulu
  17. Askofu Paulo Akyoo – Mkuu, D/Meru
  18. Askofu Charles Mjema – Mkuu, D/Pare
  19. Askofu Mteule Amon Kinyunyu- Mkuu, D/Dodoma
  20. Askofu Mteule Dr. Alex Mkumbo- Mkuu, D/Kati
Bart

--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment