Wednesday 24 October 2012

Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA

On Monday, 22 October 2012 20:35:46 UTC+3, Godfrey Ngupula wrote:
> mtu akivuta bangi kisha akaenda kuharibu mali zake nyumbani,nga kuvuta bangi ni kosa,people wil not mind.Haya yanayofanywa na wanaojiita waislam ni lazima yakemewe na yathibitiwe leo na hata kesho.Napata picha sasa kwa nin sheria ya ugaidi inapigwa.Nafikiri ipo haja sara yamkini hata katiba itamke kuhusu ugaidi.Ngupula
>
>
>
>
>
>
>
> ------------------------------
>
> On Mon, Oct 22, 2012 8:18 PM EEST Mike Zunzu wrote:
>
>
>
> >Bado haileti sense kosa lifanywe na mtu mmoja adhabu iwe kwa kundi zima, vipi kuwe na collective punishment, Hapo kuna akili ya kawaida imetumika? Nakumbuka tulipokuwa all level kundi la vijana wa kidato cha pili walificha kibiriti cha mwalimu walipokuwa kwenye maabara ya kemia, mwalimu wa kirusi aliwaomba wee wale vijana warudishe hicho kiberiti hawakufanya hivyo, kwa vile walimu wa kigeni walikuwa hawaruhusiwi kutoa adhabu ilibidi akashitaki kwa second master, ambaye aliamua kila mmoja achapwe kiboko, kulikuwa na jamaa mmoja kati yao aliwaonea huruma sana wenzake ambao anafahamu hawakushiki kitendo hicho, hivyo alijitolea kuwa yeye ndiye kakichukua kile kiberiti, alipoulizwa kiko wapi akasema amekitupa na haumbuki ni wapi, basi akachapwa viboko, yakaisha, simsifu huyuo kijana aliyejitolea , ila adhabu za watu wote hutolewa iwapo hamfahamu aliyefanya kosa. 
>
> >Hata hivyo kuhusiana ya maisha yetu ya kila siku kundi moja haliwezi likajichukulia mamlaka ya kuadhibu kundi jingine, ni kuviachi vyombo vinavyohusika, kwa vile wanafahamu wakiwakilisha hoja kwamba kundi jingine liadhibiwe wataonekana ni wapuuzi, ndiyo maana wakaamua kujichukulia sheria mkononi, huo ni uvunjaji wa sheria, waliokamatwa wakifanya huo uharifu wanastahili kupewa adhabu.
>
> >Inashangaza kuona eti kuna watu wanaipa Serikali muda waharifu hao waachiwe, hiyo itakuwa ni nchi au mkusanyiko wa majangiri? Hatupo Mexico au Bolivia hapa, ambapo magenge ya wauza unga yanaweza yakakamata watu mateka na kutoa madai yao.
>
> >
>
> >
>
> >________________________________
>
> > From: mngonge <mngonge@gmail.com>
>
> >To: wanabidii@googlegroups.com
>
> >Sent: Monday, 22 October 2012, 17:27
>
> >Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
>
> >
>
> >
>
> >Naomba nikuulize swali ndugu Peter hivi si kawaida ukivaa nguo ikachafuka na ukafua? utajisikiaje mtu akipita akakupaka uchafu? Bila shaka utakasirika, japo uzito wa hasira unaweza kupunguzwa kama utagundua hakukupaka makusudi na aliyekupaka uchafu atakwambia maneno mazuri ya kukupoza kama vile samahani nk. Lakini pia itategemea kama tangu jana au asubuhi ni mabaya mangapi umekwishafanyiwa na yeye au mtu mwingine (marejeo katika ubongo wako). Kitu kinachoweza kukunyima busara ata ya kusikiliza samahani ya aliyekuchafua na badala yake ukaanza kumzaba makofi.
>
> >
>
> >Maswali yako naweza kuyajibu kwa mfano kama huo, kwamba kitabu kinapochakaa ni kawaida kukitupa, kukichoma au kukisahau store. Acha kuchakaa ukikiacha hovyo mtoto anaweza kukikojolea, kukinyea, kukichana au kukimwagia mchuzi kikaharibika na kutupwa. Kitabu kama kitabu hakiendi kwa Mungu kinachoenda kwa Mungu ni ujumbe uliomo. Tendo lolote linalohusu namna ya kukidispose kitabu halina tatizo tatizo ni association ambayo mtu anaamua kuijenga, mfano kama kuna visa utasikia ndiyo maana umefanya hivi au vile, wewe umeniona mtu wa chini na kunidharau ndo maana umefanya na hili nk.
>
> >
>
> >Pamoja na yote kama tukio la kuchafua nguo aliyelifanya ni mtoto si kawaida kwa mtu mzima mwenye busara zake aanze kurusha makofi kwa mtoto badala yake atasamehe kwa sababu si rahisi kuassociate hasira ya aina yoyote na mtoto. ukifanya hivyo lazima kuna tatizo katika busara zako.  Kuchana au kukojolea kitabu au karatasi zake si tatizo, tatizo ni nani amefanya hivyo na nani amefanyiwa hivyo, yuko katika hali gani na historia yenu ikoje, historia yaweza kuwa ya kweli au dhaniwa
>
> >
>
> >
>
> >2012/10/22 Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
>
> >
>
> >Wanabidii,
>
> >>
>
> >>Naomba mnielimishe.
>
> >>
>
> >>Najaribu kujiuliza kwamba si ni ukweli kuwa hivi vitabu vitakatifu tulivyonavyo majumbani kwetu huwa vinachakaa? Kama vinachakaa sasa ni nani kati yetu anazo nakara zote za vitabu hivi vilivyochakaa nyumbani kwake? Nadhani ni wachache wenye nakara hizo kama wapo. Sasa nakara za vitabu hivi zilizochakaa huwa tunaziweka wapi? Tunazitupa? Tunazichoma moto? Tunazikojolea? Tunazipeleka mbinguni? Ziko wapi hizi??!! Ukichunguza kwa makini utakuta kwamba nakala hizi zilizochakaa hatujui zilipo. Zimetupwa majalalani na kuoza, kuchomwa moto, kukojolewa na kadhalika. Kama huu ndiyo ukweli basi sote tunafahamu (bila kujifahamu) kwamba kilicho cha muhimu katika vitabu vitakatifu ni ujumbe na siyo makaratasi. Tusidanganyike.
>
> >>
>
> >>Lwega
>
> >>
>
> >>
>
> >>
>
> >>
>
> >>
>
> >>
>
> >>________________________________
>
> >> From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
>
> >>To: wanabidii@googlegroups.com
>
> >>Sent: Monday, October 22, 2012 12:41 PM
>
> >>Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
>
> >>
>
> >Wahuni wameziba masikio
>
> >>
>
> >>Hawataki kusikia hilo.
>
> >>Na wanadai wanalishughulikia.
>
> >>Nitalia kama kijana aliyekojolea kuruani ataadhibiwa peke yake. Sitakuwa namlilia aliyeadhibiwa. Nitakuwa nalililia taifa letu kukosa umakini wa kutafuta vyanzo vya matatizo yetu, badala yake kutibu dalili kama unavyosema.
>
> >>Panadol inatuliza maumivu haitibu Malaria. Ezekiel-Tufanye nini?
>
> >>
>
> >>--- On Sun, 10/21/12, ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> wrote:
>
> >>
>
> >>
>
> >>From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
>
> >>Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
>
> >>To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
>
> >>Date: Sunday, October 21, 2012, 11:55 PM
>
> >>
>
> >>
>
> >>ELISA MUHINGO
>
> >> 
>
> >>Nadhani na mimi nikubaliane na wewe kwamba atafutwe huyo kijana aliyemshawishi mwenzie kukojolea hicho kitabu kwa udanganyifu wa kugeuka kuwa mjusi. Huyu ndiye mtuhumiwa namba moja katika sakata hili kwa mtizamo wangu. Kuachwa huyu ni sawa na kutibu Malaria kwa kunywa PANADOL ambayo inapunguza joto tu lakini haitibu maradhi yenyewe.
>
> >> 
>
> >>Atafutwe yule kijana aeleze alikuwa na kusudi gani. Kama alitumwa atasema tu.
>
> >> 
>
> >>K.E.M.S.
>
> >>
>
> >>From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
>
> >>To: wanabidii@googlegroups.com
>
> >>Sent: Sunday, 21 October 2012, 13:35
>
> >>Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
>
> >>
>
> >>Erick.
>
> >>Tumeandika humu kuulizia hili lakini hakuna anayejibu. Si haki kumuacha huru yule kijana aliyemshawishi mwenzake akojolee kitabu hicho. Na Polisi wangelifanyia kazi wangegundua huyo kijana alikuwa katumwa. --- On Sat, 10/20/12, Erick Mathew <mathewerick@yahoo.com> wrote:
>
> >>
>
> >>>From: Erick Mathew <mathewerick@yahoo.com>
>
> >>>Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
>
> >>>To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
>
> >>>Cc: "eric.rushiho@gmail.com" <eric.rushiho@gmail.com>
>
> >>>Date: Saturday, October 20, 2012, 11:20 AM
>
> >>>
>
> >>>
>
> >>>Habari wapendwa na watanzania wenzangu.
>
> >>>Pamoja na yote mlio changia kwa kuitakia mema nchi yetu, mimi nataka mnijuze!  hivi yule mtoto aliyekua  na masahafu hiyo na kumpa kijana
>
> >>>mwenzie na kumwambia kojolea uone kama hutageuka nyoka nae amekamatwa? maana yeye ndiye chanzo cha kushawishi mwenzie akojolee!au siku hizi sheria siyo msumeno tena kama tunavyo jua?
>
> >>>
>
> >>>From: Amos Malongo <amos_772002@yahoo.com>
>
> >>>To: wanabidii@googlegroups.com
>
> >>>Sent: Saturday, October 20, 2012 1:46 PM
>
> >>>Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
>
> >>>
>
> >>>Wapendwa wanabidii,Kwa mara hii ya kwanza naandika humu ndani, huwa nafuatilia sana hoja na majadiliano mbalimbali. Nimeona niungane na Salamu za Maaskofu wa KKKT, lakini pia nikushukuruni William, Monica, Kunyaranyara kwa kumjibu ndugu Salumu. Nami naongezea nukuu kutoka kitabu kitakatifu Biblia hapo chini, labda itasaidia kujipima ustaarabu na kuelimika kwetu katika ku-address issues za msingi.
>
> >>>
>
> >>>Luke 18:9-14
>
> >>>New International Version (NIV)
>
> >>>The Parable of the Pharisee and the Tax Collector
>
> >>>9 To some who were confident of their own righteousness and looked down on everyone else, Jesus told this parable: 10 "Two men went up to the temple to pray, one a Pharisee and the other a tax collector. 11 The Pharisee stood by himself and prayed: 'God, I thank you that I am not like other people—robbers, evildoers, adulterers—or even like this tax collector. 12 I fast twice a week and give a tenth of all I get.'
>
> >>>13 "But the tax collectorstood at a distance. He would not even look up to heaven, but beat his breast and said, 'God, have mercy on me, a sinner.'14 "I tell you that this

Ndugu Salum upo uwezekano wa mtu kudhani kuwa anaelewa unachokisema kumbe haelewi! Anahitajika aingizwe darasani. Wewe unasema baada ya kusoma tamko la Maaskofu unegundua kuwa "hatuna amani miyoni mwetu." Je baada ya kusikia uchomwaji wa makanisa uligundua nini? Tena unasema busara za viongozi wa dini bado, si watoa tamko wala wakiislamu.Je umepimaje busara ya viongozi wa kiislamu katika tamko la Maaskofu? Je unafahamu maana ya msamaha? Au unasema tu kwa sababu unataka kusema? Kama Maaskofu wanawataka wakristo ambao makanisa yao yamechomwa "wasamehe na kuendelea kuwa raia wema katika nchi ya Tanzania." Wewe unapata wapi ujasiri wa kuropoka kuwa kwa mwenendo huu bado? Je ni suluhu gani unayoitaka ifikiwe? Kama hauna cha kusema sio lazima useme.

Daniel Marura
--

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment