Friday 26 October 2012

Re: [wanabidii] SHURA YA MAIMAMU TANZANIA KAMATI KUU YA SIASA - UCHAGUZI MKUU 2010

Ndugu zanguni,ktk Tanzania,kama waislam hawatarekebisha mtindo wao wa kufikiri,hakuna kiongoz yeyote atayefanikiwa kulinda amani na umoja wa kitaifa na kudumisha misingi ya nchi kwa kuwasikiza waislam.Na waislam ni lazima wajue kuwa wao siku zote hawatasikizwa kwa wingi wao au kwa kuwa maoni yametolewa na wao.Kitachofanya wasikizwe ni busara au munyo wa ushauri wao.Nashauri,waache mara moja kuipigia serikali kelele kuwa iwasikize bali waangalie mantiki ya mashauri yao na kama yanasikizika.Huu ndio ukweli.Maandiko mtakatifu yanasema mtu mwenye busara siku zote atamtawala watu wajinga hata kama wana mali.Ngupula



------------------------------
On Sat, Oct 27, 2012 7:40 AM EEST Mohamedi Mtoi wrote:

>Rejeeni "Hawa ndio maadui wa uislamu na uislamu wenyewe" Mohamedi Mtoi.
>
>Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
>
>-----Original Message-----
>From: dani killo <killodani@yahoo.com>
>Sender: wanabidii@googlegroups.com
>Date: Fri, 26 Oct 2012 11:15:22
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
>Subject: Re: [wanabidii] SHURA YA MAIMAMU TANZANIA KAMATI KUU YA SIASA -
> UCHAGUZI MKUU 2010
>
>Ndugu,
>
>Ulichoongea ni siasa na siasa zenyewe ni chuki dhidi ya Ukristo na Wakrito si vinginevyo.
>Chuki zenyewe ziko moyoni mwako  na kwenye mioyo ya wale wenye mtazamo huo.
>nimesoma kila ulichokiandika, hapa ni uchochezi wa kuchochea umma wa Watanzania kuona kwamba adui wa Waislam ni Wakristo. Mimi binafsi sishawishiki kabisa kuamini mfumo wa serikali ya Tanzania ni mfumo Kristo, kama unavyodai;
>    kwanza Kama maaskofu walienda kwa rais kueleza hisia zao, basi kwa kutumia busara (walizotumia maaskofu) na mshehe wangeiga nao wakaomba kufanya hivyo.
>   Pili, kutoa vifungu vya  maandishi kutoka nyaraka ambazo sio rasmi au rasmi, hizo ndizo vigezo vya kwenda kwa rais na kumuonesha na kufikia muafaka  na kuondo shaka zote hizo.
>   Maisha magumu ya nchi hii sio kwa Waislamu tu, bali kwa kila mwananchi wa hali ya chini au mwenye kipato cha chini, sidhani kama kila mwananchi mwenye kipato cha chini katika nchi hii ni Mwislamu.
>
>Kukusaidia;
>Hayo yote unayoyasema hapa kama kweli una ushahidi nao peleka sehemu husika mpange hatua ya kuonana na mkuu wa dola ambaye ni rais. Na kumueleza wasiwasi wenu kuhusu jambo fulani .
>  Maaskofu, kwa Wakristo, wanawachukulia kama viongozi wa kidini tu.wao ni wanadamu,wakienda kinyume  waumini huwaita na kuwambia makosa yao kama wakisema hafai hafai tu.aondoke. Sasa waislam kama tunauhakika hawa maaskofu wamepotosha serikali waiteni pamoja na serikali muwaeleze madhaifu yao kama wanadamu. Wanadamu wote wanamadhaifu[hata wewe unamadhaifu yako mengi sana usijione umekamilika] lakini yanaongeleka kila mtu ana makosa, hata Mwenyezi Mungu alilijua hilo ndo maana akatuwekea nafasi ya TOBA. sasa kama wanadamu hatujui kusamehe basi hatutasamehewa kamwe.Lakini tufikie muafaka kwa maongezi ya kukutana pamoja sio kutumia jukwaa kama hili na kupandikiza mbegu mbaya na mtazamo mbaya kwa umma wa Watanzania. Kama wamepindisha maadili ya   nchi waambiwe na sio kulalamika pembeni.isionekane kweli  upande mmoja unakandamizwa sio kweli. Mfano mtu amekukanyaga unamwambia, kama ni bahati mbaya atakuomba msamaha.
>   Watanzania wengi ni waumini wa dini mbalimbali,hatujawahi kuchagua kiongozi ambaye sio muumini, ikitokea basi utaratibu utaafutwa wa kumuapisha.
>  Kutokana na maelezo yote hayo , TATIZO  kubwa nililoliona ni kwa serikali na sio Ukristo na Wakristo.Kwamfano hospitali nyingi zilizojengwa zilijengwa na makanisa tangu kipindi cha ukoloni, serikali ndio ikataifisha hospiali na mashule yaliyo kuwa chini ya makanisa
>ili kila mwananchi aweze kupata elimu bila ubaguzi wa kiitikadi za kididni(wakati wa ukoloni), kama unafuatilia mambo , wakoloni walikuwa wanajenga vitu vitatu katika sehemu moja au karibu zaidi, walikuwa wakijenga kanisa watajenga na shule na hospitali. Kwahiyo serikali haikutumia nguvu nyingi kujenga mashule  na hospitali bali zile zilizotaifishwa kutoka kwa wakoloni ziliendelezwa tu, shule zingine tangu enzi ya mkoloni labda wamebadilisha madawati.Mfano mzuri, shunle ya Ndanda - Mtwara, ilikuwa inaitwa(hata sasa) Ndanda Mission School, kulikuwa na mgogoro unafukuta kuwa wanafunzi wa kiislamu wanataka serikali iwajengee msikiti kama walivyojengewa wanafunzi wa kikristo! Hapa hakuna mtu alifikiria kwanza au kutafakari historia ya shule wakaingia kwenye maandamano moja kwa moja kuishinikiza serikali kujenga msikiti.
>  Niliposikia mfumo Kristo nilifikiria mambo yafuatayo;
>1. Kuna baadhi ya ofisi za serikali makanisani
> 2.Labda Wkristo peke yao wanaruhusiwa kuingia ofisi za serikali.
> watu walioongeza siku ya mapunziko ni walimu ambao kwa umoja wao waliishinikiza serikali sio kwa nguvu wala maandamano bali kwa hoja tu na serikali ikakubali, waalimu wana wa dini mbalimbali wakaungana wakaubaliwa.
>  Fahamu hapa kwamba Uhuru wa nchi haukuletwa na dini bali umoja na ushirikiano wa wananchi wenye uelewa na upendo wakati huo.
>   Sasa hivi kuna kundi kubwa tu la wananchi ambao wanashawishiwa na nchi za mgharibi na kuahidiwa mambo makubwa wakisha fanikisha matakwa ya hao  wakubwa,
>kwamfano, nitakutajia baadhi ya nchi ambazo aidha ni za kiislamu kabisa au zinaendeshwa kwa misingi ya Uislamu na mifumo ya serikali zao pia; Somalia, Libya, Yemen, Pakistani, Iran na Iraq. Hizi nchi nchi zilikuwa na ugonvi (Iran na Iraq) jiulize tatizo liko wapi? zote ni nchi za Kiislam, walishindwa kukaa na kujadili mambo yao wakayamaliza kwa amani?
>Somali; 100% ni Uislam na Waislam wameshindwa kukaa meza moja? hakuna amani.
>Libya; rais wao alikuwa akijenga misikiti Afrika nzima hata pale Dodoma kuna msikiti wa Gadafi, amewapa kilakitu, walishindwa kumuita na kumshauri ang'atuke mpaka wamuue.
>Yemen karibia wote ni waislam sasa na serikali inaendeshwa kwa maadili ya Kiislam sasa wanagombania nini? kwani wasikae na kuelewana.
>Nigeria; Kikundi cha Waislam kinaongoza kuchoma makanisa hataleo, pana kimeanzia mbali kinaenezwa taratibu mpaka ifkie dunia mzima.
>Hiyo ni baadhi ya mifano ambayo kundi la watu au nchi fulani wanatafuta udhaifu wa nchi fulani halafu inakuwa ni kichochezi ili wapate kujitokeza baadae na wananchi bila kufanya tafakuri wanakurupuka na kuharibu nchi yao kama Misri Libya na Syria,hapa Afrika mashariki; mfano Kenya kuna ukabila wakatumia ukabila, Tanzania hakuna ukabila, kwahiyo  wanatumia nafasi ya udini,Ugand hakuna ukabila kwahiyo wanachomeka udini .Rwanda ukabila, Burundi-ukabila.
>Kama unakumbuka hata sasa kule Zanzibar sehemu ya jamhuri ya muungano ya Tanzania.; mfumo mzima ni Uislam kuanzi kiongozi wa juu mpaka wa chini ni Muislam, unakumbuka kilichotokea hapa, kikundi cha Kiislam cha uamsho kikaandamana ETI kinapinga Muungano, wakachoma makanisa kwa kupinga muungano.  Waislam hatuna hoja nzito ni maneno tu ya kubambikizwa na wasiopenda amani ya nchi hii kwa kupandikiza watanzania mbegu za chuki. HIVI muungano na makanisa kuna uhusiano gani? Baraza zima la mapinduzi ni la kiislam wameshindwa kuunda mahakama ya kadhi.
>Hapa ninachokiona ni waislam waangalie wamejikwaa wapi na sio kumtafuta mchawi. Kama misaada ya makanisa imefutiwa kodi, ni misaada gani waislam waliomba kufutiwa kodi serikali ikakataa?
>   Mikoa ambayo eti haiendelezwi kwa sababu ya udini, hili sio kweli hata kidogo, nataka nikwambie halafu fuatilia, Mkoa wa Arusha; miaka ya 2010 kuja nyuma kulikua na hali mbaya ya kimazingira ambayo viongozi wa CCM wanapokelezana uchafu uliokidhiri na hali mbaya ya wananchi kiuchumi, WANANCHI WALIPOONA HILO WAKAACHANA NA CCM, WAKACHAGUA UPINZANI; SASA HIVI MTU ALIYEFIKA ARUSHA 2009 KWENDA NYUMA ,AKIENDA  LEO HII ATONA MABADLIKO MAKUBWA SANA. NA MIKOA YA TANGA, PWANI NA MTWARA ikiadhimia kwa makusudi kuiweka ccm pembeni wataona mabadiliko.FANYA UCHUNGUZI. Kwa mtu yeyote asiyekubali mabadiliko hatapiga hatua ya kimaendeleo , mtu hatumii nguvu wala dini kupiga kura zaidi ya kuchukua muda wake .
>  Ndugu Waislam tatizo hapa ni serikali sio Ukristo na Wakristo, mtachoma nyumba za ibada na maisha hayatabadilika zaidi ya kuzidi kuwa mabaya tu, makanisa hayazuii uislam kusonga mbele  ,wala misikiti haizuii Ukristo kusonga mbele. JIULIZE; MAASKOFU WAMECHOMA MISIKITI MINGAPI ILI KUFIKISHA UJUMBE KWA SERIKALI NA WAKASIKILIZWA! hawajachoma hata kibanda cha msikiti lakini wanafikisha ujumbe kwa serikali na wanasikilizwa. Zipo elimunyingine hutafuti, unaiga tu, haiitaji nguvu wala pesa. Iweje kuchoma makanisa iwe ni jibu kwa matatizo ya waislam? huo mfumo Kristo unaosema ni chuki tu dhidi ya Ukristo, kwa sabu haiwezekani.Basi wakristo wote wangekuwa na hali nzuri kimaisha!
> Ngu Waislam pangeni mipango ya kielimu ,maendeleo ya kimaisha Ukristo hauna chchote cha kuzuia mipango ya maendeleo, hapa ninachoona Waislam wanategemea serikali iwafanyie kila kitu, kujenga misikiti,

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment