Sunday 21 October 2012

Re: [wanabidii] Sehemu Ya Msimamo Wa CHADEMA Kuhusu Kukamatwa Sheikh Ponda & Amir Farid - Mwanzo

Udini haukuanza 2010. Mwalimu Nyerere aliuona akausema 1995. Ulianza wakati wa awamu ya Pili. Ni upuuzi kuupuuza toka pale. Ni upuuzi kumpuuza Mwalimu Nyerere. Ni upuuzi kuendelea kuwapumbatia viongozi wapuuzi wanaopuuza udini. Wanaupuuza kwa kutokubali kuwa wana udini. Bali kila anayesimama jukwaani huku akitenda kwa udini anahutubia kuukemea udini
Tumeandika makala hawasikii. 2015 tusiwapuuze la sivyo nasi tutakuwa wapuuzi

--- On Sun, 10/21/12, Joseph Kahoko <jkahoko@yahoo.com> wrote:

From: Joseph Kahoko <jkahoko@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Sehemu Ya Msimamo Wa CHADEMA Kuhusu Kukamatwa Sheikh Ponda & Amir Farid - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, October 21, 2012, 1:03 AM

Mbegu hii ya udini ilipandikizwa na CCM mwaka 2010 ili kuvuna kura za Waislam. Walizipata kura hizo na kushinda uchaguzi lakini matokeo yake sasa ndio haya. Waliahidiwa mambo mengi sasa wanataka yatekelezwe lakini hayatekelezeki. Tatizo ni tamaa za kupata madaraka bila kuangalia gharama za kuyapata hayo madaraka. Hivyo naunga mkono kauli ya  Profesa Safari anaposema matatizo yanayotokea sasa, yameletwa na CCM kutokana na hatua yao ya kuwatumia baadhi ya waislamu kupandikiza mbegu ya udini nchini. 

--- On Sun, 10/21/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Sehemu Ya Msimamo Wa CHADEMA Kuhusu Kukamatwa Sheikh Ponda & Amir Farid - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, October 21, 2012, 7:49 AM

Sina uhakika kama tamko hilo limehaririwa na viongozi wa juu wa CHADEMA nashawishika kuliiita tamko hilo kwamba ni maoni binafsi ya Marando na Prof. safari. Siamini CHADEMA kama imefika mahali pa kukosa uelekeo kiasi hicho. Kuna mambo hapa yanajikanganya. Wanasema waislamu wana madai yao ya msingi kwa serikali sawa na kwamba BAKWATA haikubaliki vizuri kwa waislamu.

Hivi wao Marando na Safari hayo madai wameyatoa wapi? Vurugu zinazoendelea hazina sura kama hiyo wanayodai badala yake zina sura ya udini hili halina ubishi. Kama madai yao ni kwa serikali na kutoikubali BAKWATA basi tungeshuhudia wakichoma mali za serikali na za Bakwata ikiwemo misikiti.

Tunakumbuka vizuri sana kwamba uliwahi kuwepo mzozo kati ya BAKWATA na BALUKUTA na mwisho wa siku BALUKTA ilifutwa na serikali. Kwa wakati ule ilikuwa ni sawa. Kwa sasa sura imekwishabadirika na kuanza kudai kwamba serikali ni ya mfumo kristu na hivyo wanapambana na ukristu siyo serikali wala BAKWATA. Matukio ya uchomaji wa makanisa, mihadhara ya kukashifu ukristu, pamoja na uchomaji wa mabaa na ubomoaji wa butcher za nyama ya nguruwe ni matukio yaliyo wazi. Kama wana madai kwa serikali basi ndo hayo ya kuishi kwa mjibu wa sharia siyo sheria ambazo rais aliapa kusimamia au pengine wanadai ukristu usiwepo Tanzania. Hayo ndiyo madai munayotaka serikali ijadili na hicho kikundi cha baadhi ya waislamu?

Kikundi hicho cha waislamu kimekwishabadilisha mwelekeo na kuanza vita na ukristu wala hakina matatizo na serikali. Pamoja na kwamba rais ni muislam wakiwemo mawaziri kadhaa na viongozi wengine bado kundi hilo linaendelea kusisitiza kwamba serikali ni ya mfumo kristu.

Marando na safari pengine muko sawa munaposema tatizo imelilea serikali kwa kuwaacha wavuruga amani na uhuru wa watanzania kuendelea na harakati hizo kwa muda mrefu bila kuchukuliwa hatua zinazofaa. Hili la Ponda kunyimwa dhamana binafsi sioni kama ni tatizo la msingi, tatizo la msingi ni kuchimbua mizizi ya vurugu hizi na wala siyo kushughulikia dalili. Ponda kwa sasa ana kesi kibao ata akiachiwa kwa kesi hiyo bado anaunganishwa na wale muliowaita wahuni waliovunja makanisa wakiwa na siraha (armed robbery) hiyo dhamana munayopigia kelele itakuwa na maana gani? Ponda si mgeni katika kuchochea vurugu za kidini ni mzoefu wa siku nyingi.

Natofautiana na nyinyi kwa kusema kama munawaita waislamu hao kwamba ni kikundi cha wahuni basi ni hatari. Maana mipango ya kufanya uhuni ilifanyikia misikitini na baada ya swala ya ijumaa ni watu hao hao waliotoka misikitini na kuanza fujao. Muna maana serikali imekiruhusu kikundi cha wahuni kujenga misikiti huko mbagala na kwingineko? Mimi nasema si kikundi cha wahuni bali ni kundi fulani la waumini wa dini ya kiislamu wakiongozwa na Ponda.

Munaposema waislamu wanayo madai ya msingi pengine ni kweli yapo lakini hiki kikundi cha Ponda ndo wawakilishi wa waislamu wote? Kikundi cha Ponda mumekiita kikundi cha wahuni ina maana wazee wa kiislamu wenye busara zao wamekituma kikundi cha wahuni kudai haki za waislamu kwa kuchoma makanisa? Acheni kutafuta maneno yasiyokuwa na kichwa wala miguu nafuu mungekaa kimya namna hiyo munaifanya CHADEMA iwe na sura ya watu wasiokuwa focussed na wanaolazimisha hoja bila misingi. Au mumetumwa kukichafua CHADEMA?

2012/10/20 ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Ipo siku CHADEMA itaipinga serikali ikisema 2 x2= 4.
Ninailaumu sana serikali kwa kutokaa na wapinzani kutafuta msimamo wa Pamoja kuhusu maswala ya kitaifa kama Mgogoro wa Malawi, Vurugu za WAislam nk.
Israel ilipoivamia Entebe Uganda kuwakomboa wananchi wao waliokuwa wametekwa na magaidi wa Kipalestina. Kiongozi wa Upinzani aliyekuwa ameshirikishwa siri hiyo alijitokeza hadharani kutetea kitendo hicho cha Serikali
Sasa Chadema ambao wako dressing room wakijiandaa kuchukua dola wanaweza kuikosoa serikali kuhusu msimamo wa Mahakama kuhusu dhamana ya Ponda? CHADEMA iangalie sana. Obama ameanza vizuri kampeni. Lakini kadri siku zinavyokaribia uchaguzi kura zake zinapungua. CHADEMA hawaelekei huko?

--- On Sat, 10/20/12, Magiri paul <kiganyi@gmail.com> wrote:

From: Magiri paul <kiganyi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Sehemu Ya Msimamo Wa CHADEMA Kuhusu Kukamatwa Sheikh Ponda & Amir Farid - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, October 20, 2012, 11:17 AM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekutana na waandisihi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam leo, ambapo wajumbe wa Kamati Kuu, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, wameweka waziwazi msimamo wa chama hicho kuhusiana na mgogoro kati ya waislamu na serikali na kukamatwa kwa Sheikh Farid huko Zanzibar.
http://wotepamoja.com/archives/9371#.UILqpeUSd8k.gmail
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment