Sunday 7 October 2012

Re: [wanabidii] RE: MWALIKO KUHUDHURIA NA KUSHIRIKI SHEREHE ZA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE DUNIANI JUMA TANO TAREHE 10/10/2012 VIWANJA VYA TGNP MABIBO

Dunia inazidi kuw ya kibaguzi
Kila siku tunazidi kujibagua na kuweka sherehe ya kundi fulani, kila kikundi au jamii fulani inataka kutambuliwa, taratibu tunaanza kumong'onyoa umoja wetu maana kama kuna siku ya watoto wa kike duniani lini ni siku ya watoto wa kiume duniani?
utasikia siku ya kuadhimisha walemavu wa macho, masikio, ngozi, miguu, mikono, wagonjwa wa kansa, siku ya wanawake (sijui ya wanaume ni lini) na vikundi viiiingi list inaendelea.
Kwangu mimi huu ni ubaguzi unaingia pasipo sisi wenyewe kujua.
Watoto wote ni sawa kwangu awe wa kike au wa kiume.

Jamani tunakwenda wapi nisaidieni


2012/10/7 Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
 
Hata sheria za nchi zikibadilika suala la kuoza watoto wadogo wa kike halitobadilika kama jamii hiyo na familia hiyo haitaki kubadilika kukubali wasioze mtoto mdogo. Watahama waende porini kabisa na msichana kutoroshwa na mumewe wakatokomea. wanaharakati wakifungua kesi nbaada ya kupata taarifa wazazi na ndugu watashirikiana kuhonga kesi inakuwa ngumu. Pia, msichana akikataa kuozwa akitoroka au kushitaki anaweza kuuawa akafukiwa hakuna atakayejua. Hata kesi za ubakaji ndani ya familia zinashindikana kwa wanandugu kutokutoa ushirikiano na kutoa ushahidi wa uongo na kumtishia anayeifuatilia au mshitaki. Wengine hujali kupata mahari ya fedha au mifugo bila kujali uambukizi wa HIV, haki za msichana na haki za binadamu. Mila ni nini? mbona inaweza kubadilika kama tu tutakubali kubadilika. Kuna usemi kuwa hata elimu ya vidato na ya uelewa ya uovu ni muhimu lakini sio solution kuwa itabadilisha behaviour ni mpaka mlengwa akubali kubadilika (health education or education is important but not sufficient for behaviour chage).
 
Sheria itasaidia lakini sio ndio tija maana hata mwizi anajua atafungwa na mbakaji pia atakula miaka 35 lakini bado anatenda uovu. Hata hakimu au polisi anapokea rushwa na sheria na adhabu anazijua. Ndoa za umri mdogo zinaongeza Fistula, HIV, mateso, uduni wa elimu na kurudisha maendeleo nyuma. Limbikizo la mifugo kutokana na mahari uharibifu wa mazingira. wengine huingiza udini ktk ndoa za aina hii. Hii leo TZ kuna watu wanaoza mtoto wa mama mkubwa na mdogo au umeolewa umemkuta mume anawatoto wa kiume nawe umekuja na wa kike toka ndoa ingine hao wanaozwa (mume kakuoa wewe mwanae wa kiume anaoa wako wa kike uliyekuja nae au wa mdogo wako). Bado jamii zinasafirisha watoto wa kike kuwaoza kwa mizee huko Ngazija au Oman. Hawajali nani anampenda nani bali kumlazimisha mtu aolewe tena za zee au kijana asilolipenda. Halafu lawama nyingi kuhusu elimu kuwa duni, wasichana hawasomi, jamii ya kabila fulani au dini fulani haina elimu wakati sisi nasi tunahusika kutokutilia maana elimu ya darasani kwa sababu zetu binafsi.

From: Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, 6 October 2012, 16:08
Subject: Re: [wanabidii] RE: MWALIKO KUHUDHURIA NA KUSHIRIKI SHEREHE ZA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE DUNIANI JUMA TANO TAREHE 10/10/2012 VIWANJA VYA TGNP MABIBO

Mikakati gani inatarajiwa kuundwa katika jitihada za kutokomeza ndoa za utotoni? Lazima sherehe hizi za mtoto wa kike ziwe na maana, na hii si nyingine, bali  wadau waje na mikakati hiyo. Si jambo rahisi kutokomeza ndoa za utotoni kwa kuwa ni jambo lililojikita katika utamaduni-desturi, mila ambazo zinahitaji kubadilishwa kidogokidogo. Lakini pia lazima lianze kushambuliwa kwa kuweka sawa sheria zetu. Je, zina unga mkono juhidi hizi zetu sisi wadau wa utetezi wa haki za mtoto hasa huyu wa kike? Kazi ni kwetu!
Vin 

2012/10/6 Demetria Kalogosho <demetria.kalogosho@tgnp.org>
Wapendwa,                                                                                                    
 
 
              
RE: MWALIKO KUHUDHURIA NA KUSHIRIKI SHEREHE ZA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE DUNIANI JUMA TANO TAREHE 10/10/2012 VIWANJA VYA TGNP MABIBO
 
Salaam kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)!
 
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ni shirika lisilo la kiserikali lenye dira ya kuwa na jamii ya Tanzania yenye usawa na haki kijinsia, wanawake walio na maendeleo maisha endelevu na haki ya kijamii. Ni shirika tetezi la haki za binanadamu, hususani haki za makundi yaliyoko pembezoni, ya wanawake, ya walemavu, ya wasichana, ya vijana, ya watu waishio na VVU/UKIMWI nk. Dhamira yake ni ukombozi wa wanawake kimapinduzi.
 
Kuhusu Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, 'INTERNATIONAL DAY OF THE GIRL CHILD, ni siku ya kimataifa itakayosherekewa Oktoba 11 ulimwenguni kote.  Siku hii itasherekewa kwa mara ya kwanza duniani baada ya kupitishwa na kutangazwa na Umoja wa Mataifa  kupitia mkutano wake mkuu wa tareha 19/12/2011. Hii ni siku ya kutambua haki za wasichana na changamoto maalumu zinazowakabili kama wasichana ulimwenguni. Hii imetokana na kampeni za miaka mingi za wanaharakati wa Kanada na Amerukani. Siku hii,  imetengwa maalumu kwa ajiri ya wasichana kufanya  utetezi na kuchukua hatua wao wenyewe na kwa ajiri ya wenzao. "Tokomeza ndoa za utotoni"; ndio kauli mbiu ya siku hiyo.
 Lengo na madhumuni makuu ya siku ya mtoto wa kike ni kutangaza,  kuhamasisha na kuongeza uelewa  na  ufahamu juu ya,  na kutetea  haki za mtoto wa kike ulimwenguni.  Uamuzi wa Umoja wa Mataifa kutangaza siku hii ni ishara ya kutambua changamoto zao  na uwezo walionao wasichana. Pia Umoja wa Mataifa umeonesha dhamira yake ya kutokomeza mawazo mgando, ubaguzi, ukatili na tofauti za tabaka katika masuala ya kiuchumi yanayopelekea wasichana kupata vipato visivyo sawia.
 
Kwa kuungana na wenzetu duniani, TGNP, tumeamua kuisherekea siku hiyo katika semina yetu ya jinsia(GDSS) ya Juma tano tarehe 10/10/2012 hapa viwanja vya TGNP Mabibo karibu na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji.    Muda wa sherehe utakuwa ni masaa 2 tu. Tutaanza saa 9:00 alasiri na kumaliza saa 11:00 jioni. Mada ya siku hiyo; "Tokomeza ndoa za utotoni:kuza vipaji vya wasichana". Pia kutakuwepo na jopo la wazungumzaji. 
 
Aidha napenda kukuhabarisha  kuhusu jukwaa la wazi kwa jamii maarufu kama 'Semina ya Jinsia na Maendeleo (GDSS). Semina hii hufanyikia viwanja vya TGNP Mabibo karibu na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Mkabala na Soko la Mabibo. Kwa kawaida, semina hii/jukwaa hili huendeshwa mara moja kwa wiki na huwa ni  siku ya Juma Tano saa 9 alasisri mpaka 11 jioni (kwa masaa mawili tu). Kulingana na Muktadha wa wakati huo, kwa kutumia mbinu mbalimbali, mada raghbishi hutolewa kwa  wanajamii ambapo masuala mbali mbali huibuliwa kwa mjadala na baadaye kumalizia na mkakati  wa nini kifanyike. Jukwaa hili linatoa fursa kwa wanajamii wote, wanawake kwa wanaume, vijana na makundi yote ya kijamii wakiwemo watu wenye ulemavu, waishio na VVU/UKIMWI, wanaharakati wa haki za binadamu na za wanawake. Bila kujali jinsi, umri, dini, itikadi za kisiasa, wanajamii huweza kukutana na kujadili mada mbalimbali za maendeleo na kutoa kero zao. Pia katika semina hizi washiriki hupashana habari mbalimbali, hujengeana uwezo, hujifunza, na kujenga mtandao wa vuguvugu la ukombozi wa wanyonge na makundi ya pembezoni.   
 
Hivyo, tunapenda kukualikeni, wanabidii nyote pamoja na mitandao yenu na marafiki, kuja kuhudhuria na kushiriki pamoja na Mtandao wa Jinsia Tanzania katika sherehe za siku ya kimataifa ya mtoto wa kike.
 
Mwaliko huu unatokana na kutambua juhudi na harakati zenu katika kuhabarishana na kupeana uzoefu katika nyanja mbalimbali za kijamii.
 
Kuhudhuria na kushiriki kwenu, kutawezesha mafanikio ya semina hiyo na siku ya mtoto wa kike duniani. Pia naomba kuzingatia kuwa usafiri wa kuja na kurudi ni wa kujitegemea. Huduma ya mkalimani wa viziwi itatolewa.
  
 Wako katika harakati za  kutetea haki za wasichana na kuinua vipaji vyao.
 
Asante.
 
 
 
Demetria Kalogosho
 
 
 
 
 
 
 
 
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment