Sunday 7 October 2012

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Yanga wanakwepa rangi ya mnyama

Wakati mwingine Viongozi wa Klabu hizi mbili [Simba na Yanga] hutumia ujinga wa washabiki wao kugomea vitu vya kijinga [Natumia neno ujinga kwa maana ujinga hutoka pindi mtu akielimishwa].

Viongozi wa Timu hizi 2 hawajadili wala hawasumbui akili zao kujiuliza hadi lini wataendelea kutegemea fedha za milangoni kuendesha Klabu? Hawajiulizi hadi lini wataendelea kutegemea mfuko wa mtu mmoja kulipia mshahara wa Mwalim wa Timu na baadhi ya Viongozi? Hawana muda wala hawajishughulishi hadi watakuwa na vitega Uchumi au Majengo ya kisasa ya Makao Makuu ya Klabu zao? Hawana muda wala hawataki kufikili na nadhani ni wavivu wa kufikili kwamba hadi lini watawaku kama walivyo.

Nataka kuwaeleza Viongozi hao wa Klabu hizi mbili zinazojiita kubwa wakati ni ukubwa wa pua ambao hauhalalishi kwamba ni vingi wa kamasi.

Fumbueni macho washabiki wa Yanga na Simba waulizeni maswali magumu hao mliowapa dhamana ya kuongoza.

On Oct 7, 2012 7:21 PM, "A S Kivamwo" <kivamwo@yahoo.com> wrote:
Sasa wewe Ngowi,

Kama damu yenu nyie watu wa Yanga sio kama ya mnyama (mammal) a.k.a nyekundu ni rangi gani? sasa..ha ha haa..usinichekeshe kuwa wana Yanga wana damu ya kijani ha ha ha ha!!!. Waambie yeboyebo wenzio wasikubali kushuka daraja, kisa eti doa jekundu tu!!
Mbona tutawa-miss mkishuka!

From: Deus Ngowi <deusngowi@yahoo.com>
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, October 7, 2012 6:30 PM
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Yanga wanakwepa rangi ya mnyama

Matinyi uliiona wapi hiyo damu?

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Mabadiliko <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, October 7, 2012 4:28 PM
Subject: [Mabadiliko] Yanga wanakwepa rangi ya mnyama

Jamani, wazee wa Yanga  akina Kulangwa na Simbeye, na wengineo,
Tafadhalini toeni ushauri kwenye chilabu chenu....hakuna ubaya kuvaa jezi yenye nembo ya Vodacom (rangi nyekundu). Mbona damu za Yanga wote ni nyekundu?
 
Vaeni tu rangi ya mnyama.
 
Yanga: Tupo tayari kushuka daraja Send to a friend
Saturday, 06 October 2012 10:16
Jessca Nangawe na Sosthenes Nyoni
UONGOZI wa Yanga umesema utasimama kwenye mstari wa utamaduni wa enzi wa klabu hiyo kutokuvaa jezi yenye rangi nyekundu, na kwa sababu hiyo haiko tayari kutumia jezi za wadhamini wakuu wa Ligi Kuu Bara, Kampuni ya Huduma za Simu ya Vodacom.
Katika kusisitiza msingi wa uamuzi wao, uongozi umesema uko tayari kwa hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yao na hata ikibidi kushushwa daraja lakini siyo kuvaa jezi za Vodacom zenye nembo ya rangi nyekundu.
Tayari Yanga imecheza mechi mbili za ligi bila kuvaa jezi zenye nembo ya Vodacom, huku wadhamini wao wakiwajibu barua yao kwa kusisitiza hawawezi kuondoa nembo hiyo ambayo walikubaliana nayo wakati wa kuingia mkataba wa pamoja.
Katibu mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako, alisema jana pamoja na vitisho kutoka Shirikisho la Soka Tanzanua (TFF) kutaka kuwashusha daraja na kuwatoza faini, hilo haliwasumbui na badala yake watabaki kwenye msimamo wao wa kuheshimu katiba yao inayotambua rangi za kijani, nyeusi na njano.
 
Endelea: http://www.mwananchi.co.tz/michezo/-/26458-yanga-tupo-tayari-kushuka-daraja
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment