Saturday 6 October 2012

Re: [wanabidii] Re: CHADEMA WAELEMISHENI WATANZANIA KABLA YA UCHAGUZI

Lengai ingefaa ukatumianjina lako halisi

DPK Ng'wizukulushilinde

On 6 Oct 2012, at 18:12, LENGAI OLDOINYO <lengai2000@yahoo.co.uk> wrote:

Mimi kama mwanachama hai wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA nawashauri viongozi wetu wajikite kuwaelemisha Watanzania nini maana ya ukombozi kwani mpaka leo kuna wanaoamini kuwa sio watumwa ndani ya CCM. Bado wanadhanishia CCM itabadili maisha yao kumbe chama kimekuwa cha ndugu na ukoo wa baadhi ya Viongozi.

 

Hivi kama viwanda vyote vya nguo kama URAFIKI, MWAREX, MUTEX, KILTEX, na vinginevyo vilivyoachwa na Wakoloni na hata vili vilivyoachwa na Baba wa Taifa viko wapi. Kuviua viwanda hivi ndiko kumechangia wakulima kukosa soko la kuuza Pamba.  Vimeishia mifukoni mwa viongozi wa CCM na kutufanya sisi watumwa ndani ya nchi yetu.

 

Hivi ile reli ya kutoka Dar es salaam kwenda Arusha na kutoka Tanga hadi Kprpgwe iko wapi kama sisi hatupo utumwani kuwazalishia viongozi na matajiri kwa kuchangia ujenzi wa barabara ili malori yao yapite na bidhaa zao waje kutulangua kama hatuko utumwani.

 

Hivi yale mashule ya bure aliyokuwa anayasimamia mkoloni na hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere yako wapi mpaka watoto wetu wanasomea kwenye mashule ya Kata yasiyo na madawati, Walimu na hata huduma hata za vyoo tukiachilia mbali maabara kama hatuko utumwani.

 

Hivi yale Mashamba makubwa ya Taifa aliyokuwa anayasimamia Mwalimu yakawa yanazalisha Ngano, Kahawa, Pamba, Katani yako wapi kama sisi Watanzania hatuko utumwani.

 

Hivi yale Mashirika makubwa yaliyokuwa yanasimamiwa na Serekali kama STAMICO, SHIRECU, KNCU, MWARECU, ARCU, TARECU, MORECU, TIPPER nk yamefia wapi kama sisi Watanzania hatuko utumwani.

 

Hivi ziko wapi fedha za Rada, Epa, Meremeta, Kagoda, Kiwira, na Dola Milioni 350 zimefichwa ulaya na kiongozi tuliyemuamini yuko komya kama hatupo utumwani.

 

Hivi wako wapi wale Wanyama pori walikuwa wamezagaa kila pahali wakati Hayati Mwalimu Nyerere akiwa hai. Yako wapi yale madini yalikuwa yanaokotwa juu ya ardhi enzi za Mwalimu Nyerere. Iko wapi ile misitu ya kutisha ambayo Mwalimu alikuwa anaitunza. Iko wapi ile mito mikubwa ya mafuriko tuliyokuwa nayo enzi za Hayati Mwalimu Nyerere kama hatuko utumwani.

 

CHADEMA kama mtawaelemisha Watanzania wajue kuwa kila alichoacha Mwalimu kimewekwa mfukoni na hawa viongozi wa awamu ya pili, ya tatu nay a nne nina imani kila mtu ataukataa utumwa na kuchagua chama cha ukombozi. Mtu anayemchagua Kiongozi aliyepo CCM kuingia tena Ikulu alaaniwe yeye na kizazi chake. Bora kukichagua chama kingine kulikoni CCM.

 

Tanzania pamoja na kuwa na rasilimali nyingi sana lakini CCM imetufanya watumwa ndani ya nchi yetu. Watanzania wanavunjiwa nyumba na kuachwa wakihangaika, Watanzania wananyang'anywa ardhi yao wanaachwa wakihangaika, Watanzania wananyimwa haki ya elimu, Watanzania wanajilipia huduma za afya, Watanzania wanapandishiwa bei za bidhaa. Watu wanataka mabadiliko wanatutishia vita. Wanzishe wao ndio wana vitu vya kuchoma wapate hasata. Mimi na nyumba yangu ya nyasi nina wasiwasi gani. Utumwa huu lazima tuukatae mwaka 2015.

 

Hakuna kuichagua CCM wala mtu alikuwa ndani ya CCM kati ya Mwaka 1997 hadi 2012. Viongozi hawa wametunyanyasa sana ndani ya miaka hii 15. Bora kuchagua CHADEMA, NCCR, TLP, SAU lakini CCM hapana. CUF pia inanipa mashaka. Yani pamoja na mateso yote haya ua utumwa tulio nao unasimama jukwaani kumpeza mpinzani mwenzako anayetaka mabadiliko unashadidia chama kilichosheheni Wizi, Ufisadi, Mauuaji, Utapeli, Unyanyasaji, Udhalilishaji nk.

 

Mtanzania anayekipigia upatu chama cha CCM ni mwenda wazimu au anayo masilahi anayopata nap engine amechukua rushwa ndani ya CCM. Mimi chama cha CUF kimenifadhaisha sana. Unayajua aliyoyafanya CCM mpaka hata kuwaua wanachama wako wa CUF kule Pemba leo unarudi unakaa na CCM meza moja?.

 

Kweli Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hakukosea kusea rushwa ni adui wa haki. Mwalimu Seif Sharif Hamad, na Lipumba mumechukua Rushwa ya uongozi na hata fedha inawezekana. Watanzania makini hawana imani na CUF. Mimi niwaulize tu Watanzania mliopo ndani ya CUF na CCM nyie mlipata nini wakati hawa wakubwa wanagawana madaraka. Au Ndio Mwenyezi Mungu anawapa adhabu ya kuvunjiwa nyumba na kunyan'ganywa mashamba ili wapewe wawekezaji. Watanzania tutavuna tunachopanda 2015.

Mkereketwa

Lengai Ole Letipipi

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment