Sunday 28 October 2012

RE: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja – Lipumba - Mwanzo



 


Ndugu zanguni,

Suala la dhamana sio haki ya moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Katiba yetu, maamuzi mbali mbali ya mahakama za ndani na nje, dhamana ni HAKI ya kila mtuhumiwa. Hata hivyo, mahakama hizi hizi, na baadhi ya sheria zetu zinaruhusu kukiukwa kwa HAKI hii kwa sababu mbali mbali.

Katiba yenyewe, kupitia Ibara ya 30, inatamka wazi kuwa haitakuwa ni uvunjaji wa HAKI iwapo haki na stahili zote zilizoorodheshwa ndani ya Ibara ya 12-29 (Bill of Rights) zitaondolewa katika kutekeleza sheria nyingine za nchi. Ibara hiyo inaelekeza kuwa dhamana inaweza kuzuiwa kwa "maslahi ya umma"(Public interest)-dhana tata!

Kif. 148 cha Sheria ya Makosa ya Jinai (Sura ya 16), mtuhumiwa anaweza kukataliwa dhamana endapo kosa halina dhamana(uhaini, mauaji, au unyang'anyi wa kutumia silaha)

Mtuhumiwa anaweza kukataliwa dhamana kwa sababu nyingine.

1)  Endapo kuwepo kwake huru kunaweza kuingilia upelelezi

2)  Endapo akiachiwa, anaweza asihudhurie mahakamani(km Mpakistani wa wanyamapori Arusha)

3)  Endapo kuwepo kwake huru kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani(Ally Athumani Maumba)

4)  Endapo kuwepo kwake huru, kutokana na kosa lake kuikera jamii, kutahatarisha usalama wake mwenyewe(Ally Athumani Maumba)

5)  Endapo atatenda kosa wakati akiwa nje kwa dhamana ya shtaka jingine

6)  Endapo atakosa wadhamini wenye sifa

7)  Endapo anasubiri kusafirishwa kwenye mahakama nyingine(yenye mamlaka ya kusikiliza kesi yake)

8)  Endapo ni raia wa nchi ya nje, na hiyo nchi ikaomba azuiliwe wakati taratibu za kuja kumchukua zinafanyika.

Uamuzi wa kukubaliana au kutofautiana na upande wa waendesha mashtaka uko kwa hakimu.(Entirely in his/her discretion).

Kwa anapoamua, upande usioridhika unayo haki ya kutafuta HAKI kwenye mahakama ya juu. Kauli ya kuiambia mahakama au mamlaka yoyote yenye dhamana hiyo, kuwa Sheikh Ponda aachiliwe, halikupaswa kutoka kwa mtu ambaye kwa miongo kadhaa, amekuwa akijinasibu kuwa anaweza akawa kiongozi wetu.

MJL

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment