Sunday 28 October 2012

Re: [wanabidii] Abridged summary of wanabidii@googlegroups.com - 98 Messages in 42 Topics

Prof. Lipumba sioni tofauti ya mawazo yako na waliojiita wasemaji wa
Chadema(Marando na Prof. Safari), matamko yenu yana harufu ya kuungwa
mkono na waislamu. Wakati wa kutoa matamko ebu jitahidini kukaa
katikati ili muweze kutoa hoja zenye mashiko. Ninahushimu sana
uprofesa lakini inafika mahali nashindwa kuuona uprofesa wenu kwenye
hoja munazozitoa.

Ni kweli serikali ya JK ilichelewa kufanya maamuzi katika swala zima
la chochoko za kidini, kabla ya tukio ilikuwepo mihadhara mingi sana
yenye malengo ya kukashifu dini za makundi tofauti. Upo uwekano mkubwa
kwamba kilichotokea Mbagala kilipangwa kwa muda mrefu iweje serikali
na mkono wake mrefu ishindwe kubashiri na kuzuia?

Kuhusu swala la Ponda naona munatafuta umaarufu tu, hivi mtu mwenye
madai ya kiwanja chake au jumuiya yake ana haki ya kuvamia kiwanja
hicho akiwa na mapanga pamoja malungu? Eti munajifanya hamjui sheria
na kusema aliyevamiwa apeleke kesi mahakama ya ardhi? Kwa uprofesa
wenu hamjui hapo kuna kesi nyingine mbali na madai ya kiwanja?

Munapoilaani serikali kwamba Ponda kaunganishwa na kesi ya kuchochea
vurugu za Mbagala ina maana hamjui kwamba Ponda kwa sasa kashikiliwa
kwa kesi ya kiwanja wala ya siyo ya vurugu za mbagala? Je muna uhakika
gani kama kupitia upelelezi Ponda hausiki na vurugu za Mbagala? Kwa
vile kesi iko mahakamani na upelelezi unaendelea kwa nini musisubiri
kesi isikilizwe na kutolewa hukumu ili tujue kama Ponda aliusika au
la?

Inakuwaje mutwambie waliohusika kuvunja makanisa ni wahuni na hapo
hapo munasema serikali inachochea vurugu miongoni mwa watanzania wenye
imani tofauti kwa kuchelewa kushughulikia kesi. Kwani wahuni si
wahuni tu tena wa dini tofauti na watashughulikiwa kwa mujibu wa
sheria?
Kama ni wahuni na vurugu zote zilianzia misikitini basi ni vibaka
ambao walitumwa na uongozi wa misikiti la sivyo tungekwishasikia
kwamba misikiti ya Mbagala ilivamiwa na kutekwa na vibaka ili wapange
mambo yao ya kuvunja sheria.
TOENI HOJA ZENYE KUJENGA SIYO KUJITAFUTIA UMAARUFU KISIASA INAPOTOKEA
MATATIZO YA KULITUMBUKIZA TAIFA KWENYE VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE

2012/10/28 Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com>:
> Naona hapa kuna makengeza, Ponda ana kesi ya wizi katika kampuni ya
> afritanza ltd, hakuwa kati ya watu walioba kanisani wala sio sheikh wa
> msikiti wa waumini vibaka. Kwa maelezo ya wachangiaji hata wakili wa Ponda
> hajishughulishi kupeleka shauri mahakama kuu kudai dhamana ya Ponda,
> chamsingi hapa wapatikane wanasheria mahiri ili atendewe haki stahiki, kama
> belusconi alivyosema "kuna unyanyasaji wa kisheria" inawezekana hata Ponda
> anapata unyanyasaji wa kisheria tu.
>
>
> 2012/10/27 Godfrey Ngupula <ngupula@yahoo.co.uk>
>>
>>
>> ni swali nzuri bwana Kagaruki.Nafikiri waislamu wanayomengi ya kufanya
>> kuhakikisha hisia juu ya Mungu wao hazizidi uwezo wao wa kufikiri.Uislam uko
>> kwa ajili ya mwanadamu na si mwanadamu kwa ajili ya uislamu.Na pia,muonekano
>> wa waislamu mbele ya jamii utatokana na matendo yenu na si maneno peke yake.
>>
>> Ni kweli malez ya vijana wetu ipo haja ya kuongeza msisitizo.Wanadini
>> tuache kuwadanganya na kuwatia hofu vijana wetu na pia umuhimu wa kuheshimu
>> imani za wengine.Ngupula
>>
>> ------------------------------
>> On Sat, Oct 27, 2012 10:45 PM EEST Lutgard Kagaruki wrote:
>>
>> >Mbona kule Pemba muislamu aliyekojolea kitabu chenu na kumvalisha tasbihi
>> > mbwa hakusulubiwa wala makanisa kuchomwa?
>> >
>> >
>> >
>> >Lutgard Kokulinda Kagaruki
>> >Executive Director
>> >Tanzania Tobacco Control Forum
>> >P. O. Box 33105
>> >Dar es Salaam, Tanzania
>> >Tel: Off. +255 732 924088
>> >Tel: Mob. +255 754 284528
>> >Fax: +255 22 2771680
>> >
>> >
>> >
>> >
>> >________________________________
>> > From: Ibrahim Lipumba <lipumba@yahoo.com>
>> >To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
>> >Sent: Saturday, October 27, 2012 10:18 PM
>> >Subject: Re: [wanabidii] Abridged summary of wanabidii@googlegroups.com -
>> > 98 Messages in 42 Topics
>> >
>> >
>> >Ndugu Tony na wengine ni hii ifuatayo. Mara nyingi nimetoa maelezo
>> > kulaani vitendo vya kuonewa watu mbalimbali. Hata Mhe. Freeman Mbowe
>> > alipokamatwa na kuwekwa ndani kwa kisingiziyo cha kutohudhuria mahakamani na
>> > nikaenda kumtazama Central Police Station. Kila mtu ana haki ya kuunga mkono
>> > chama na wanasiasa anaowapenda lakini si vyema kupotosha na kujenga chuki.
>> >TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: WATANZANIA TUSIKUBALI
>> >KUINGIZWA KATIKA MAPAMBANO YA KIIMANI
>> >Nchi yetu imeingia katika mgogoro na mtafaruku mkubwa
>> >baada ya kijana mmoja kukojolea kitabu cha Qur'an tukufu maeneo ya
>> > Mbagala na
>> >kufuatiwa na baadhi ya makanisa hapa nchini kuharibiwa na kuchomwa moto.
>> > Kwa
>> >Waislam kitendo cha kuinajisi Qur'an ni udhalilishaji wa hali ya juu na
>> > vyombo
>> >vya dola vinapaswa kuelewe kuwa hisia za Waislam wengi zinaathiriwa sana
>> > na
>> >kitendo hicho. Hatua za haraka za kumkamata na kumuhoji kijana
>> > aliyehusika na
>> >kutoa maelezo kwa umma kuwa suala hili linashughulikiwa ipasavyo
>> > kungewatuliza
>> >wananchi wengi. Kuchelewa kuchukua hatua kulitoa mwanya kwa watu wengine
>> > na
>> >vibaka kuvamia Makanisa kupora, kuyaharibu na kuyachoma moto. Kitendo
>> > hiki
>> >kimewaumiza, kuwakasirisha na kuwafadhaisha Waumini wa Makanisa hayo na
>> >Watanzania kwa ujumla.
>> >CUF Chama Cha Wananchi kinalaani vikali kitendo
>> >kilichofanywa na kijana kunajisi Qur'an tukufu. Huku ni kuporomoka
>> > kukubwa kwa
>> >maadili ya vijana wetu. Kitendo cha kijana huyu kilipaswa kuchukuliwa
>> > hatua
>> >mara moja baada ya taarifa kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
>> >Kitendo cha kijana huyu hakihalalishi kwa namna yeyote
>> >ile kuvamia makanisa, kuyapora, kuyaharibu na kuyachoma moto. CUF Chama
>> > Cha
>> >Wananchi kinalaani vikali vitendo vya kihalifu na vya kuchochea mfarakano
>> > ndani
>> >ya jamii vilivyofanywa na watu na vibaka waliovamia makanisa haya.
>> > Tunawapa
>> >pole Waumini wote walioathirika na matukio haya.
>> >Baada ya matukio ya kuharibu makanisa, polisi walieleza
>> >wamewakamata watu waliohusika na vitendo hivyo na kuwa watawafikisha
>> >Mahakamani. Rais Kikwete alienda kukagua makanisa yaliyoathirika na
>> > kuwapa pole
>> >waumini wa makanisa hayo. Hii ilikuwa hatua ya mwanzo yakulirudisha taifa
>> >katika maelewano.
>> >KUSHIKWA KWA SHEIKH PONDA
>> >Katika hali hii ya kuvurugika kwa amani kulikochangiwa na
>> >vyombo vya dola kutochukua hatua za haraka dhidi ya kijana aliyeinajisi
>> > Qur'an,
>> >polisi walimkamata Sheikh Ponda. Vyombo vya Habari vimemnukuu Kamanda wa
>> > Kanda
>> >Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akieleza pamoja na mambo mengine
>> > kuwa
>> >Sheikh Ponda "Amekuwa akifanya maandamano kinyume cha sheria na hata
>> > kutishia
>> >umwagaji damu Dar es Salaam, kipindi chote tulikuwa katika uvumilivu wa
>> > kufuatilia
>> >nyendo zake kila kukicha,...licha ya hali hii, Oktoba 12, mwaka huu,
>> > Ponda
>> >pamoja na wafuasi wake, walisababisha kuvunjwa makanisa usiku wa manane,
>> >uharibifu wa magari na wizi na upotevu wa vifaa katika makanisa… haya
>> > yote
>> >yameongozwa na Ponda na madhara yake ni makubwa." (Mtanzania ALHAMISI,
>> > OCTOBA 18, 2012
>> >05:06)
>> >Unaweza usikubaliane na Sheikh Ponda katika maelezo na
>> >msimamo wake kuhusu dhulma dhidi ya Waislam, lakini ni makosa makubwa
>> > kumsingizia mambo ambayo hakuyatenda. Kwa jeshi
>> >la polisi kutoa shutuma hizi ambazo hazina msingi wowote kunaongeza
>> > mfarakano
>> >ndani ya jamii.
>> >Hata hivyo kesi aliyoshitakiwa Sheikh Ponda ni ya kuvamia
>> >kiwanja kisochokua chake. Kiwanja ambacho Sheikh Ponda anadaiwa kukivamia
>> > ni
>> >kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na East African Muslim Welfare Society
>> > kwa
>> >madhumuni ya kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam. Baada ya serikali kuivunja
>> > East
>> >African Muslim Welfare Society na kuanzisha BAKWATA, mali zake
>> > zilikabidhiwa
>> >BAKWATA. Anachodai Sheikh Ponda ni kuwa kiwanja hicho cha Waislam
>> > kimeuzwa
>> >kinyume cha utaratibu na sheria zinazolinda mali ya Waqfu.
>> >Kesi ya viwanja ni ya mahakama ya ardhi. Mwenye kiwanja
>> >alistahiki kwenda mahakama ya ardhi na kueleza kuwa kiwanja chake
>> > kimevamiwa.
>> >Kutumia polisi wa FFU kumkamata Sheikh Ponda kwa tuhuma za kuvamia
>> > kiwanja ni
>> >kitendo ambacho kimechochea vurugu. Matamshi ya Kamanda Kova
>> > yakumuhusisha
>> >Sheikh Ponda na uchomaji wa Makanisa jambo ambalo hakuhusika nalo na
>> > kutoa wito
>> >kwa wafuasi wa Sheikh Ponda kujisalimisha polisi ndilo lililochochea
>> > maandamano
>> >ya Ijumaa tarehe 19 Oktoba 2012.
>> >Jeshi la Wananchi ni la kulinda mipaka yetu siyo la
>> >kwenda kupiga raia wanaoandamana. Kitendo cha kuwaingiza barabarani
>> > wanajeshi
>> >kupambana na raia ni kitendo cha aibu na cha kusikitisha. Serikali iepuke
>> >kujenga uhasama kati ya Jeshi la Wananchi na raia.
>> >Kitendo cha kumnyima dhamana Sheikh Ponda na wenzake siyo
>> >cha haki.
>> >Kuinusuru nchi isingie katika mgogoro, Sheikh Ponda na wenzake wapewe
>> > dhamana. Hiyo
>> >ni haki yake yao ya msingi. Mwenye kiwanja apeleke malalamiko yake
>> > mahakama ya
>> >ardhi na kesi hiyo ya kiwanja ihamishiwe huko.
>> >Baada ya uchaguzi mkuu wa 2010, Rais Kikwete alizungumzia
>> >mgawanyiko wa kidini uliotokea wakati wa uchaguzi. Hata hivyo hajachukua
>> > hatua
>> >zozote za kuleta maelewano ya kujenga utamaduni wa kuvumiliana baina ya
>> >Watanzania wenye imani tofauti. CUF Chama Cha Wananchi kinatoa wito kwa
>> >Watanzania kuwa na mjadala wa kujenga mahusiano mazuri na kuvumiliana
>> > baina ya
>> >dini na madhehebu hapa nchini. Mijadala hii ifanyike katika ngazi ya
>> > kitaifa na
>> >katika maeneo ya wananchi na yahusishe viongozi wa dini wa taasisi zote,
>> > vyama
>> >vya siasa na vyama vya kijamii kwa lengo la kujenga na kuimarisha
>> > utamaduni wa
>> >kuvumiliana na kuheshimiana. Watanzania wote wajisikie kuwa ni raia wa
>> > daraja
>> >la kwanza katika nchi yao.
>> >
>> >Ibrahim Haruna Lipumba
>> >Mwenyekiti - CUF
>> >
>> >From: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
>> >To: Abridged Recipients <wanabidii@googlegroups.com>
>> >Sent: Friday, October 26, 2012 11:54 PM
>> >Subject: [wanabidii] Abridged summary of wanabidii@googlegroups.com - 98
>> > Messages in 42 Topics
>> >
>> >
>> > Today's Topic Summary
>> >Group: http://groups.google.com/group/wanabidii/topics
>> > * BITUMEN [1 Update]
>> > * Ponda Aachiwe Mara Moja – Lipumba - Mwanzo [15 Updates]
>> > * Breaking News:: Waziri Mkuu wa Zamani wa Italia, Berlusconi,
>> > Afungwa Miaka 4! - Mwanzo [4 Updates]
>> > * Invitation to IT security seminar, Dar Es Salaam 06/11/2012 [1
>> > Update]
>> > * Italy's Berlusconi sentenced to jail for tax fraud [1 Update]
>> > * SHURA YA MAIMAMU TANZANIA KAMATI KUU YA SIASA - UCHAGUZI MKUU
>> > 2010 [6 Updates]
>> > * Fw: Tanzania: Christians threatened by Islamisation [1 Update]
>> > * [Mabadiliko] Aibu kwa Tanzania: Hong Kong wakamata pembe ztu za
>> > ndovu [1 Update]
>> > * Fw: Tanzania: Christians threatened by Islamisation [1 Update]
>> > * Fw: UNBELIEVABLE AND WRITTEN BY A MUSLIM VERY INTERESTING [1
>> > Update]
>> > * WANABIDII BENKI - BAJETI [1 Update]
>> > * Fw: Tanzania: Christians threatened by Islamisation [1 Update]
>> > * MWISILAMU KAKOJOLEA KORAN NA KUMVISHA MBWA TASIBILI HUKO PEMBA
>> > [16 Updates]
>> > * Picha – Mwalimu VETA Morogoro Akutwa Amejinyonga:: Viewers
>> > Discretion Advised - Mwanzo [1 Update]
>> > * Accessing Theses on Tanzania Done in the UK [1 Update]
>> > * New Map Dividing Lake Nyasa/Malawi is Legal – Tanzania - Mwanzo
>> > [1 Update]
>> > * Kigali leading the way; The Clean Kenya Campaign [1 Update]
>> > * CHADEMA – ARUSHA: Nassari (Mb) anusurika kukung'utwa; MOSHI:
>> > Madiwani wakung'utana; SHINYANGA: Mwenyekiti achomwa mkuki - Mwanzo [4
>> > Updates]
>> > * Dk Shein atangaza vita na wavunjifu wa amani Zanzibar [2
>> > Updates]
>> > * ARAB SPRING RESURFACES IN BAHRAIN [1 Update]
>> > * Video : What Can Economists Know? [1 Update]
>> > * 1 Weird Spice That Cures Diabetes [1 Update]
>> > * ZANZIBAR POLICE COMMISSIONER SAYS: UAMSH
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment