Friday 12 October 2012

Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?


Bart
 
Ungekuwa mkweli ungeleza pia rushwa ya kimfumo iliyomo cdm.
wew ni shabiki, sitaki kulumbana
 
Asante kwa maoni yako
 
Mungu akubariki
 
Ngw'izukulushilinde
 
--- On Fri, 10/12/12, Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com> wrote:

From: Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, October 12, 2012, 10:58 AM

Dr. Kafumu,
 
Daima nimekuheshimu, ni kweli pia siamini na wala sijawahi kukufikiria kuwa wewe ni mla rushwa au mtoaji wa rushwa.
 
Lakini kuna tatizo kubwa ndani ya CCM ambapo sasa rushwa inatoka kutoka kwa mtu mmoja mmoja na kuwa rushwa ya kimfumo ndani ya chama. Sasa ndani ya CCM, siyo lazima wewe mwanachama au mgombea uhonge au upokee rushwa. Rushwa ndani ya CCM inaanza kuwa ni rushwa ya chama au makundi makubwa ndani ya chama. Wewe kama Kafumu hukuhonga Igunga lakini CCM kama chama kilihonga na wala sishangai mtu akisema kuwa pia CCM ilikilikula rushwa.
 
Watendaji, wapenzi, mashabiki wa CCM, na viongozi wa serikali waliokwenda Igunga kwa mgongo wa CCM, walitoa hongo, walitoa ahadi za hongo ili mgombea wake apite. Na kwangu mimi, tatizo la rushwa ya mtu mmoja mmoja ni afadhali kuliko rushwa ya chama kama taasisi. CCM sasa kimekuwa 'chama cha rushwa' kwa sababu rushwa inafanywa na watendaji, wasimamizi wa chama na makundi wakilishi. CCM pia imelalamikiwa maeneo mengine kuwalazimisha wafanyabiashara kukichangia, na kuwatisha pia kuwa wasipofanya hivyo biashara zao zitaathirika - hiyo nayo ni hongo. Kwa hiyo, CCM kama taasisi, kwa sasa imekuwa chama kinachotoa na kupokea rushwa. Ni ukweli pia kuwa kwa CCM kama chama kuonekana ni chama cha rushwa, ndicho kitu kinachoonekana kuwa kila anayeingia huko, hata kama hatoi au kupokea rushwa lakini atakuwa anafurahia rushwa.
 
Nakubaliana kabisa kuwa hakuna chama cha siasa au taasisi yeyote ambayo daima ina watu wasafi tu, kimatendo na kifikra, iwe ni hapa Tanzania au mahali pengine popote Duniani. Lakini ambacho huangaliwa zaidi ni je, taasisi inayohusika au chama kinaichukia rushwa? Kina mifumo ya kudhibiti rushwa? Kinawachukulia hatua za wazi na dhahiri, ambazo watu wakitazama na kuona wanaweza kusema kuwa, 'kweli CCM inachukia rushwa?'. Ndani ya CCM, kwa sisi tuliopo huku nje hatulioni hilo, na badala yake tunaona jinsi rushwa inavyohusudiwa na kupendwa ndani ya CCM. Ni bahati mbaya sana, Dr. Kafumo hata uwe msafi namna gani, si rahisi wewe mtu mmoja au wawili au hata 10 mnaweza kuubadili mfumo wa rushwa uliokubalika ndani ya CCM. Tena hilo lipo wazi sana, na unaona jinsi makundi makubwa ya rushwa yalivyo na nguvu ndani ya CCM.
 
Dr. Kafumu if you are really against corruption and you want to burn the 'corruption nest' you must be outside it, otherwise you will perish together with you host, the 'corruption nest namely CCM'.
 
Kuna watu wapo CCM, wapo upinzani na hata nje ya vyama vya siasa wanaoipenda sana nchi yao, hawa wanatakiwa kuungana na kujiuliza  kama kweli kuna uhakika kuwa ndani ya mfumo wa uongozi wa TANU/CCM tulioishi na kuongozwa nao kwa miaka 50, sasa una uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa kwa muda mfupi, japo umeshindwa kwa miaka mingi. Kama jibu ni hapana, basi Watanzania ni lazima tufanye 'overhall change' ambayo itasababisha kuleta mifumo mipya ya uongozi na usimamizi, maana mwisho wa yote tunachotaka ni kuondoka kwenye mfumo usio na matumaini. Kilicho muhimu si CCM wala CHADEMA bali ni taifa letu, japo tunajua kuwa matatizo mengi yamesababishwa na CCM. Tujenge mifumo mipya ambayo hatua ya kwanza iwe ni kuiondoa CCM ambayo mifumo yake ni kipingamizi kikubwa kuweza kuleta mabadiliko yenye tija kubwa kwenye maendeleo ya Taifa. CCM ni tatizo kubwa kwa Tanzania kwa sababu dhamira yake ya kuendelea kuwepo katika madaraka siyo kwa sababu ya kuleta mabadiliko bali kwaajili ya kuendelea kufuyarahia madaraka hata kama Watanzania wengi wataendelea kuteseka.
 
Ikiondoka CCM ni rahisi kujenga mifumo mipya itakayokilazimisha chama chochote kuondolewa kwenye madaraka kiurahisi ikiwa uongozi wake haukidhi matarajio ya Watanzania. Mfumo wa namna hiyo hatunao kwa sasa, ndiyo maana kuna baadhi yawatu wameendelea kuwepo katika madaraka japo wananchi walio wengi hawawataki.
 
Bart

From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, October 12, 2012 10:58 AM
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
Anael wa Nzega
 
Pole, siasa za vyama vyingi siyo utamaduni wa mwafrika, ni jinamizi kutoka kwa wakoloni mamboleo, tunavyolikumbatia kiasi cha kuwagawanya watu wetu ni hatari kwa amani na ustawi wa nchi yetu.
 
Huwa niashangaa ninapoona viongozi na vijana wenye imani kali ya cdm wanapomwita kila mwanaccm hata kama anaatoka kijiji cha Karitu (nzega) kuwa ni fisadi kwa vile ni mwanachama wa ccm ni kitu cha kutisha,
 
Ninapoona mara nyingi mama wa ccm kavaa kitenge chake cha ccm anatukanwa na kupigwa mawe na vijana wa cdm ninashangaa. Hali hiyo inajenga uhasama miongoni mwa wananchi wa kawaida na uhasama huo utakapokolea na wananchi wakaanza kubaguana kwa kufuata vyama hatutapona.
 
Wakati wote ninawaomba wenzangu ndani ya ccm na ndani ya cdm ninao marafiki, tujitahidi kuujenga mfumo huu bila chuki ili tuweze kubadilisha utawala wakati ukifika bila kumwaga damu. Chuki na matusi kwa sababu ya vyama havifai, vitalibomoa taifa letu...
 
Anael ubarikiwe
 
Nitakuletea kitabu nzega, Niarifu namba yako ya simu nitamtuma mtu akuletee
 
Kitabu ni katika llugha ya kingereza na bei yake ni sh 15,000 tu
 
Asante sana
 
Ngw'izukulushilinde --- On Thu, 10/11/12, Anael Macha <kowiri@hotmail.com> wrote:

From: Anael Macha <kowiri@hotmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, October 11, 2012, 8:07 PM

Dr. Kafumu,
Nitakinunua kitabu, tafadhali kifikishe nzega.
Unasema upinzani kuwa wanajenga chuki, sawa ila ccm unataka kujitenga nao. Wewe msafi ila wao walisema/walifanya. Ccm wanajenga nn? Kazi ipo, siasa zinawenyewe bana.
Ok, nashukuru na ubarikiwe nawe pia AM
On Oct 11, 2012, at 21:43, "Dr Peter D Kafumu" <kafumu@yahoo.com> wrote:
Bw. Nkumbaro.
 
 Nilishawahi kusema kwenye mabadiliko, cdm imejaa watu wema na pia mafisadi, kwa sababu hao ni binadamu wenye damu na nyama. Pia ccm imejaa wema na pia mafisadi kwani nao ni watu. Maandishi yako yanaonesha wewe sasa umegandamana na siasa za upinzani, zenye chuki na hasira iliyokithiri na ushabiki unaoona kuwa CDM malaika CCM mashetani. 
 
Katka uchaguzi mdogo wa Igunga mimi mgombea sikutoa rushwa yoyote, sikutukana mtu yoyote na sikukiuka kanuni zozote za uchaguzi. Hukumu imetolewa dhidi yangu kwa tuhuma siyo za rushwa bali za maneno ya watu wengine siyo mimi. Lakini pia kulikuwa na tuhuma zilizotolewa na washitaki kuhusu kutolewa kwa rushwa na baadhi ya wanccm (siyo mimi) lakini jaji alizikataa akasema hazina ushahidi.
 
Kwa maoni ya jaji; maneno ya wengine yalitosha yeye kuhukumu alivyohukumu. Maneno yako yamejaa ushabiki na hasira dhidi ya ccm na wanaccm. Huo siyo utamaduni wa ushindani wa vyama vingi tunaotarajia kuujenga Tanzania, utamaduni wa kuita watu wote wa ccm au chama kisicho chako kuwa waovu na wazuri wote wako cdm.  Sipendi kulumbana nawe kwa sababu sitaki kujenga chuki dhidi ya mtu yoyote.
 
Nakushukuru kwa mchango wako.
 
Mungu akubariki
 
Ngw'izukulushilinde --- On Thu, 10/11/12, John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com> wrote:

From: John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, October 11, 2012, 2:21 PM

Dear Kaka Kafumu,
Kaka  HK anaandika kuwa, hakukuwa na tuhuma za rushwa kwako wala kiongozi yoyote wa CCM ama serikali aliyetuhumiwa na kukutwa na hatia ya kutoa rushwa kule Igunga.
Definitely Kaka HK hajui nini rushwa. Kwake yeye labda ukikutwa unatoa pesa ndio unaweza kutuhumiwa na hatia ya rushwa. 
Rushwa, Kaka Kafumu, is any dishonest act committed in return for personal gain. Hata yule aliesema kuwa daraja halitomalizwa Igunga kama CCM haitoshinda – nae pia alitenda kitendo cha rushwa kwa upande wako.
Mahkama Kuu imegundua kuwa dishonest acts (yaani rushwa) zilitumika na ndio maana ikapinduwa ushindi wako.
Kaka HK nae anaeleza kuwa yumo katika kuandika kitabu chake pia. Hili ni jambo zuri sana na ninampongeza kama ninavyokupongeza wewe, kwani 'vizazi na vizazi vitapata kusoma na kujifunza',
lakini sijui kitabu chake kitakuwa kuhusu nini – most probably his book will be titled - How fast a Cowboy draws his  gun on his enemy.
Hapa netini, mimi nilikuwa katika watu wa mwanzo kukupa hongera baada ya ule ushindi wako na nilikuwa peke yangu nilie-withdraw hongera zangu baada ya kufahamu nini kilitokea Igunga na kuwa kumbe ulishinda kwa mazonge na rushwa. 
Ninastaajabu, vipi mtu anaandika kitabu kuhusu ubaya na extent ya rushwa nchini na huku anakuenda kugombania ubunge kupitia CCM na sio Chadema. Are we serious? The only CCM member ambae alikuwa free of rushwa kwa bahati mbaya amefariki tokea 1999. Sidhani kama yupo mwengine. Mwengine ambae tungelimdhania juzi aliadhirika Kisutu kuenda kudai kodi zake alizotapeliwa. Sisi tulimpa usukani ndugu yetu kumbe mwenzetu alikuwa busy kujenga nyumba za kukodisha katika kila corner ya DSM. Kama ni mimi nisingelikuenda Kisutu kujiadhirisha na ningelimuachia tu huyo mwizi hicho alichochukuwa – kama vile na yeye amechukua chake mapema kutoka kwangu!

http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/mzee-sio-muachie-tu-raia-wako.html

Anyway, najua mpo wengi hapa ukumbini (Tony, HK, etc) na kwahivyo bora nikimbie kwa haraka!

//Nkumba.
 
From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, October 10, 2012 3:55:48 PM
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
Waungwana
 
Nawaomba mnunue kitabu kwanza msome, na kufanya "a book review" na mjadili na kutoa maoni yenu. Kitabu ni cha kingereza mwandishi wa gazeti kajaribu kutafsiri - ni vizuri kusoma mwenyewe. Tuwasiliane mpate kitabu. Kinauzwa Shs 15,000 tu. Karibuni..
 
Ng'wizukulushilinde --- On Wed, 10/10/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, October 10, 2012, 5:05 PM

Mimi siyo Kafumu na wala sijabahatika kusoma kitabu chake lakini kwa kuiangalia sehemu uliyonukuu "...kwamba kuishi kwa uaminifu katika jamii iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki aliyejeruhiwa baharini" unaweza kutoa tafakari.  Maneno hayo ni ya kiswahili yanayoweza kueleweka kwa wasomaji japo mwandishi anaweza kuwa na tafsiri zaidi. Kwa vile katuandikia wasomaji ili tusome kitabu chake na bila shaka kuelewa ujumbe anaokusudia tuupate. Binafsi namuelewa kwamba si rahisi kuuona uaminifu wa mtu au watu waaminifu wachache wanaoishi na jamii kubwa isiyokuwa na uaminifu (wala rushwa). Kwa kufafanua anachokimaanisha akafananisha mchango wa mtu mwaminifu na tone la damu ya samaki baharini. Kwa ufupi kama mada inahusu rushwa na tukiamua kujielekeza katika tukio lililompata mwandishi wa kitabu hicho tunaweza kupata maana zaidi. Yeye Kafumu amevuliwa ubunge kwa sababu ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi yumkini ikiwemo rushwa. Maana pana zaidi tunayoweza kupata ni kama waziri mstaafu (Sumaye) alivyosema juma lililopita kwamba rushwa inanuka katika chaguzi za CCM. Inawezekana Kafumu alianza kudaiwa rushwa tangu kuteuliwa na chama chake hadi kwenye uchaguzi wenyewe. Hivyo anavyosema mtu mwaminifu hawezi kutokea kwenye kundi la wala rushwa maana hawatampitisha na hivyo hawezi kuonekana au kueleweka kwa namna yoyote. Lakini pia Kafumu anaweza kuwa na maana pana zaidi ya kwamba watanzania kwa ujumla wetu tulikofikia ni mwendo wa kutoa chochote ili uchaguliwe "Toa kula nikupe kura" Kwamba nchi imekuwa ya watu wasiokuwa waaminifu na hivyo mchango wa mtu mwaminifu hauwezi kuonekana kwa namna yoyote. Nafikiri Kafumu hana mpango wa kuomba radhi bali ameamua kuanika alichokiona ndani na nje ya CCM Naamini Kafumu mwenyewe atatueleza nini hasa alichokimaanisha ili tuweze kununua na kukisoma kitabu chake kwa uelewa zaidi 2012/10/10 Said Issa <saidissa100@yahoo.com>: > Hi All, > Nd. Peter Kafumu ameandika kitabu kuhusu rushwa nchini kinachoitwa "Sauti > Inayolia-Tafakuri Binafsi" (a Crying Voice-personal reflections). > Maelezo yake ya mbio mbio yananipa fikra kama huyu Mhe anatubia labda kwa > kushinda kule Igunga kwa kupitia mambo ya rushwa na sasa anaomba radhi. > Anyway, kila mtu atafahamu kivyake, lakini mimi ninamuona kama anaomba > radhi, hasa pale alipoandika kuwa...."...kwamba kuishi kwa uaminifu katika > jamii > iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki aliyejeruhiwa > baharini". > > Najua Mhe Kafumu yupo hapa ukumbini. Ningelimuomba atupe briefing ya kitabu > chake ambacho kidogo hakifahamiki - yaani haeleweki kama anai-expose > rushwa au anaomba radhi kwa rushwa iliyotendeka Igunga mpaka akashinda? > > > http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/peter-kafumu-alishinda-kutokana-na.html > > -- > Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ > Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ > Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ > > Kujiondoa Tuma Email kwenda > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha > ukishatuma > > Disclaimer: > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal > consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be > presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to > this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. > > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment