Tuesday 2 October 2012

RE: [wanabidii] Maandalizi Ya Maonyesho Ya Asali Yamekamilika

Bwana Matiko
Nawapongeza wote kwa hatua hiyo nafikiri hii itawafungua macho watanzania wengi kufahamu kwamba shughuli ya ufugaji nyuki ni sawa na shimo
la dhahabu ambalo wengi hawajagundua. Nitajitahidi kuhudhuria.

Ruzika N. Muheto MSc, BSc(Hons)
Executive Director
EarthCare Consulting Co.
P.O Box 79467
Mob. +255754692282,
Dar Es Salaam
Email: rmuheto@hotmail.co.uk or rmuheto@gmail.com
Formerly worked initially as Director of Natural Resources and later Founding Director of the Directorate of 
Environmental Planning and Research at the National Environment Managemnt Council, NEMC, TANZANIA.
NEMC IS THE TANZANIA ENVIRONMENTAL REGULATOR WITH ALSO ADVISORY ROLES TO GOVERNMENT AND SOCIETY IN GENERAL.  




 

Date: Tue, 2 Oct 2012 12:35:43 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Maandalizi Ya Maonyesho Ya Asali Yamekamilika
From: samchaz307@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

MZEE JOJI MATIKU BADO NASUBIRIA SIMU YAKO KUHUSU WATU  WATAKAOKUJA KWENYE KIPINDI CHA HOT MIX MZEE,, NI SAMSON CHARLES HAPA

2012/10/1 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Maandalizi ya MAONYESHO YA ASALI YA DAR ES SALAAM (DAR ES SALAAM HONEY EXHIBITION) ambayo yatafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) Dar es Salaam tangu tarehe 3 hadi 7 Oktoba 2012 yamekamilika. Wananchi wanakaribishwa kuhudhuria maonyesho hayo ambayo hayatakuwa na kiingilio. 

Katika maonyesho hayo watu wataelimika kuhusu manufaa yatokanayo na asali, pia watapata utaalam wa kufuga nyuki na wataonja na kununua asali bora kwa bei nafuu. Kaulimbiu ya maonyesho hayo ambayo ni ya kitaifa ni ASALI KWA AFYA NA USTAWI (HONEY FOR HEALTH AND PROSPERITY). Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na wadau wengine wa Sekta ya Ufugaji Nyuki. Lengo kuu la maonesho ni kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ya nyuki. Tarehe 3 Oktoba ni siku iliyotengwa maalum kwa ajili ya kufanyika Kongamano la Ufugaji Nyuki. Hivyo wafugaji nyuki, wataalam na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo wanakaribishwa kuhudhuria kungamano hilo ambalo litafanyika katika ukumbi wa J. M. Kikwete ulioko kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere . 
 

Ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo utafanyika tarehe 5 Oktoba 2012 ambapo Mgeni Rasmi anategemewa kuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb). Waonyeshaji waliothibitisha kushiriki ni Halmashauri za Wilaya zote, kampuni zinazonunua asali, watengenezaji wa mizinga na vifaa vingine vya kisasa vya ufugaji nyuki, na watengenezaji wa bidhaa zinaotumia asali na nta kama malighafi. Inategemewa kuwa katika maonyesho hayo waonyeshaji watajitangaza ili waweze kupata wanunuzi wa asali na mazao mengine ya nyuki. 
 

Pia wanunuzi wa mazao ya nyuki watapata fursa ya kuwafahamu wafugaji. Aidha inategemewa kuwa utaundwa mtandao ambao utawaunganisha wazalishaji, wafanyabiashara, wataalam na wadau wa sekta ya nyuki.
 
 George Matiko
 MSEMAJI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII 
30 Septemba 2012

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment