Monday 8 October 2012

Re: [wanabidii] MAALIM SEIF ASISITIZA JUU YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR!

Mimi ni mmjoa ya watu wanaoafiki kura ya maoni kuhusu muungano ipigwe visiwani na bara lakini baada ya wananchi kuelimishwa sana.Na kisha ionekane wazi wazi kama muungano unahitajika au la?na kama unahitajika faida ya pande zote mbili ni nini?ni nini kila nchi inachopoteza na nini inachopata.Maana kama ilivyo katika urafiki huwezi ukapata bila kupoteza ka dhalika na katika muungano pia.Kuna umuhimu wa ku analyse ni nini bara inachopata kwa kuwepo katika muungano na ni nini inachopoteza,hali kadhalika na Zanzibar pia. And then,kila upande upime faida na hasara na kufanya maamuzi ambayo ni irreversible.  Kwa mtazamo wangu nahisi Wanzanzibar hawaelewi wanachopata katika muungano,bali wanachojua ni kile tu wanachopoteza. Suluhisho la jambo hili ni kuwaelimisha watu kwani pia wengi wao wamepotozwa. Mie sidhani na wala hainingii akilini hata kidogo mtu akidhani kuwa akiwa na passport ya Zanzibar ana heshimika zaidi katika jamii ya kimataifa kuliko akiwa na passport ya Tanzania.Kwa lipi?

Let us say leo hii tunapata sarafu moja ya East African shillingi halafu Mtanzania akaona fahari sana kubakia na Tanzanian shilling kuliko kuwa na East African shilling. Ukimuona mtu wa jinsi hiyo,hakuna sababu ya kumcheka,isipokuwa ujue kuwa pengine  rangi na shape ya pesa ni muhimu sana kwake kuliko mambo mengine.
Ngupula Godfrey


From: Bakari Maligwa Mohamed <maligwa1968@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Sent: Monday, 8 October 2012, 10:29
Subject: Re: [wanabidii] MAALIM SEIF ASISITIZA JUU YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR!

..Alaaaaa; kumbe Mobhare ni DIKTETA! Nilidhani mwanzo Afrika ina madikteta "wakongwe" na wa zamani enzi za akina Mobutu Sese Seko...kumbe hata sisi kizazi cha miaka ya 1960 tuna mawazo ya kiimla [?]....kwani "muungano" si watu? Au, nchi ziliungana zenyewe? Kama jibu la kwanza ni NDIO [watu waliungana]..sasa wanataka kutengana; kuna tatizo?
 
Mobhare, Wazanzibari si ndio watakaoamua; au? Kwani mwaka 2010 walipobadilisha Katiba ya Zanzibar, 1984 [RE 2010] na kuweka Ibara inayotamka kwamba "Zanziar ni nchi' mlidhani wanafanya "mzaha" na siasa? Nadhani Wazanzibari tutawasikia...na watasema sasa; kazi kwetu Watanganyika ambao kwa kuamini jina ziri la TANZANIA na tutajiita Watanzania na kusahau Utanganyika tutaweweseka na Zanzibar...muda ukifika KURA YA MAONI itaamua baina ya wao na sisi...HAYA NI MAWAZO HURU!
 
Mobhare, kwa nini wasiachwe Wazanzibari kama wanavyosema "WAPUMUE NA ZANZIBAR YAO" NA SIYE WATANGANYIKA TUANGALIE MUSTAKABALI WETU? Hivi; muungano ni LAZIMA isiyoepukika? Au kuna kilichofichwa NYUMA ya PAZIA? Hii lazima isiyoepukika ndio inayowafanya baadhi ya watu wadhani kwamba MUUNGANO NI WA KULAZIMISHA...na huu ni UDIKTETA WA CHAMA CHA MAPINDUZI ambao kwao mabadiliko hayawezi kutokea hadi "KWA MBINDE."

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, October 8, 2012 3:08 AM
Subject: RE: [wanabidii] MAALIM SEIF ASISITIZA JUU YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR!

Wacha apige kelele mpaka atokwe povu, Muungano hauvunjwi hapa!
 
Date: Sun, 7 Oct 2012 15:36:04 -0700
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: [wanabidii] MAALIM SEIF ASISITIZA JUU YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR!
To: wanabidii@googlegroups.com

"Mimi sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na 
Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba. Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na muhuri na wimbo wa taifa, 
hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? 
Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale. Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, 
nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu. Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje".

http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/seif-asema-tunataka-dola-huru.html

--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment