Tuesday 23 October 2012

RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;

Kabalika,
Nilikuwa mapumziko ya chai/kahawa nikawa nasoma huu upupu. Nitaujibu kwa vielelezo vyenye vyanzo rasmi. Huyu mtu ni mzushi mwenye ajenda ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kushindwa kuibani. Ni hili genge linalokua siku hizi ambalo siku si nyingi litatumbukiza kwenye matatizo makubwa.
Matinyi.
 

Date: Tue, 23 Oct 2012 15:47:50 +0100
From: rotts76@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
To: wanabidii@googlegroups.com

Mchambuzi hakuonyesha source ya baadhi ya information ili wengine wajiridhishe na ukweli wa alichoandika. Vile vile hajazungumzia wimbi la upendeleo wa watu fulani kwenda kusoma India, Ukraine, Uturuki, Italia huku wakiwa watokea kwenye utamaduni wa aina moja na kuwaacha watu wa tamaduni zingine steanded. Hajaongelea kinachoendelea sasa kuhusu mambo ya upendeleo kwa watu wa utamaduni mmoja. Uchambuzi wake haujakamilika aandike na mapungufu ya wengine wote waliopo na waliopita wakirithi kiti hicho. Mwisho nasema naonya tu kuwa tukihukumu watu cheaply hivi bila kufanya fare and thorough analysis tutaishia pabaya.


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>;
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
Sent: Tue, Oct 23, 2012 12:01:25 PM

Kama huyu mwandishi amesema kwamba suala la Amin lingewezwa kumalizwa kwa mazungumzo, na nimeona kuna vijineno vya aina fulani hivi amevichomeka, nadhani ni kupoteza muda kuisoma, labda kama lengo litakuwa kuokoa upotoshaji. Na kwa lugha yake ya sentensi chache niliziona, huyu muungwana anajulikana na yumo humu humu jamvini. Ni matatizo yale yale tu. Nyerere alikuwa binadamu na kiongozi makini aliyeipenda nchi yake; na katika utendaji wake kuna mambo alikosea lakini hatupaswi kuchambua uongozi wake kwa uongo, udini, n.k.
Matinyi.
 

Date: Tue, 23 Oct 2012 12:51:16 +0100
From: ngupula@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
To: wanabidii@googlegroups.com

Binafsi ingawa namfagilia sana Mwalimu kama mwanasiasa safi,lakini huwa nakubali kuwa alikuwa na mapugufu mengi pia kama binadamu.Ni hotuba nzuri ingawa msimuliaji hakuwa na balance katika kuelezea haswa balance ya mambo fulanifulani. Mfano,anaposema vita ya Uganda ingeweza kuisha kwa mazungumzo...sio kweli. Kwa tuliokuwepo kwa wakati huo Nyerere alitoa nafasi kubwa kwa OAU na UN yamkini hata ya kumlaani AMIN na hakuna taifa lililofanya hivyo. Sasa,unawezaje kusubiri mazungumzona mtu kicha kama Amin asiye na utu na huku anaua watu wako.Diplomasia ni nzuri but ina wakati wake.Ukiiikosea unaonekana tu ni mtu usiye na maamuzi.Kwa hilo hakukosea,sio kweli.

Na kuhusu utaifishaji,anaweza akalaumika kwa upande fulani,lakini kwa upande mwingine halaumiki. Kwa mfano,alivyotaifisha mashule ili kufanya watu wote wasome kwa usawa...

Hayo ni baadhi tu...

Godfrey








From: Ben Nyitambe <matikubn@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, 23 October 2012, 9:05
Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;

Asante sana kaka!

On 10/23/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
> Mwandishi wa makala kaibua maswali muhimu ambayo majibu yake ni juu
> yetu kutafakari. Siamini kama kuna mtu anayefikiri kwamba Nyerere
> hakufanya kosa ata moja. Yeye mwenyewe (Nyerere) alikiri kwa kinywa
> chake kwamba yapo makosa mengi yaliyofanywa na serikali yake lakini
> pia yapo mazuri aliyoyafanya. Wakati akipigania haki za watanzania,
> yapo mambo ambayo siamini kama yalikuwa na baraka za umma bali matakwa
> yake mwenyewe hasa hasa mambo yaliyohusu mahusiano yetu na nchi za
> nje.
>
> Sera zake za ndani zilididimiza maendeleo ya maeneo fulani huku
> akiyainua mengine bila shaka kwa nia nzuri, bila kuwa dikteita kwa
> wakati huo tusingekuwa na Tanzania tunayoiona leo. Sitegemei kama
> wamissionari na mabepari wenye mashamba makubwa walifurahishwa na
> kitendo cha Nyerere kutaifisha mali zao. Kulikuwa na machifu ambao
> uhusiano wao na watu wengine ni wa bwana na mtumwa hawa kwa vyovyote
> vile lazima wamlaani Nyerere kwa vile walikuwa ni wanyonyaji na
> wangependa kuendelea kufanya hivyo. Yapo mambo mengi tu ambayo
> tunaweza kuyaangalia kwa mitizamo tofauti kutegemea na nafasi
> tulizokuwa nazo au tulizo nazo kwa sasa.
>
> Kwa mtizamo wangu namuona Nyerere kama mtu aliyekuwa na mapungufu ya
> kawaida kama binadamu lakini kwa ujumla namuona kama kiongozi safi wa
> wakati huo katika mazingira ya wakati ule.
> 2012/10/23  <hkigwangalla@gmail.com>:
>> Duh! Makala nzuri, imeandikwa kwa umahiri japokuwa wengi wetu
>> hatutoikubali
>> kwa sababu tunampenda Baba wa Taifa na tunaamini ni mtu aliyekuwa na nia
>> nzuri na Taifa hili na nia hiyo haikujificha hata siku moja! Kuanguka kwa
>> itikadi zake ama kutotekelezeka kwa mikakati yake haimaanishi he was a
>> bad
>> leader, wengine tunaona better him he tried...
>> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
>> ________________________________
>> From: amour chamani <abachamani@yahoo.com>
>> Sender: wanabidii@googlegroups.com
>> Date: Mon, 22 Oct 2012 20:40:41 -0700 (PDT)
>> To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
>> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
>> Subject: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>>
>>
>> Mwandishi Wetu|RAIA MWEMA,Toleo la 263 |17 Oct 2012
>>
>> WATAFITI wengi wamejaribu kuelezea kwa kina Julius Nyerere alikuwa
>> binadamu
>> wa aina gani, lakini baadhi yao wanaamini alikuwa ni mtu ambaye ni vigumu
>> kumuelezea kinagaubaga taswira yake na mwenendo wake mzima kwa ujumla.
>> Katika makala hii tutajaribu kumchambua angalau tupate ufunuo kuhusu
>> hilo.
>> Katika zama zake kileleni Mwalimu, kama wafuasi wake walivyopenda
>> kumwita,
>> msomi huyu mahiri wa Afrika, alinyenyekewa mno kwa heshima na Watanzania
>> wengi huku wengi pia wakimnanga kwa staili ya utawala wake ambao ulikuwa
>> wa
>> kibabe na wenye harufu za kidikteta. Wengine walimpa jina 'dikteta
>> mrahimu'.
>>
>> Ukweli ni kuwa Watanzania mara kwa mara wamekuwa wakishindwa kutafsiri
>> yale
>> ambayo Mwalimu aliyasimamia, misimamo yake ya sera zenye misingi ya utu
>> wa
>> binadamu na azma zake za kifilosofia. Kuyajadili mafanikio yake na
>> vilevile
>> makosa yake. Tumeshindwa kumsoma bila ya ushabiki, sijui ni kwa sababu za
>> uvivu au ni woga. Kwa hakika, kwa yeyote atakaye kupanda ngazi ama ya
>> kijamii au ya kisiasa, basi busara ya kawaida tu itamlazimu akwepe kutaja
>> makosa ya Nyerere hata kama yanafahamika kwa wote. Hii imekuwa kama hulka
>> ya
>> Kitanzania.
>>
>> Nyerere hayuko nasi leo na hii ni sababu nzuri ya kutaka kukumbuka kuwa
>> hapo
>> zamani alipata kuwapo mwanasiasa aliyeongoza harakati za kutafuta uhuru
>> wa
>> nchi hii; akabahatika kuaminiwa na watu wake; akajaribu kufanya yale
>> aliyoamini kuwa ni ya manufaa kwa nchi yake; akalazimisha majaribio tata
>> ya
>> fikra na sera zake kwa wananchi wake aliowapumbaza, kwa muda wa miongo
>> miwili na nusu na tofauti na watawala wengine wa Kiafrika, hakustaafu kwa
>> kupinduliwa. Lakini mwishowe, kwa msaada wa masharti magumu ya kiuchumi
>> ya
>> Benki ya Dunia (Bretton Wood Institutions) aliachia ngazi, mwaka 1985.
>>
>> Hivi Nyerere alikuwa ni nani? Je, alikuwa ni mwana wa chifu mmoja
>> asiyejulikana kutoka madongokuinama aliyeamua kuishi maisha ya mtu wa
>> kawaida? Je, alikuwa mkristo mzuri aliyevaa baraghashia ya kiislamu kama
>> vazi lake la kawaida tu? Au, ni mwalimu msomi aliyeacha kufundisha ili
>> ajiunge na siasa? Au, 'Mkomunisti' aendaye kanisani kila leo na kupata
>> sakramenti? Ama kiongozi aliyejizatiti kuwafikiria wananchi wake na
>> ukombozi
>> wa Afrika tu? Yawezekana alikuwa muunganishaji aliyetuachia Muungano
>> wenye
>> nyufa tele? Au alikuwa mmajumui wa Afrika aliyekataa katakata kuanzishwa
>> kwa
>> Serikali moja ya Bara la Afrika. Haswa, huyu Nyerere alikuwa mtu wa aina
>> gani?
>>
>> Mwalimu alikuwa mtu mwenye familia njema na alijaaliwa watoto kadhaa.
>> Ukweli
>> sote tunaujua kuwa, familia yake iliishi maisha ya kawaida bila ya
>> kuonyesha
>> kiburi, fahari au kuwanyanyasa watu wa kawaida. Ukitambua namna Mwalimu
>> akiogopwa, hata mara moja hakufikiria wala kujaribu kuendeleza 'ufalme'
>> kwa
>> kumtayarisha mwanae au nduguye amrithi. Pengine angetaka, asingekuwapo wa
>> kupinga! Lakini alipinga mchezo huo wa 'ndugunaizesheni'. Na kwa hilo
>> anastahili heko. Hata hivyo, Mwalimu aliweza kufanya mengi ambayo hakuna
>> aliyediriki kumzuia. Alifuta mfumo wa uchifu, alifuta serikali za mitaa,
>> ushirika, vyama vya wafanyakazi na hata vyama vya siasa vya upinzani.
>> Alitaifisha mali binafsi za watu, shule, hospitali na kila kilichomkalia
>> sawa. Aliendesha uanzishwaji wa vijiji vya Ujamaa bila ya mpangilio wala
>> ubinadamu, alisweka ndani wapinzani wake, alitekeleza sheria kadhaa
>> kandamizi na kupiga marufuku maandamano na migomo. Sote tunakumbuka zama
>> zile mambo haya yalikuwa ya kawaida kabisa. Mwalimu alifanya atakavyo na
>> hakuna aliyesema fyoko!
>>
>> Hadharani, Nyerere alijitahidi kuwaunganisha Watanzania kwa dhati kabisa.
>> Watanzania kwa wakati ule walikuwa wachache mno kulinganisha na ukubwa wa
>> nchi. Msimamo wake huu wa umoja ulijidhihirisha zaidi kwa namna
>> alivyokuwa
>> akiulinda na kuutetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano ambao
>> uliundwa chapchap, kwa kufumba na kufumbua macho na ukawa, kufuatia
>> mapinduzi yaliyoendeshwa na genge dogo la watu pasipo na silaha za moto
>> wala
>> mafunzo ya kijeshi kumpindua Sultan Jamshid.
>> Miongo mitano imepita sasa na baada ya nyaraka za siri za Serikali ya
>> Marekani kuwekwa bayana, wachambuzi wamekuwa wakihoji sababu za kweli
>> ambazo
>> ndizo chanzo cha Muungano huo kuundwa.
>>
>> Pamoja na nia njema ya Nyerere, ukweli ni kuwa Muungano huo uliasisiwa na
>> Serikali za Marekani na Uingereza kwa nia ya kuzuia uwezekano wowote wa
>> 'wakomunisti' kuteka mapinduzi ya Zanzibar. Hili lingewezekana kwa sababu
>> Serikali ya ASP ilikuwa dhaifu mno na Abdulrahman Babu, kiongozi wa Umma
>> Party na mkomunisti aliyekubuhu, aliwanyima raha Wamarekani, Waingereza
>> na
>> Nyerere. Kwa hiyo, Nyerere akalazimishwa na Wamarekani na Waingereza
>> kupeleka askari kanzu 300 wa Tanganyika kwenda Zanzibar ili wamlinde
>> Karume
>> na Serikali yake, hii ikasaidia muda mfupi baadaye kumtisha Karume
>> akubali
>> haraka kutia sahihi mkataba wa Muungano.
>>
>> Lakini ni vyema pia kukumbuka kuwa Nyerere mwenyewe alikumbana na zahma
>> adhimu kama miezi miwili kabla Dar es Salaam kutokana na uasi wa kijeshi
>> na
>> yeye kuingia mafichoni kwa siku kadhaa. Akawaomba Waingereza wakaleta
>> manowari na majeshi na kufanikiwa kumrejesha madarakani. Kwa Mwalimu,
>> tukio
>> la yeye kuwaomba wakoloni msaada lilimuaibisha bila kifani. Kwa hiyo
>> haikuwa
>> vigumu 'kumminya' Nyerere ili afanye kazi yao ya 'Muungano' baada ya yeye
>> kufaidi fadhila za Waingereza. Waswahili wana msemo, 'Fadhila huzaa
>> fadhila'. Hata hivyo, Mwalimu katika miaka yote hii, amekuwa akijitetea
>> kuwa
>> Muungano umesababishwa na sababu za udugu baina ya nchi hizi mbili na
>> kuwa
>> hii ni hatua ya mwanzo ya kufikia 'Muungano wa Afrika' nzima.
>>
>> Watanzania wanakumbuka fika kuwa kabla na baada tu ya Uhuru wa
>> Tanganyika,
>> taasisi zetu kama vile kampuni za reli, simu, posta, Idara ya Ujenzi na
>> nyinginezo ziliweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.
>> Mathalan,
>> reli waliweza kuendesha ratiba ya kuaminika ya safari za treni bila ya
>> hitilafu. Barabara ya Dar es Salaam sehemu za Magomeni, Ilala, Kinondoni
>> na
>> Temeke zilikuwa ni za lami. Wazee wetu wanafahamu, hizo ndizo siku za
>> kuzikumbuka kwa tabasamu.
>>
>> Ilipofika mwaka 1975, miundombinu takriban yote ilikuwa nyang'anyang'a.
>> Hali
>> ilifikia pabaya. Nchi ilikuwa inaporomoka vibaya chini ya usimamizi wa
>> Nyerere. Taratibu za kiutawala za Serikali Kuu zilidorora na nidhamu
>> ilishuka vibaya. Miaka ya mwanzo ya themanini mashirika ya umma karibuni
>> 400, karibuni yote mali ya watu binafsi iliyotaifishwa, yalikuwa
>> yanakaribia
>> kufilisika kutokana na ubadhirifu na wizi usiomithilika. Kwa Nyerere,
>> ilikuwa dhahiri kuwa 'majaribio' yake yalikuwa yamefeli ile mbaya.
>>
>> Utaifishaji wa mali za watu binafsi uliofuatia Azimio la Arusha mwaka
>> 1967
>> uliendeshwa vibaya kiasi cha kufikia hatua hata ya kutaifisha vijiduka
>> vidogo vya rejareja vijijini kutoka kwa watu binafsi. Lakini Nyerere
>> hakusita na zoezi liliendelea. Katika miaka ya kati ya sabini, Ujamaa
>> ulikuwa unafaidi ruzuku na misaada mingi kutoka nchi za Scandinavia na
>> China
>> na ndiyo maana Mwalimu aliweza kuwapa wananchi wake elimu bure, huduma za
>> afya bure na vingine vingi. Watanzania wakalemaa. Mwalimu naye akawa
>> shujaa
>> kwa watu wake angalau kwa muda mfupi. Haikupita muda Shirikisho la Afrika
>> Mashariki likavunjika mwaka 1977 na kuathiri uchumi kwa kiasi kikubwa.
>>
>> Punde si punde, Vita ya Kagera nayo ikaleta maafa makubwa kwa uchumi wa
>> taifa. Ugumu wa maisha ukakaba taifa. Wachunguzi hata hivyo wanahoji sasa
>> hivi kwa nini Mwalimu hakujaribu kutatua mgogoro ule kwa mazungumzo? Hivi
>> kweli ilikuwa lazima tupigane vita wakati Umoja wa Afrika (OAU) ulikuwa
>> ukijaribu kusuluhisha? Hivi inawezekana, Mwalimu angetangaza vita
>> kumng'oa
>> Idi Amin kama sahibu wake wa karibu Milton Obote asingekuwa anapanga
>> kunyakua madaraka nchini Uganda? Obote aliweka kambi za kijeshi hapa
>> nchini
>> kwa miaka mingi.
>>
>> Hatimaye Obote alifanikiwa kurudi madarakani angalau kwa muda mfupi na
>> kupinduliwa tena kwa sababu ya ubadhirifu mkubwa wa mali za umma na
>> kurudi
>> uhamishoni Zambia mpaka alipokufa miaka michache iliyopita. Vyovyote
>> utakavyoangalia, leo hii bado nchi hii inajaribu kujiponya kutokana na
>> athari za kiuchumi ambazo vita ile ilitusababishia. Urafiki wa Nyerere na
>> Obote uligeuka tatizo letu la kitaifa.
>>
>> Ilipofika hapo, uchumi ukiyumba na sera yake ya Ujamaa ikiwa inayoyoma,
>> Nyerere sasa akawa amefikia ukomo wa safari yake. Amekwama! Manyang'au wa
>> Benki ya Dunia na mafisi wa IMF wakafurahia kutokana na uhaba mkubwa wa
>> chakula nchini. Wakasema, sasa umefikia wakati wa kumkomesha Nyerere
>> kisawasawa. Naam, wakafanya ilivyotarajiwa, wakamwekea Mwalimu masharti
>> magumu ya mikopo ya kunusuru uchumi wa nchi yake.
>>
>> Kama mbinu ya kuwaliwaza wananchi wake Mwalimu akamruhusu Waziri Mkuu
>> wake,
>> Edward Sokoine (sasa marehemu) awashughulikie 'wahujumu uchumi'.
>> Akataifisha
>> mali na kuwafunga matajiri. Akaanzisha Mahakama zisizo na uhalali wowote
>> kuwahukumu. Mfano, mtu mmoja alifungwa miaka kadhaa kwa kuwa na
>> televisheni.
>> Na mwingine alienda jela kwa kuwa na kopo la dawa za tetracycline. Chini
>> ya
>> usimamizi wa Mwalimu, maafa makubwa yaliwapata wananchi wa kawaida na
>> wakati
>> mwingine yalisababisha vifo.
>> Kampeni hii ya uhujumu uchumi ya mwaka 1983 ilifananishwa na ujio mpya wa
>> Azimio la Arusha la mwaka 1967. Utaifishaji huu holela uliojaa dhuluma
>> ulithibitisha kuwa sera za Mwalimu zimeshindwa katika kuitawala nchi kwa
>> ufanisi. Ukweli huu ulijidhihirisha zaidi katika siku zake za mwisho
>> kabla
>> ya kung'atuka. Ili kunusuru uchumi ilibidi akubali kushusha thamani ya
>> sarafu ya nchi kutokana na masharti ya IMF.
>>
>> Kung'atuka kwa Mwalimu ikawa ni suala la muda tu. Ilipofika mwaka 1985,
>> aling'atuka huku akiiacha nchi kwenye uchumi mbaya kuliko wakati wowote
>> katika historia ya nchi hii. Hata hivyo, harakati kubwa zikafanywa na
>> propaganda za kisiasa zikatekelezwa ili kumpa kisingizio cha muonekano
>> kuwa,
>> Mwalimu aliamua kustaafu urais kwa hiari yake. Katika historia, ni vyema
>> tukakumbuka, moja ya nyakati ambazo Nyerere alijikwaa na kuvurunda
>> ilikuwa
>> pale alipounga mkono kujitenga kwa Jimbo la Biafra kule nchini Nigeria.
>> Hiyo
>> ikiwa kinyume kabisa na maazimio ya Umoja wa Afrika ambayo Nyerere
>> aliiasisi. Aliivalia njuga kampeni hii hadi kukusanya michango na misaada
>> isiyo ya hiari nchi nzima, na kuipeleka Biafra. Ilishangaza wengi duniani
>> kuwa Nyerere alikuwa anashadidia kuvunjika kwa taifa huru la Nigeria.
>>
>> Siri ilikuja kufichuka baadaye ilipothibitika kuwa kumbe mpango mzima
>> ulikuwa ni hila tu za Kanisa Katoliki zikisimamiwa na Nyerere, Houphouet
>> Boigny wa Ivory Coast na Rais Eyadema wa Togo. Hiyo ilishusha kwa kiasi
>> heshima na uadilifu wa Nyerere miongoni mwa Waafrika na vita hiyo ya
>> Biafra
>> ikisababisha vifo visivyo na lazima, takriban milioni moja na maafa
>> makubwa.
>> Kwa bahati, Nigeria kama nchi ikasalimika.
>>
>> Pamoja na mikenge yote hiyo, Mwalimu alisifika kwa msimamo wake, hususan
>> katika mambo ambayo aliyaamini. Alikuwa hatetereki asilani. Alipiga vita
>> ukabila kwa kuwastaafisha machifu wote nchi nzima baada tu ya Uhuru.
>> Alifanya juhudi za makusudi kuimarisha na kuirasimisha Lugha ya
>> Kiswahili.
>> Aligundua baadaye umuhimu wa lugha hii kama nyenzo ya kuimarisha utawala
>> wake. Alipiga vita rushwa na ufisadi bila ya kuchoka. Alitetea wanyonge
>> mpaka mauti yalipomkuta na hakusita kuwabamiza wale wote walionadi sera
>> za
>> kibaguzi. Na baada ya kustaafu, aligeuka mkosoaji mkubwa wa serikali hadi
>> kuchukiwa kwa uchokonozi wake dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka.
>>
>> Kiukweli kabisa, Mwalimu alikuwa na umahiri mkubwa kama mzungumzaji na
>> ufasaha wake wa lugha ulimbeba. Angeweza kusema chochote wakati wowote.
>> Na
>> wasikilizaji wakasikiliza na kumwelewa. Ni kipaji tu. Alipokuwa
>> akizungumza
>> wasiompenda walikuwa wanaungua kwa ghadhabu, na alipoamua kujibu mapigo
>> ya
>> mahasimu wake ilikuwa ni balaa, watu waliingia mitini. Cha kushangaza
>> zaidi
>> ni kuwa Kiswahili na Kiingereza ni lugha mbili alizozimudu kwa kina
>> lakini
>> zote hizo hazikuwa lugha mama kwake. Alijifunzia ukubwani kwa kujizatiti
>> sana.
>>
>> Lakini Mwalimu alitambulika kwa tabia yake ya uropozi. Alikuwa hamkopeshi
>> mtu na kwa hiyo tabia yake ilikuwa ni neno kwa neno. Kuna wakati mmoja
>> alikorofishana na Margaret Thatcher, Waziri Mkuu wa Uingereza aliyepita
>> na
>> kumbwatukia 'Bi Thacher anafanya uhuni na heshima ya taifa lake' au pale
>> alipomnanga Idi Amin na kumuelezea kuwa '… Amin ana kichaa
>> kilichosababishwa
>> na kaswende'. Ni kutokana na hulka hii basi haikushangaza kumsikia Ian
>> Smith, Waziri Mkuu dhalimu wa Rhodesia akimwita Mwalimu 'ibilisi
>> mbunifu'.
>>
>> Mwalimu, katika uhai wake ameandika vitabu vingi na tenzi na mashairi
>> pia.
>> Hata hivyo, aligoma kabisa kuandika kitabu kuhusu maisha yake yeye
>> mwenyewe.
>> Watu kadhaa wa karibu kwake walimsihi sana lakini wapi. Ni ngumu kuelewa
>> kwa
>> nini basi, Mwalimu ambaye alisikiliza sana dhamira yake katika kila jambo
>> alilotenda lakini kinyume chake aliishi maisha yake yote huku akiwaza
>> namna
>> historia itakavyomkaanga hapo baadaye.
>>
>> Kisiasa, Mwalimu ametuachia CCM iliyojaa wafuasi maamuma na mbumbumbu
>> wakiongozwa na genge dogo la watu wenye uchu wa madaraka wanaopenda
>> kujilimbikizia mali. Wazoefu wa kuimba nyimbo za kusifiana kwa vigelegele
>> na
>> makofi mengi. Chaguzi za Chama cha Mapinduzi zimegeuka gulio la kuuza na
>> kununua kura mchana kweupe. Na hao wanaojinasibu kuwa ni wafuasi wa
>> Nyerere
>> hutumia nukuu zake na wosia wake pale tu wanapokuwa na maslahi binafsi.
>> Hawa
>> hawakujifunza kitu kutoka kwa Mwalimu.
>> Hivi sasa kuna fukuto la mvutano wa kidini nchini. Waislamu wanalalama
>> kuwa
>> kwa makusudi Mwalimu alitumia urais wake kunufaisha ukristo na wakristo
>> katika teuzi za uongozi, nafasi za masomo na ugawaji wa keki ya taifa.
>> Mwalimu katuachia tatizo hili na sasa linatishia utaifa wetu.
>>
>> Na hivi tunavyoadhimisha miaka 13 ya kifo chake, mtu huyu ambaye
>> alionekana
>> kama vile anapiga vita udini, Kanisa Katoliki liko mbioni kumtakasa na
>> kumtawaza kuwa ni 'mtakatifu'. Hatua hii imezaa utata na maswali mengi.
>> Watu
>> wanauliza je, Kanisa lina ajenda gani? Nimalize kwa kuangalia utawala wa
>> takriban robo karne Mwalimu akiwa kiongozi wa nchi hii. Mwishoni, Mwalimu
>> alishitushwa sana na namna mambo yalivyokwenda segemnege, hakutarajia
>> kuwa
>> Watanzania wale ambao alidhani wamemuelewa kumbe walimpuuza. Walimsikia
>> lakini hawakumsikiliza. Aliangalia nyuma na kutazama uharibifu aliouacha
>> na
>> mambo yote yalivyoparaganyika. Alisononeka mno.
>> Mwisho wa siku Mwalimu hakuwa na marafiki wa kweli, familia yake
>> iliathirika
>> kutokana na kukosa malezi yake, umasikini nchini bado umetamalaki, ujinga
>> nao umejikita, huduma za afya zimedorora na hazitoshelezi, Muungano
>> unayumba
>> na rushwa na ufisadi vimeshamiri kila sekta. Kama vile madhila hayo
>> hayatoshi, CCM ilitupilia mbali zile tunu mbili za Nyerere, yaani siasa
>> ya
>> Ujamaa na Azimio la Arusha. Kwa Nyerere huo ulikuwa mithili ya uhaini,
>> aliiona CCM ikimsaliti angali hai.
>>
>> Kwa vile kila alichosimamia Nyerere hakikusimama badala yake
>> kiliporomoka,
>> Mwalimu alikufa akiwa na usongo mkubwa moyoni, Mwalimu aliaga dunia huku
>> akisononeka kutokana na kuangushwa na watu waliomzunguka. Nyerere
>> alikuwapo
>> na daima hakutokuwa na Nyerere mwingine. Ni dhahiri, Nyerere alikuwa ni
>> kitendawili.
>>
>>
>> Walewale.
>> ________________________________
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.





--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

1 comments:

  1. This is ALBERT HASTINE SERVICE, An International loan lending firm,We are
    investors /Loan lenders. We focus on startup funds, mortgage loans, Agricultural
    loans, Personal loans, Educational loans,e.t.c. Are you in need of a loan to
    pay your bills or for your child education? Are you in need of a loan to
    purchase a property or for project establishment? Are you in need of a loan
    for Agricultural purpose or for construction? Are you in need of a loan for
    Business expansion or startup? Have you been turned down by your bank or
    other lenders because of your credit facility? Fidelity Loan Agency
    is granting you the opportunity to actualize your dream.We offer all type of
    loans to interested persons for any purpose
    before any further process, you will be required to fill the following loan application form below and return if you are interested in a loan
    LOAN APPLICATION.
    Full Names:...........
    Loan Amount Needed:...
    Loan Duration:........
    Monthly Income........
    Next of kin...........
    Occupation............
    Company...............
    Phone number:.........
    Country:..............
    Address:..............
    State:................
    Hope to hear from you soon
    alberthastineservice@gmail.com

    ReplyDelete