Friday 19 October 2012

Re: [wanabidii] KAULI YA ZAWA UK JUU YA VURUGU ZANZIBAR

Abdalah, asante kwa wito huo mzuri. Hapa Dar es Salaam hali si shwari
vilevile. Kwa yote ambayo yametokea huenda yakaongeza 'suspicion' ya
undugu kati ya Waislamu na Wakristo na hasa kwa kuzingatia kuwa bado
nyumba za ibada zinaendelea kushambuliwa na vitisho vingine vya
umwagaji damu kutolewa.

On 10/19/12, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
> Jumuiya ya Wazanzibari waishio UK ZAWA UK inasikitishwa na matukio
> ambayo yanaendelea kutokea huko nyumbani Zanzibar yaliyoanza
> kujitokeza jana tarehe 17/10/2012 ambayo yamesababisha vurugu kubwa
> katika Miji ya Zanzibar na vitongoji vyake.
>
> Matukio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa maisha ya askari wa
> jeshi la polisi,mali za Umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya
> siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa Maduka, vyombo vya
> usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, pamoja na kuchomwa moto
> maskani za CCM
>
> Kutokana na vitendo hivyo, ZAWA UK kinaalaani vikali matukio hayo
> ambayo yamepelekea uvunjifu wa mkubwa wa amani ya nchi, na kusababisha
> hofu kubwa kwa raia pamoja na wageni wanaotembelea Zanzibar.
>
> Pamoja na vurugu hizo, ZAWA UK kimepokea kwa mshangao mkubwa taarifa
> ya Serikali ya Zanzibar pamoja na ile ya Serikali ya Jamhuri ya
> Muungano kupitia jeshi la Polisi iliyoeleza juu ya kutoweka kwa Sheikh
> Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya kutatanisha.
> Katika Taarifa hiyo, Serikali zimethibitisha kuwa vyombo vyake vyote
> vya ulinzi havijamkamata Sheikh Farid, jambo ambalo limezidisha hofu
> na wasi wasi kwa wananchi juu ya mahali alipo na hali yake kiongozi
> huyo wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar.
>
> ZAWA UK kinaziomba Serikali zote mbili kuendeleza juhudi zote za
> kuhakikisha taarifa za ukweli na za uhakika zinapatikana juu ya kadhia
> ya kutoweka kwa Sheikh huyo kwani Sheikh Farid ni raia wa nchi hii, na
> Serikali hii ni kwa ajili ya wananchi wote, ili kuondoa hofu na wasi
> wasi ambao umesababisha baadhi ya wananchi kujengwa na dhana mbaya.
>
> Vile vile ZAWA UK kinawaomba wananchi wote kwa ujumla kutojiingiza na
> kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya
> nchi yetu.
>
> Sote kwa pamoja tukatae kabisa kujihusisha na vitendo vya kuleta
> vurugu kwa vitendo na kauli zitakazopelekea kuiondolea sifa njema nchi
> hii ya Zanzibar.
>
> Mwenyekiti ZAWA UK
>
> Hassan Mussa Khamis
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment