Friday 19 October 2012

Re: [wanabidii] Kauli Ya Kamishna Wa Polisi Zanzibar Kuhusu Askari Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Aliyeuawa Leo Kwa Kukatwa Mapanga! - Mwanzo

Madame 
Umeongea embryo nilitegemea viongozi wetu  wakuu wangeyaona na kuyakemea Sikh nyingi  sanaa.  Too bad viongozi wetu tunaodhani wameelimika wanaota urais badala  ya kuitetea Tanzania wanayotamani kuiongoza.  Nobody wants to be a president of an Afghanistan-like nation yet they sit back and do nothing when they swould be talking sense and doing something at these delicate times! Big shame!

Sent from Samsung Galaxy Note


-------- Original message --------
Subject: Re: [wanabidii] Kauli Ya Kamishna Wa Polisi Zanzibar Kuhusu Askari Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Aliyeuawa Leo Kwa Kukatwa Mapanga! - Mwanzo
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
CC:


 
Ndio maana mkoloni aliweka kota za watumishi wa serikali pamoja na polisi maeneo yao maalum. Tumeuza au tumezibomoa. Ujamaa ulitufanya tuamini kuwa kuishi pamoja na viongozi, na askari wa aiza zoote ni salama na udugu. Sasa askari amepanga uswahilini na anapita vichochoroni, au magistrate aliyemfunga mwana uamsho kajenda huko au amepangiwa huko ambako wenye vurugu wanaishi. Au, nyumba aliyopanga mmiliki ni mfuasi wa uamsho. Wakimkosa yeye watawapata wana familia yake. Tutayaangalie haya baadae National housing iangalie suala la kujenga quarters maalum kwa askari polisi na FFU, mahakimu na wengineo kuwalinda isije ikawapata haya.
 
Kinachosikitisha au kuchekesha ni taarifa za kuvunja bar  na maduka ya pombe na kuondoka na bidhaa hizo au chupa badala ya kuzivunjia hapo hapo. Mtu unajiuliza-huu kweli ni ugomvi wa dini? Mbona madai ni mengi sio tu mtoto kukojolea msaafu? inakuja kuchana biblia, kuondoka na vitu vya kanisani kupeleka nyumbani (kumkaribisha bwana Yesu na kumpeleka home kwako), kuvunja duka la kitu haram (pombe za chupa etc) na kuchukua kupeleka home (kumpeleka shetani na haram home). Mara kudai aliyekojolewa atolewe auawe lakini yupo chini ya sheria. hata hivyo wakwako aliyefanya fujo na kuchana biliblia, kuchoma kanisa au kuhamasisha hayo atolewe asidhuriwe awe huru kwa dhamana (ana haki ya kuua na kuvunja mali, ni juu ya sheria). Mashule ya wakristu yaweke ulinzi kuokoa maisha ya watoto. Hii huko ZNZ itafikia nyumba hadi nyumba na itahama kutoka kukojolea msaafu itaingia hawatoacha hadi ZNZ ijitenge. Hii haitakwisha, watauawa wengi sana pamoja na ndugu zetu waislamu kuchinjana wenyewe kwa wenyewe kama hivi alivyouawa huyu askari wa dini hiyo hiyo. Itafikia huenda hata kuchomeana misikiti kati ya uamsho na wasio uamsho. Ni sisi wenyewe haina mkono wa wageni ila wameua tourism ZNZ. Wafanya biashara wanaathirika, booking za ndege na hoteli pesa itabidi zirudishwe, ajira na kipato vinaathirika. tumeyaona ya Libya, Misri, Congo, Rwanda lakini hatujifunzi. Tunaona afghanistani wamefikia hata kukataa elimu dunia (watoto wasisome shule za kizungu bali quran tu) na ambapo dunia sasa ni utandawazi. Imehama toka kwa wamarekani ipo wenyewe kwa wenyewe wa dini moja. Tusifike huko. wasomi wa dini hii na viongozi wa dini wasaidie kuelimisha.  Mungu atusaidie. Inauma kuona wamemuua asiye na hatia. Wazazi DSM tuna wasiwasi na watoto na wajukuu wasomao mjini-temeke, chang'ombe,Tegeta etc usafiri tabu na  kama watarudi salama daily.

--- On Thu, 18/10/12, Magiri paul <kiganyi@gmail.com> wrote:

From: Magiri paul <kiganyi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Kauli Ya Kamishna Wa Polisi Zanzibar Kuhusu Askari Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Aliyeuawa Leo Kwa Kukatwa Mapanga! - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 18 October, 2012, 15:09

Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6.30 usiku katika eneo la Bububu.
 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema mauaji hayo yamesababishwa na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid Hadi usiku wa kuamkia jana.
 Kamishna Mussa amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu waliofanya mauaji ya Coplo Saidi Abdulrahaman ili kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani kama sheria za nchi zinavyowaelekeza.

http://wotepamoja.com/archives/9134#.UIAbhU7blVg.gmail
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
  

0 comments:

Post a Comment