Friday 19 October 2012

Re: [wanabidii] Hali ya Usalama Jijini Dar es salaam

Thanx Yona,ila bado nina wasiwasi na utendaji wa vyombo vyetu vya ulinzi.haya matatizo hayajaanza leo na sijawahi kusikia serikali ikichukua hatua kali za kusitisha na kuzuia kutotokea tena.kwa mtu mwenye akili timamu utajua kuwa madhara ya fujo hizi ni makubwa kwani yanajenga wasiwasi,na kutokuaminiana sasa hiyo ni hali mbaya sana ni ufa huo. Viongozi ni vema wawe situational kurespond ktk matatizo kwa uzito unaostahili.
Unajua ss wenye watoto huwa mtoto anaweza fanya kosa ukamwangalia tu usoni yeye atajua amefanya kosa ataacha, lakini makosa mengine itakubidi mzazi umwite mtoto karibu uongee nae na kumkanya kwa ukali ili ajue ni kosa na asirudie, na kwa makosa mengine kiboko ni vema kikatumika.vivo hivyo viongozi wa nchii warespond kwa changamoto zinazotukabili kwa uzito unaostahili sio kufanya usanii,kimsingi uzembe wao ndo umetufikisha hapa
Download the latest BlackBerry® applications from Zantel on www.zantel.com/zantelapps

From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Fri, 19 Oct 2012 16:51:51 +0300
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>; Wanazuoni<wanazuoni@yahoogroups.com>; <wanakenya@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Hali ya Usalama Jijini Dar es salaam

Hali ya Katikati ya Jiji la Dar es salaam


Sasa hivi hakuna daladala inayokuja posta mpya wala zamani zote zinaishia huko njiani au haziji kabisa , askari wametanda kuanzia wizara ya mambo ya ndani na maeneo mengine ya jirani  .


Watu wengi wameshaenda majumbani kwao na wengine ndio wanaendelea kwenda majumbani kwao kuhofia usalama wao na wa mali zao .


Tusiwe na shaka vyombo vyetu vya usalama viko makini na vinatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi ingawa wakati mwingine wajibu unaweza kuzidi kimo na kulazimika kutumia nguvu ya ziada kama inavyoonekana kwa kipindi cha sasa tunapoelekea jioni

.

Tuache propaganda hii ni nchi yetu sote , tupiganie amani na utulivu wa nchi yetu , hakuna atakayekuja kutufundisha wala kutuletea amani , upendo na mshikamano wetu .


Kama una mhisi mtu kuhusika katika vitendo hivi toa taarifa kwa vyombo vya usalama na vitachukua hatua stahiki .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment