Tuesday, 1 July 2014

Re: [wanabidii] Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL, (Tegeta Escrow account) ni mali ya umma

Kwa kauli hii ya zitto sasa kafulila nimemwelewa. Hoja ya kafulila ilipaswa ielezwe kwa ufasaha na ieleweke vizuri. Lakini pia nimepata picha kwanini baada ya waraka wa zitto maswi kawa mkwezi dhidi ya tumbili.

Je kama tumbili anawapa tabu hivi, manyani yakiingia sipatachimbika? Au yameshapozwa ndo maana yametulia wala hayajikuni.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, June 29, 2014 12:02:58 PM GMT-0700
Subject: [wanabidii] Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL, (Tegeta Escrow account) ni mali ya umma

NA ZITTO Z KABWE

Kwa mara nyingine serikali kupitia viongozi na watendaji wake akiwamo
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba kiasi cha Dola za
Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika 'Tegeta Escrow
Account' si mali ya serikali na hivyo si mali ya umma. Akaunti hiyo
ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na kampuni ya Independent Power Limited
(IPTL).

Kwa bahati mbaya sana viongozi wa serikali wamekuwa wakiendelea kurudia
kuueneza huo uongo kwamba fedha hizo si mali ya umma. Inasikitisha pia
kwamba vyombo vya habari vimekuwa navyo vikibeba na kusambaza huo uongo
bila kuhoji na kuchunguza. Inashangaza sana pia asasi za
kiraia nazo zimekaa kimya. Inatisha na kushangaa tena kuona wapinzani
wakimwachia suala hili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David
Kafulila, pekee wakati mapambano dhidi ya rushwa ni ajenda kuu ya
wapinzani. Kafulila amekuwa akiendelea kuhoji suala hilo bungeni peke yake
bila kupata kuungwa mkono na kupewa msaada wa aina yoyote kutoka kwa
wenzake wa kambi ya upinzani bungeni.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilielekeza kuwapo kwa ukaguzi
maalumu kwenye akaunti hiyo ya Tegeta escrow account iliyokuwa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) kwa kuwa ndani yake kulikuwapo fedha za umma. PAC haina
sababu yoyote ya kufuatilia fedha za watu binafsi. Mwaka 2009 iliyokuwa
Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilitoa maelekezo kwa BoT
kutothubutu kutoa fedha hizo. Agizo hilo la POAC lilitokana na sababu
kwamba fedha hizo zilikuwa ndani ya hesabu za Tanesco.

Akaunti ya 'Tegeta escrow' ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana
kuhusiana na gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na
kuuzwa kwa TANESCO. Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika
uamuzi wake wa Februari, 2014 ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco
walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL. Kwa
uamuzi huo ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti
hiyo maalumu ya escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya
hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.

Hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Disemba 2012 za Tanesco zinaonyesha wazi
kwamba fedha hizo ni mali ya shirika hilo la umma linalomilikiwa na
serikali kwa asilimia mia moja. Fedha za kampuni ni suala la kisheria kama
inavyobainishwa katika sheria ya kampuni ya mwaka 2002.

Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuaje serikali ianze kudai kwamba fedha
hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi
zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa
asilimia 100? Ni lini fedha hizo zimekoma kuwa za umma? Je ni baada ya
baadhi ya watendaji wa serikali kula njama za kuzichukua fedha hizo kwa
kushirikiana na 'mwekezaji' aliyechafuka kwa ufisadi duniani?

Serikali inadanganya waziwazi kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma. Umma
una haki ya kukumbushwa kwamba madai hayo yalitolewa pia katika lile sakata
la ufisadi maarufu wa EPA unaofanana kwa kila hali na huu wa sasa wa
'Tegeta Escrow'.

Hoja nyingine ni kwamba, Mbunge Kafulila alisema kwamba Jaji Utamwa wa
Mahakama Kuu ya Tanzania hakutoa uamuzi wa kuchukuliwa fedha kutoka akaunti
ya 'Tegeta Escrow'. Nimepitia kwa makini hukumu ya Jaji Utamwa na kubaini
kwamba hakuna popote alipotaja akaunti ya 'Escrow'. Hata hivyo, nilipopitia
muhstasari wa kikao kati ya TANESCO, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini,
ndipo kwa mara ya kwanza nikakuta wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai
kwamba fedha zote za 'Tegeta Escrow' zipewe kampuni ya PAP (inamilikiwa kwa
asilimia 50 na Harbinder Singh na 50% na Simba Trust iliyosajiliwa
Australia). Hiki ndicho kikao kilichofanya maamuzi ya kuiba na kugawana
wenyewe fedha hizo (Hukumu ya Jaji Utamwa na muhstasari wa kikao
vinaambatanishwa).

Wote waliohudhuria kikao hicho kilichojipa mamlaka ya kutafsiri hukumu ya
Mahakama Kuu, wanapaswa kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa
sheria zilizopo. Inawezekana vipi uamuzi wa mahakama ukatafsiriwa na kikao
cha Wizara? Muhstasari wa kikao hicho ndio uliowasilishwa Benki Kuu (BoT)
kuhalalisha madai kwamba fedha hizo lazima zitolewa kutoka akaunti ya
Escrow.

Fedha zinazohusiana na akaunti ya Escrow ni Dola za Marekani milioni 250,
katia ya hizo Dola milioni 122 zilizokuwa BoT zimeshatolewa na kiasi
kilichosalia Dola milioni 128 zitalipwa na Tanesco kutokana na fedha zake
kwa madai ya kushindwa kulipa kwa wakati. Fedha zilizolipwa ni zile ambazo
zimetoka Wizara ya Nishati na Madini ambayo kisheria ndio walipaswa kulipia
gharama za uzalishaji umeme (capacity charge) fedha zilizotoka kwa walipa
kodi.

Ikumbukwe kwamba uhamishaji wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda PAP
umeambatana na nyaraka za kughushi kutokana na kutokuwepo kabisa kwa
uthibitisho wa cheti halisi cha hisa (share certificate) kutoka kampuni ya
Mechmar kwenda kampuni ya Piperlink. Nyaraka za TRA zinaonyesha kwamba hisa
hizo (70%) ziliuzwa kwa Shilingi za Kitanzania milioni sita (6) tu. Na bado
hakuna ushahidi kuonyesha kwamba uhamishaji huo wa hisa ulipata baraka za
mamlaka husika kama inavyotakiwa na sheria za nchi.

Wakati huyo anayejiita mmiliki mpya wa IPTL aliposaini mkataba wa kuchukua
fedha kutoka akaunti ya Escrow zilizokuwapo BoT, hakuwa mmiliki halali
kisheria kwani kodi ililipwa siku moja baada ya wao kupokea fedha kutoka
BoT. Sheria inataka kutolewa kwa cheti na Kamishna wa TRA kama uthibitisho
kwamba kodi yote imelipwa ipasavyo (Sheria ya Fedha ya 2012 kifungu cha 29).

Ni nani wamiliki wengine wa kampuni ya PAP? Uchunguzi ni muhimu ukawalenga
vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara ya
Nishati na Madini.

Inapaswa tutafakari kuona kwamba Harbinder Singh aliyechukua fedha za
Escrow, anamiliki vitalu vya mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo
HydroTanz ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na anwani sawa na
ya kampuni ya Simba Trust. Kitalu hicho cha mafuta kinaitwa 'Mnazi Bay
North', jirani kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani Mtwara.

Tunatarajia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), atafichua
ukweli wa sakata hili na TAKUKURU itawafikisha mahakamani wahusika bila
kujali nyadhifa zao serikalini.

Kauli ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kwamba
kuna watu waliokula rushwa na kwamba nyaraka zinazotajwa ni karatasi za
kuuzia vitumbua, ni kauli zenye kuonyesha kutapatapa kwa watendaji
serikalini. Hakuna hata mahali pamoja ambapo nimemtaja mtu kuwa ni mwizi
zaidi ya kuwasilisha hoja zinazohitaji majibu mwafaka na si matusi, vitisho
na tuhuma za kuzusha. Nyaraka za TRA haziwezi kuwa za kufungua maandazi
kama ambavyo hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu haiwezi kuwa karatasi za
kufungia maandazi na badala yake ni nyaraka halali zinazohitaji maelezo
kutoka kwa viongozi na watendaji wa serikali badala ya kuropoka na
kuporomosha matusi.

Hali kadhalika, Bunge lina kila sababu kupitia sheria yake ya Haki, Maadili
na Madaraka ya Bunge kulinda hadhi yake kutoka kwa watendaji kama Maswi
ambao wanatoa matamshi ya kuonyesha kwamba chombo hicho ni chombo cha watu
wasiofaa na kwamba watu wanaofaa wanazungumza nje ya Bunge. Maswi na
wengine kama wana ushahidi wa rushwa dhidi ya mbunge ama yeyote hawapaswi
kupayuka ovyo bali kwa nafasi zao wanaweza kuwasiliana na vyombo vya dola
kama TAKUKURU na polisi ili wachunguze na kuchukua hatua kama ambavyo
vinawachunguza wao.

Kauli ya Maswi kwamba "wanaume" hawazungumzi ndani ya Bunge si tu
udhalilishaji wa chombo hicho bali pia inaashiria ugonjwa wa mfumo dume
uliotawala miongoni mwa viongozi wetu kwa maana kwamba wanaume ndio wenye
hadhi, uwezo na heshima na wanawake ni dhaifu na wasiostahili heshima.
Tufumbue macho tuone na tuondoe hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi,
chuki na misimamo yetu ya kisiasa. Tuwe wazalendo ili tuweze kusimamia
utaifa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment