Wednesday 30 July 2014

[wanabidii] Chama cha ACT-Tanzania hakina Mfadhili Mkuu

Chama cha ACT-Tanzania hakina Mfadhili Mkuu

1.     Katika toleo lake la siku ya Jumatano ya tarehe 30 Julai 2014 Gazeti la Tanzania Daima limechapisha habari zilizodai kuwa mwanasiasa moja maarufu hapa nchini ndiye mfadhili mkuu wa Chama cha ACT-Tanzania.

2.     Kwa niaba ya uongozi wa ACT-Tanzania, na kwa nafasi yangu kama Mtunza Hazina na Mhasibu Mkuu wa ACT-Tanzania, napenda kuwataarifa wanachama na wapenzi wa chama na wananchi kwa ujumla kuwa taarifa hizi ni uzushi na uwongo wenye lengo la kuchafua taswira ya chama cha ACT-Tanzania. Napenda kuutaarifu umma kuwa moja ya misingi mikuu ya ACT-Tanzania ni uadilifu na uwazi. Kwa misingi hii, vyanzo vya mapato na matumizi ya ACT-Tanzania yapo wazi kwa mtanzania yeyote anayetaka kujua ukweli.

3.     Tangu chama kianzishwe mwezi Januari mwaka huu, kimeshapokea na kutumia jumla ya shilingi 74, 857,000/= (milioni sabini na nne laki nane na elfu hamsini na saba) zilizochangwa na wanachama, wapenzi na wananchi wasiopungua 50 wanaouunga mkono misingi ya chama hiki. Taarifa ya kwanza ya fedha ya chama iliwasilishwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya ACT-Tanzania katika mkutano uliofanyika Mjini Singida tarehe 25-26 Julai 2014. Kwa mtanzania yeyote ambaye angependa kuona orodha ya watu waliokichangia chama anakaribishwa kufika ofisi ya Makao Makuu iliyopo Ubungo National Housing mkabala na Hoteli ya Royal Njombe.

Pamoja na salamu za uzalendo za ACT-Tanzania

Peter Mwambuja, PGDA, CPA (T)

Mtunza Hazina na Mhasibu Mkuu wa ACT-Tanzania.

Imetolewa Jumatano 30 Julai 2014 



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment